Home Makala SAINI MILIONI 4.7 ZAKUSANYWA KUTAKA MATOKEO YA KURA ZA URAIS YABADILISHWE

SAINI MILIONI 4.7 ZAKUSANYWA KUTAKA MATOKEO YA KURA ZA URAIS YABADILISHWE

458
0
SHARE

Kuna wananchi wengi wa Marekani ambao hawamtaki Donald Trump kuwa rais wao. Na pengine ndiyo sababu alishindwa kwa Hillary Clinton kwenye kura za ujumla – kwa zaidi ya kura 2.5 milioni.

Zaidi ya watu 4.7 milioni wametia saini ombi la kutaka wawakilishi wa Kura za Majimboni (Electoral College) kumzuia Trump asiwe Rais wa Marekani.

Na inasemekana hilo ndiyo hasa linaweza kutokea – yaani inawezekana kabisa kwa wajumbe hao wa Electoral College kuketi tena na kumpigia kura mgombea ambaye wanaamini ndiyo halali kuwa rais wa Marekani.

Gazeti la The Independent la Marekani liliandika wiki iliyopita kwamba “Hillary Clinton alipata kura nyingi zaidi kuliko Donald Trump, lakini Trump anakuwa rais mteule kutokana na mfumo wa uchaguzi.”

Ombi hilo linasema: “Ifikapo Desemba 19, wajumbe wa Electoral College wataketi na kupiga kura, na kama wote watapiga kura kwa namna Majimbo yao yalivyopiga kura, Donald Trump atashinda.

“Lakini katika majimbo 14 miongoni mwa yale aliyoshinda Trump, wajumbe hao wanaweza kumpigia kura Hillary Clinton bila hata ya kuvunja sheria yoyote iwapo watafanya hivyo.”

Ombi hilo laendelea kusisitiza kwamba Hillary Clinton alishinda kura za jumla (popular vote) na hivyo anapaswa kuwa Rais.

Nao wadadisi wa masuala ya siasa wanasema: “Lakini wajumbe wa Electoral College watakapoketi wanaweza kutoa ushindi kwa yoyote baina ya wagombea wawili hao.

Wanahoji: “Hivyo kwanini tusitumia njia hii ambayo siyo kabisa ya kidemokrasia iliyomo katyika taasisi zetu kuhakikisha kupata matokeo ya kidemokrasia?”