Home Michezo NI VITA YA KANUNI AU MAPATO?

NI VITA YA KANUNI AU MAPATO?

377
0
SHARE

NA GEORGE KAYALA

RATIBA ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, inaonyesha kwamba mwishoni mwa wiki hii, Azam itakuwa mwenyeji Simba. Mchezo huu ni moja ya michezo mikubwa katika Ligi ya Tanzania hasa kutokana na ukweli kwamba timu hizo licha ya upinzani lakini ni miongoni mwa timu tatu zinazofukuzana kuwania ubingwa.

Ikiwa imebaki siku moja tu, mchezo huo kucheza bado kumekuwa na mvutano mkubwa mkubwa baina ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wenyeji wa mchezo huo Azam FC juu ya uwanja wa kutumika kwa mchezo huo.

Wenyeji Azam FC wanatumia wanataka mchezo huo uchezwe kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex, ulipo Chamazi, nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam, wakati TFF wao wakitaka mchezo huo uchezwe kwenye uwanja wa Uhuru au usogezwe mbele ili uje kufanyika uwanja wa Taifa.

Hoja za TFF

TFF kama wasimamisi wa soka la Tanzania Bara, wamekijikita katika kuelezea sababu za kuisalama kwamba uwanja huo ni mdogo sana ilinganishwa na mashabiki wa timu kama Simba na kwamba uwanja huo haufai kutoka kwa mechi hiyo kwa sababu ni mechi kubwa katika ligi ya Tanzania.

Kinachozungumzwa na TFF ni sahihi kwa upande wao, kweli uwanja wa Azam Complex unaingiza watazamaji 7,000 tu, hivyo kimsingi unaweza usitosheleze mahitaji ya mechi hiyo hasa kwa kuwa Simba ina mashabiki wengi mno jijini Dar es Salaam ambao wangependa kuitazama mechi hiyo uwanjani.

Lakini pamoja na usahihi huo wa suala la usalama, lakini hakuna kanuni inayokataza mechi hiyo kufanyika katika uwanja huo kutokana na ukweli kwamba uwanja huo umekidhi vigezo vyote vya kimataifa vya kuufanya utumike katika michuano ya kimataifa inayotambuliwa na mashirikisho ya juu kwa maana ya CAF na FIFA.

Hoja za Azam FC

Kimsingi Azam wamejikita kwenye kanuni za TFF, CAF na FIFA ambazo zinaruhusu timu kucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani hasa kama uwanja huo unakidhi vigezo vyote. Uwanja wao wa Azam Complex umetimia kwa kila kitu hivyo hawaoni sababu nyingine inayozizuia timu zingine zisicheze kwenye uwanja huo wakazi zingine zinakwenda.

“Tuna uwanja uliotimia, hilo suala la usalama tunajiuliza linatoka wapi? TFF isitumie kigezo cha usalama kuficha mambo au kufanya mambo kwa mazoea, ikiwa mechi zetu zote za kimataifa tunacheza pale iweje mechi za Yanga na Simba zisichezwe pale?” anahoji Saad Kawemba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam.

Anasema hoja ya TFF ni zaidi ya usalama lakini hawataki kiweka wazi, na kimsingi Azam hawatakubali suala hilo lifanyike kwa mazoea kwani wanachokifahamu ni kwamba kanuni zimewaruhusu kutumia uwanja huo na hakuna pingamizi lingine na kwamba ofisa usalama wa TFF anapaswa kutoa ripoti ya kweli kabisa juu ya hali ya usalama.

“Kama uwanja wa taifa kunatumika polisi 100, sisi Azam tuko tayari kulipa askari 200 zaidi kwa gharama zeti ili waje kulinda huo usalama unaosemwa,” anasisitiza Saad.

Hoja zilizo nyuma ya Pazia za Simba na TFF

Kutokana na malumbano hayo, RAI limekwenda mbali zaidi na kuangalia nyuma ya pazia kuna kuna jambo gani la msingi? Rai limebaini kwamba Simba na TFF wamekuwa na ajenda zaidi ya suala la usalama.

Vyanzo vya RAI hili vimebainisha kwamba, kwa sasa Simba kala klabu haiku sawa kiuchumi hivyo wanaona kutumia uwanja wa Azam Compelx kutawanyima mapato ambayo yanaweza kusaidia baadhi ya shughuli za uendeshaji wa klabu hiyo.

“Ni kweli viongozi wa Simba na walikutana na baadhi ya viongozi wa TFF na walikubaliana mamboa kadhaa ambayo baadaye waliwashirikisha Azam lakini Azam walikataa kutokana na ukweli kwamba hivi sasa Azam wanataka kutumia uwanja wao, kutokana na hilo kulikuwa kunafanyika mipango ya kubadilisha uenyeji wa mechi hiyo ili Simba iwe mwenyeji katika mechi hii ya kwanza kisha mechi ijayo ya raundi ya pili Azam ndio iwe mwenyweji,” kilisema chanzo chetu.

Alisema kwamba mpango mzima ulioko nyuma ya pazia ni mapato na si jambo lingine lolote na kwamba Simba iko yatari kwenda kucheza Chamazi lakini katika mchezo wa pili na ndiyo maana wamezungumza na TFF ili kubadili uenyeji wa mezi hiyo.

“Ilitakiwa TFF wawasiliane na Azam na wake meza moja pande zote tatu kwa maana ya Azam, Simba na TFF, lakini inaonekana kama vile TFF imeipuuza Azam na baada ya kujadili na Simba wanaona wamemaliza hili ndiyo linaonekana kuwa tatizo maana Azam hawakubali,” alisema.

Madai hayo japo yalikanushwa na Ofisa Habari wa wa TFF, Alfred Lucas, lakini alisema kwamba wameshawaita Azam na kuzungumza na kwamba suala hilo limewekwa sawa hivyo mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru kwa tarahe iliyopangwa.

“Madai mengine siwezi kuyazungumzia, lakini ninachoweza kukuambia ni kwamba leo hii (Jumanne) tumezungumza na viongozi wa Azam, na tumekubaliana juu ya mambo yote ya msingi na mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Uhuru,” alisema Alfred.

Mechi hiyo itakuwa ya 16 kuzikutanisha timu hizo kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania tangu Azam ilipopanda msimu wa 2008/09.  Katika mechi 15 zilizopita Simba imeshinda mechi saba, Azam imeshinda mechi nne huku zikitoka sare mara nne.