Home Makala EAC inalo jukumu la kuwadhibiti Al-Shabaab

EAC inalo jukumu la kuwadhibiti Al-Shabaab

323
0
SHARE

NAIROBI, Kenya

KUNDI la kigaidi la Al-Shabaab, limekuwa kero na mateso kwa wananchi wa Kenya hasa wale wanaoishi katika mji wa Mombasa.

Limekuwa jambo la kawaida kwa askari wa kundi hilo kuvamia makazi ya watu na kuua raia wasiokuwa na hatia na wakati mwingine kupora mali na kuwafanyia vitendo vya kidhalimu.

Mwendelezo wa mateso haya kwa wananchi wa Kenya unatajwa kuwashangaza wafuatiliaji wa mambo hasa ya kiusalama, kwamba Kenya na nchi washirika ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameshindwa kabisa kulishughulikia kundi hili linalofanya mauaji mara kwa mara.

Mshangao huo umekolezwa na mauaji ya watu 12 waliovamiwa na watu wenye silaha na kushambulia hoteli iliyopo mjini Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Mauaji hayo yamedhibitishwa na msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ambaye alisema watu sita wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ya Bishaaro.

Wanaotajwa kutekeleza mauaji hayo wanaaminika kuwa ni Wanamgambo wa kundi la al-Shabaab, ambao walitekeleza  ukatili wao saa tisa usiku.

Walichokifanya ni kufyatua mabomu  madogo madogo  kisha walizama kwenye nyumba hiyo na kuanza kuwafyatulia risasi watu waliokuwemo ndani.

“Sehemu ya jumba iliporomoka, na kuua watu 12. Watu sita wametolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo wakiwa hai kufikia sasa,” ni kauli ya Kiraithe kupitia mtandao wa Twitter.

Wataalamu wa mabomu wanafanya uchunguzi kubaini ni vilipuzi vya aina gani vilitumiwa kutekeleza shambulio hilo.

Tayari kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo, mji wa Mandera umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa al-Shabaab, kundi linalopigana dhidi ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika taifa la Somalia.

Wanamgambo hao wamekuwa wakishambulia watu ambao si wa asili ya Kisomali, pamoja na mauaji hayo hivi karibuni kundi hilo lilishambulia na kuua watu sita baada ya kushambulia mtaa mmoja mjini Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Taarifa zinasema washambuliaji hao walivamia eneo lenye nyumba za makazi Bulla usiku wa manane.

Gavana wa jimbo la Mandera Ali Roba ameandika kwenye Twitter kwamba watu sita wameuawa na mmoja kujeruhiwa.

Amesema watu 27 kati ya 33 waliokuwa kwenye eneo hilo  wameokolewa na maafisa wa usalama.

Ingawa wachambuzi wa mambo wanasema hatua ya kundi hilo la kigaidi kuishambulia Kenya inatokana na hatuya yake ya kupeleka  vikosi vyake vya kijeshi nchini Somalia mwaka 2011 ikitaka kuzima mashambulizi ya mara kwa mara na kuisaidia serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo wafuatiliaji wa mambo sasa wanaliona suala hilo kama janga kwa Kenya na kwa nchi zote za EAC na kwamba ipo haja kwa nchi zote wanachama kuisaidia Kenya na Somalia kulitokomeza kundi hilo  ambalo mara kwa mara hutekeleza mashambulio nchini Kenya ikiwemo mauaji ya watu 67 katika maduka ya Westgate mjini Nairobi mwaka wa 2013.

Mwezi Juni mwaka huu, wanamgambo wa kundi hilo walishambulia gari ya polisi aina ya ‘Land Cruiser’ kilomita chache kutoka mji wa Mandera, na kuua maafisa watano wa polisi.

Mwaka uliopita al-Shabab walitekeleza mashambulizi katika chuo kikuu cha Garissa na kusababisha vifo vya wanafunzi 148

Al Shabaab ni nani?

Jina Al-Shabab linamaanisha Kijana kwa lugha ya kiarabu. Kundi hilo liliibuka kama tawi la vijana la muungano wa mahakama za

kiislmau ambao baadaye ulivunjika mwaka 2006, wakati ilipopigana na wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini Somalia kuunga mkono serikali iliyokuwa dhaifu.

 

Kuna taarifa chungu nzima kuhusu wapiganaji wa kiisilamu wanaokwenda Somalia kupigania Al Shabaab.

Kundi hilo limeweka sheria kali za kiisilamu katika maeneo ambayo linadhibiti ikiwemo kupigwa kwa mawe hadi kufa wanawake wanaodaiwa kufanya uasherati pamoja na kuwakata wezi mikono.

Udhibiti

Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti, wa miji mikubwa, bado linakita mizizi katika maeneo ya mashinani.

Lililazimika kuondoka katika mji mkuu Mogadishu, mwezi Agosti mwaka 2011 na pia kuondoka katika mji wa bandarini wa Kismayo mwezi Septemba mwaka 2012.

Kismayo ulikuwa mji muhimu kwa kundi hilo, ambao ulikuwa unawezesha bidhaa kuwafikia wapiganaji wa kundi hilo pamoja na kuwatoza watu ushuru kwa shughuli zao.

 

Na kama unavyofahamu Kundi hilo  la wapiganaji wa kisomali la al-Shabaab, limevamia jumba la kifahari lenye maduka na mikahawa nchini Kenya. Al Shabaab lenya mizizi yake nchini Somalia, limeweza kuondolewa kutoka miji mikubwa ya Somalia ikiwemo Mogadishu na sehemu zengine za Somalia, ingawa bado linasalia kuwa tisho kubwa kwa kanda nzima.

Hizi ni silaha za Al Shabaab walizonasa wanajeshi wa AU

Muungano wa Afrika, ambao unaunga mkono juhudi za majeshi ya serikali, ulisherehekea ushindi huo ingawa al-Shabab hunfanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kujitoa mhanga mjini Mogadishu na kwingineko.

Wadadisi wanaamini kuwa al-Shabab limeanza kufanya mashambulizi ya kuvizia baada ya kushindwa na majeshi ya Muungano wa Afrika wanaotumia nguvu dhidi yao.

Lakini linakabiliwa na tisho kubwa kutoka kwa wanajeshi wa Kenya walianza hatarakti zao dhidi ya kundi hilo kuanzia mwaka 2011.

Kenya ilituhumu wapiganaji wa al-Shabab kwa kuwateka nyara wanajeshi wake pamoja na watalii na sasa wamekuwa katika msitari wa mbele kupambana na kundi hilo la kigaidi.

Wakati huo, wanajeshi wa Ethiopia waliweza kukabiliana na wapiganaji hao na kudhibiti miji ya Beledweyne na Baidoa.

Kiongozi wake

Ahmed Abdi Godane ndiye kiongozi wa kundi hilo. Anajulikana kama Mukhtar Abu Zubair, na anatoka katika jimbo la Somaliland.

Kumekuwa na taarifa za mgawanyiko katika kundi hilo, ambazo hata hivyo zinapingwa vikali na kundi lenyewe. Inaarifiwa kuwa uongozi wake unapingwa, na wanachama wanaotoka maeneo ya Kusini na ambao ni wengi katika kundi hilo. Inakisiwa idadi yao ni kati ya wanajeshi 7,000 na 9,000.

Bwana Godane huwa haonekani hadharani . Mtangulizi wake Moalim Aden Hashi Ayro, aliuawa katika shambulizi lililofanywa na Marekani mwaka 2008.

Uhusiano wa Kimataifa

Al-Shabab lilijiunga na al-Qaeda mwezi Februari mwaka 2012. Katika ujumbe wa Video, kiongozi wa al-Shabab Ahmed Abdi Godane alisema anaahidi kuunga mkono kingozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri.

Makundi hayo mawili yamekuwa yakifanya kazi kwa pamoja, na raia wa kigeni wamekuwa wakiunga mkono kundi hilo, na hata kuwasaidia katika harakati zao za mapigano.

Mwaka jana maafisa wa al-Shabab waliambatana na mtu aliyesema ni mwanachama wa al-Qaeda na kumtambua kuwa raia wa Marekani Abu Abdulla Almuhajir alipokuwa anatoa msaada wa chakula kwa waathiriwa wa njaa.

Maafisa nchini Marekani wanaamini kuwa wapiganaji wa Al Qaeeda ambao hawajahusina sana na mashambulizi nchini Afghanistan na Pakistan kufuatia mauaji ya kiongozi wao,Osama bin Laden, wapiganaji wake wengi wanakwenda kutafuta hifadhi nchini Somalia