Home Makala ELIMU SIASA INADUMAZA FIKRA ZA VIJANA

ELIMU SIASA INADUMAZA FIKRA ZA VIJANA

253
0
SHARE

NA THADEI OLE MUSHI


KWA kiasi kikubwa sekta ya Elimu hapa nchinbi imetawaliwa na siasa. Unaweza kuiita Elimu siasa, waamuzi wakubwa kwenye masuala nyeti yanayoihusu elimu yanafanywa na wanasiasa, huku wataalamu husika wakiwa watazamaji tu.

Hali hiyo ndio imekuwa msingi mkuu wa kuwadumaza vijana, hasa katika kupambana kwenye soko la ajira. Wengi wao wanafikiria kuajiriwa tu.

Nchini  Kenya hali ni tofauti, asilimia 80 ya wahitimu wa vyuo ufahamu wao upo kwenye kujiajiri huku asilimia 20 tu ndio inayotegemea kuajiriwa na Serikali ama sekta binafsi.

Kwa Tanzania asilimia 90 ya wahitimu wanasubiri kuajiriwa huku asilimia 10 wakijaribu ujasiriamali (Kujiajiri).

Sijui kama wizara inayohusika na ajira kama ina taarifa  halisi za ukubwa wa tatizo la ajira nchini, hata hivyo kwa macho ya kawaida tu tatizo hili linaonekana kuwapo na litaendelea kuwapo.

Kadiri tunavyoendelea huko mbele tatizo hili litazidi kuwa kubwa kutokana na vyuo vingi kudahili wanafunzi wengi zaidi ambao wote wanakwenda kupatiwa elimu siasa, ambayo imejaa nadharia kuliko uhalisia wa maisha halisi mtaani.

Ushahidi wa tatizo hili niliwahi kuutoa hapa nikaonyesha idadi ya vijana waliojitokeza uwanja wa Taifa ambao walikuwa ni zaidi ya 15, 000 wote walikuwa wakigombania  nafasi 70.

TRA nao walishawahi kuendesha usaili wa nafasi zisizofika 100, wakajitokeza zaidi ya vijana 10,000. Hata nikiangalia mazingira yanayonizunguka naona tatizo hili kuwa kubwa.

Wanaotafuta ajira badala ya kujiajiri hawana kosa, kosa ni la mfumo wa elimu yetu kuania ngazi ya Msingi mpaka elimu ya Juu.

Tatizo kubwa lipo kwenye aina ya Elimu tunayoipata.Elimu yetu haiendani na uhalisia wa kilichopo njee ya mfumo wa elimu. Tunachokifundisha na kufundishwa si kilichopo huko mtaani.

Hebu fikiria kwa Taifa ambalo linajinasibu kuwa kilimo ndio uti wa mgongo ila tunashindwa kuingiza somo la kilimo kuanzia ngazi za chini kabisa (Primary).

Jamii pia kuona mtu aliyeelimika tu ni yule mwenye kufika chuo kikuu, elimu yetu baada ya uhuru ilipaswa ilenge falsafa kweli ya kujitegemea yaani mtu akimaliza masomo yake katika ngazi yoyote aweze kujitegemea bila kusubiri ajira serikalini.

Kwa nini tusianze kufundisha elimu ya ufundi kuanzia kwenye ngazi za chini? Kila kata iwe na shule moja ya ufundi itakayofundisha ufundi tofauti tofauti. Inawezekana hata kwenye shule zetu za kata kuingiza masomo ya ufundi tena liwe la lazima….

Kwa nini tusipanue vyuo vyetu vya ufundi viweze kudahili wanafunzi wengi zaidi? Kwa nini bodi ya mikopo isiwatambue wanaosoma ufundi? Tuwekeze katika eneo hili kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili na kujiandaa kuingia kwenye uchumi wa viwanda.

Content zinazofundishwa madarasani kwa sasa zimeshindwa kutukimbiza kimaendeleo. Lazma tuangalie namna ya kuzibadilisha ikiwezekana.

Pia tuachane na course za ajabu ajabu tunazozisoma chuo kikuu, tusome kwa kuangalia soko la ajira linazungumza nini. Mtu unasoma political science na ulifaulu vizuri masomo ya science kwa nini usiangalie course ambayo unajua nikitoka nitaweza kujibangaiza au kuajirika?? Matokeo yake ni kila kijana kutaka kuwa mwanasiasa.

Serikali itusaidie kubadili mindset za vijana kwa kuwaandaa toka mashuleni…. kuna mabenki kibao yanatoa mikopo kwa vijana waliopo kwenye vikundi ila hawajitokezi kwa kuwa wameandaliwa kuajiriwa… narudia si kosa lao kusubiri ajira kwa kuwa ndivyo elimu yetu inavyotuandaa.

Tumeshindwa kabisa kuachana na minyororo ya kikoloni,mpaka leo tunalumbana tutumie lugha gani kufundishia.Wala usijali umesomea kayumba au shule za mchepuo wa Kiingereza tatizo letu mwisho wa siku ni moja.umefungwa na wakoloni mpaka leo. Ningeshauri kuwepo mabadiliko ya haraka kwenye sekta ya elimu katika mambo kadhaa yafuatayo:-

 

  1. Recruitment: – Hiki ni kitendo cha kuwavutia watu kujiunga na taaluma flani au taasisi flani na kufanya nayo kazi. Mfano katika taasisi nyingine kama vile bank, uhasibu, sheria nk hufuata utaratibu huu katika kuwapata wafanyakazi wake. Tumekuwa tukiona matangazo mengi ya kazi kutoka wizara mbalimbali wakiwataka watu kuomba nafasi hizo ila kwa upande wa elimu hakuna utaratibu wa waalimu kutakiwa kuomba nafasi za kazi, badala yake hupangwa moja kwa moja kwenye vituo vya kazi mara tu wamalizapo vyuo.

Udhaifu huu unasababisha kuwalazimisha watu kufanya kazi wasiyoitaka na matokeo yake hufundisha ilimradi tu mwisho wa mwezi ufike wapate mshahara. Wanasaikolojia wanasema mtu anapoifanya kazi anayoipenda hufanya vizuri na kwa ufanisi zaidi hata kama mshahara ni mdogo.
Serikali iangalie upya upatikanaji wa waalimu katika shule zake, Wasiwapangie wahitimu moja kwa moja mara tu wanapomaliza chuo wawaache waende mtaani halafu waombe wenyewe kama kada nyingine wanavyofanya, Pia waendeshe usaili kupata walio bora si kila mtu anachukuliwa kuwa waalimu. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa waalimu kwenye maeneo ambayo watu hawapendi kufanya kazi. Mfano mikoa ya kusini na kanda ya kati. Serikali inapotangaza ajira hizi waseme kabisa kuwa waalimu wanaotafutwa ni wa kufanya kazi mikoa A, B, C kama upo tayari omba hili litapunguza hata vimemo pale wizarani. Kama mtu anataka kufanya kazi Dar asubiri hadi uhaba utakapojitokeza Dar aendelew kukaa mtaani.

2.Selection:- Hatua hii nayo ni muhimu kwani hapa humpima mtu kama kweli anafaa kwenye nafasi husika. Kada nyingine hili nalo linafuatwa kwani watu huitwa kwenye usaili na kuangaliwa kama walichokiomba wanakiweza na si kurelay kwenye vyeti vyao tu. Katika kada ya ualimu hili nalo halipo watu wanaajiriwa tu bila kuangaliwa kama credentials zao zinafiti kwenye taaluma husika. Tumekuwa tukisikia mara nyingi tu waalimu kuwabaka wanafunzi, kuwa walevi wa kupindukia nk. Kwa nchi nyingine hili linafuatwa na wanafanikiwa sana hata hapa kwetu angalia shule za binafsi wanafanya hili na linganisha matokeo yao na shule za Umma. Utasikia waalimu wakikuambia kuwa watoto wamefeli kwa kuwa hawana maabara lakini si kweli kwani hayo masomo mengine kama history kisw nk yanahitaji maabara?

 

  1. Content:- Niwakati pia wa kufanya review ya mitaala yetu kuanzia shule za msingi hadi sekondari. Kuna baadhi ya mambo ambayo wanafunzi hufundishwa ila kiuhalisia hayana uhisiano wowote na maisha yao ya baadaye. Elimu yetu ijikite kwenye kulikomboa taifa kiuchumi na kimaadili. Kuna content nyingine ni za kikoloni. Kwa nini tusijikite kuwafundisha kilimo bora kuanzia huku chini?? Kwa nini tusiwekeze kuwafundisha namna ya kutumia maji yanayotuzunguka kila mahali?? Eneo hili ndilo linalotuchelewesha lazma tukubali kubadilika tufundishe wanafunzi wetu kulingana na mazingira yao na fursa zilizopo. Tukiweza kujinasua hapa tutasonga mbele kwa kasi kimaendeleo.
  2. Lugha ya Kufundishia:- Kwa Tanzania sasa kuna matabaka makubwa mawili. Moja ni la wanafunzi waliopitia shule za mchepuo wa kiingereza yaani kuanzia pre-primary hadi darasa la saba wanasoma kwa lugha ya Kiingereza na kundi lingine ni lile linalopitia shule zetu za kawaida kama mtakuja primary School. Hawa kwa pamoja wanakuja kukutana secondary wanatumia lugha moja. Utafiti unaonyesha kuwa wanaopitia hizi za mchepuo wa Kiingereza wanafanya vizuri zaidi sekondary kuliko hawa wengine. Serikali ifike mahali ikubali ama wakubali tutumie kiingereza kuanzia huku chini mpaka juu au tutmie kiswahili kuanzia huku chini hadi juu.

Tuondoe mkanganyiko huu unaojitokeza hata hivyo shule hizi zenye kutumia mchepuo wa Kiingereza wamekuwa wakifaulu zaidi elimu ya msingi hivyo hawa ndio wanaojaza nafasi kwenye shule nzuri za serikali za boarding kama Mzumbe, Ilboru na nyinginezo. Hakuna “fairground” huku ni swala la maamuzi tu.Nilibahatika kuangalia wanafunzi kwa mfano waliopangiwa shule ya Mzumbe toka mkoa wa Kilimanjro, hakuna mwanafunzi hata mmoja anayetokea kundi la shule za kawaida za serikali, wote wanatokea shule za binafsi vivyo hivyo kwa waliopangwa Ilboru kwa hiyo asilimia zaidi ya 95 ya waliopangwa kwenye shule hizo wametokea kwenye shule hizi za mchepuo wa kiingereza.

  1. Utaratibu wa kurudia STD Seven:- Ulishawahi kuchunguza?? Serikali haitambui mwanafunzi aliyefeli darasa la Saba. Hali ni tofauti na ngazi nyingine za Elimu kidato cha nne mtoto mwanafunzi akifeli anaruhusiwa kurudia mtihani huo kama mtahiniwa binafsi (private candidate) kidato cha sita hali kadhalika chuo kikuu kuna suplimentary kwa anayefeli course flan lakini hapa chini pamesahaulika.

Kama mtoto akifeli std Seven na mzazi hana uwezo wa kumlipia private basi ndoto ya mtoto huyu inazimwa kabisa. Wakati serikali ikiwa inasubiri mpango wa elimu ya msingi hadi form four miaka sita ijayo wafungue hapa wanaofeli waruhusiwe kujaribu tena.

Nina imani huyu mtoto anaweza kuwa anafeli kutoakana na uwezo wake mdogo wa ku accomodate matatizo katika mazingira wanayoishi kuliko hawa wakubwa wanaopewa nafasi nyingine ya kujaribu.

  1. Masomo ya Ufundi:- Serikali ikubali sasa kuwa elimu ya ufundi si jambo la hiyari tena bali ni kwamba halikwepeki. Tanzania tuna kila kitu kasoro teknolojia, kinachotuangusha kila mahali ni uhaba wa teknolojia. Ni aibu hata magorofa yanayojengwa kwenye miji yetu yanajengwa na makampuni ya nje, si kwenye kilimo na si kwenye madini teknolojia ndio imetushikisha adabu kweli kweli. Niliwahi kusema hapo kabla kuwa serikali inapswa kufuta masomo ya sayansi kuwa masomo ya “option” pindi mwanafunzi afikapo kidato cha tatu. Tushukuru kuwa kwa sasa serikali imeamua kuyafanya kuwa ni masomo ya lazima hadi kidato cha nne. Japokuwa tulichelewa kuyafanya hivyo ila itasaidia sana.

Kwa sasa tunapswa kugeukia kwenye masomo ya Ufundi, Serikali ipitishe utaratibu kuwa kila shule ya Sekondari ichague fani mbili za kufundisha (za ufundi na kilimo) ambazo mwanafunzi atazisoma kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Bahati mbaya sana kwa shule ambazo zina masomo hayo wanafunzi wamekuwa wakiyadharau. Niliwahi kufika shule moja ya sekondari ambayo hufundisha fani mbalimbali kama vile upishi, uchoraji, muziki, ushonaji nk.

Ajabu ni kwamba wanafunzi wamekuwa wakiyadharau masomo haya na nilijaribu kuingia kwenye darasa moja la Ushonaji mwalimu wa Somo lile akaniambia kuwa huwa hapati wanafunzi wengi kwa kuwa wanafunzi wengi hukimbilia kwenye somo la kompyuta ambako huko hawaendi kujifunza bali huenda kuchat kwenye social media.

Hapa napo Serikali inapswa kupaangalia upya watoe mkazo kwenye hizi shule za sekondari  ambazo tayari zina fani hizi. Ni aibu kusikia majeshi yetu yanaagiza uniform toka njee ya nchi wakati zingeweza kutengenezewa hapa nchini.

ITAENDELEA………….