Home Makala Kumtii Mungu ni wajibu wetu sote

Kumtii Mungu ni wajibu wetu sote

351
0
SHARE

MUNGU amewachagua baadhi ya watu kuwa watu bora hapa duniani, Rais John Magufuli wewe ni chaguo la Mungu kuwa mtu bora duniani na mbinguni. Mungu amekupa Tanzania ili uweze kutimiliza ubora wako hapa duniani.

Rais wa zamani Haile Selassi wa Ethiopia alikuwa na washauri 102, lakini hao wote yeye ndie aliwashauri badala ya wao kumshauri… Hakika hakupenda wala kupokea ushauri uliokuwa kinyume na afikiriavyo yeye. Hakika Mungu alikuwa na makusudi nae ili taifa lake liponywe.

Hata taifa lilipoingia katika hali ngumu ya njaa na chuki kubwa dhidi ya utawala wake, washauri wake waliendelea kumsikiliza yeye apendacho, na zaidi walimwambia “Jah anakupenda sana, na watu wakushi kwa wahabeshi wanakupenda sana”…. Taifa likapona.

Mfalme Docomo Solon wa Nodi alisema hivi siku ya kumuusia mwanamfalme wa Ukalidayo, ” kanyo la machweo, ni tiba la mawio”

Watu ni watu, hadhira zao hubadilika kadili kope zao zifumbapo na kufumbua. Rais Magufuli, Mungu ana makusudi na wewe ndio maana kakupa Tanzania, si kwamba Watanzania milioni hamsini ni wajinga, la hasha! Sauti ya mmoja ni twezo la maelfu.

Watu hawa wana Mungu, ni Mungu yuleyule aliyekupa nchi ya Tanzania, ni Mungu yule yule aliyekubarikia uitende kazi yake. Na ni Mungu yule yule anayewaongoza washauri wako…

Hongera sana kwakununua ndege, walau sasa tunasimama kama taifa..  Kenya, Rwanda , na Ethiopia zinashindana kununua Airbus A380 . Tanzania imenunua ndege mbili kutoka Canada zenye  Mapangaboi, inasemwa hata rangi ndio vinapakwa. Safari zitakuwa kuanza Dar es salaam hadi Mwanza saa tatu na nusu.

Mungu asipoulinda Mji wake Waulindao wanakesha bure!

Yericko Nyerere,

Kigamboni, Dar es salaam