Home Michezo Kimataifa Van Gaal anafurahisha mdomoni kuliko uwanjani

Van Gaal anafurahisha mdomoni kuliko uwanjani

295
0
SHARE

Louis-van-Gaal-649404MWANDISHI WETU NA MITANDAO

TANGU atue katika klabu ya Manchester United kuchukua mikoba ya David Moyes, Louis van Gaal, amekuwa ni mtu wa kufurahisha sana vyombo vya habari na vituko vyake na hilo ndilo alilofanikiwa zaidi England kuliko kazi yake ya kukinoa kikosi cha United msimu huu.

Mdachi huyo amegeuka lulu kwa waandishi wa habari nchini humo kwa kauli zake za kufurahisha, ambapo kauli yake ya mwisho ilikuwa ni baada ya mchezo dhidi ya Leicester wikiendi iliyopita alipovuta nywele za mwandishi wa habari aliyemuuliza kuhusu tukio la Marouane Fellaini kuvutwa nywele zake wakati wa mchezo huo.

Kuhusu tetesi kuondoka United

“Nadhani sijawahi kutamka hivyo. Umetengeneza habari zako. Kwa hiyo ngoja nikwambie sitafanya hivyo kwa sababu ni kitu cha ajabu kwangu lakini unaweza kuandika.”
“Ni mara ya tatu mnasema nitafukuzwa lakini bado nipo. Nina furaha kushiriki nanyi (mkutano na waandishi wa habari). Kila mtu anauliza bila heshima. Kila mara nimekuwa mtu wa imani.
“Unapopoteza mchezo ni jambo baya. Nilitabiri kabla ya kukabiliana na Southampton. Sasa sitapoteza tena kwa sababu ni mara ya nne hii mnasema nimefukuzwa. Labda itakuwa kweli.”

Malengo yake na United

“Natumai nitamaliza kazi yangu hii kwa ubingwa. Hiyo ni kauli mbiu yangu na itakuwa vizuri sana kwa kuwa hata Manchester United wanaitumia pia.”
“Mimi sio kocha wa muda mfupi. Mara zote ninawaza mafanikio ya muda mrefu.”
“Najiamini kwamba nitafanikiwa hapa.”
“Nimesaini mkataba wa miaka mitatu. Niamini, nitamaliza vizuri hapa (United).”

Kuhusu falsafa yake

“Unatakiwa kuendana na falsafa yetu na hilo lilikuwa ni gumu kwa (Angel) Di Maria.”
“Kitu cha muhimu ni kwamba, nawanoa wachezaji kwenye ubongo wao na sio kwenye miguu. Hii ni nguvu ya ubongo.”
“West Ham wamecheza asilimia 71 ya mipira mirefu na sisi tumecheza asilimia 49. Chukua hiyo alafu nenda kwa Big Sam (Alardyce, kocha wa West Ham.”
“Tayari nimetumia mifumo takribani sita na bado naendelea kutafuta uwiano sawa kwenye hii timu.”
“Leo tumecheza vizuri sana ila tumesahau tu namna ya kufunga. Tunatakiwa kuwa na kasi zaidi.”
“Nimefanya kazi ya ufundishaji kwa kipindi cha miaka 35 nikitumia mfumo wa kushambulia.”

Baada ya mechi sita bila ushindi

“Najua kwamba imani kwa kocha ni kitu cha muhimu sana. Na kama ukipoteza michezo, imani hiyo lazima ishuke. Ndicho kinachotokea sasa hivi. Siwezi kufumba macho yangu.”

Akapoteza tena kwa Southampton

“Nina huzuni kubwa sijaweza kuwaridhisha mashabiki. Walikuwa na matarajio makubwa na mimi lakini siwezi kufanya hivyo sasa. Nimesikitishwa na hilo.”

Kuhusu mashabiki kumtaka atimke

“Mashabiki wanatakiwa kutoa ushirikiano la sivyo wataifanya kazi hii iwe ngumu kwa wachezaji.”

Kumuita mwandishi ‘bonge’

“Unamwita Wayne Rooney ni bonge, mimi simwiti hivyo (akimnyooshea kidole), wewe pia ni bonge!”

EPL kutokuwa na mapumziko kipindi cha baridi
“Hakuna mapumziko wakati wa baridi na nadhani hili ni jambo la ajabu kabisa katika tamaduni hii.”
“Nina mke, watoto na wajukuu na sitaweza kuwaona katika sikukuu ya Krismasi.”

Siku moja kabla ya usajili wa Anthony Martial
“Sidhani kama tunahitaji straika. Nina machaguo mengi katika eneo hilo.”

Tukio la Felaini kuvutwa nywele

“Ukiangalia namna Huth alivyomfanyia Fellaini ni penalti kabisa. Nivute nywele zako? (anamvuta) Umejisikiaje? Nywele zako ni ndogo sana.
“Nadhani hakufanya jambo la ajabu sana (Fellaini kumpiga Huth na kiwiko baada ya kuvutwa nywele). Kila binadamu anapovutwa nywele basi lazima afanye vile.
Ashakum si matusi. “Kuvutana nywele hufanyika wakati wa tendo la ndoa.”