Home Afrika Mashariki NIKISHINDWA SITANG’ANG’ANIA MADARAKA-KENYATTA

NIKISHINDWA SITANG’ANG’ANIA MADARAKA-KENYATTA

382
0
SHARE
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

NYERI, KENYA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameelezea nia yake ya kuachia madaraka kwa amani kama ikitokea akashindwa katika uchaguzi mkuu ujao. Kauli hii ambayo ni muendelezo kutoka kwa Uhuru ameitoa kwa waandishi wa habari wiki hii, akifafanua hisia zake juu ya hali ilivyokuwa ikiikabili nchi ya Gambia ambayo nusura iingie katika machafuko kutokana na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kutaka kung’ang’ania kubakia madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika mwezi Desemba mwaka jana.

Jammeh baada ya kukubali yaishe amekimbilia uhamishoni nchini Equatoria Guniea na hali hiyo imetokana pia na nguvu ya Mataifa ya Afrika Magharibi ambayo aliyatangaza kutomtambua na kasha yakasimamia kuapishwa kwa mshindi halali wa uchaguzi huo sasa Rais Adama Barrow. Sherehe za kuapishwa kwa Barrow zilifanyika katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal katika jiji la Dakar.

Kenya inatarajia kufanya uhaguzi mkuu wake mwezi Agosti tarehe 8, mwaka huu na tayari joto la uchaguzi huo limeshakuwa kubwa kufuatia mabi zinazopingana kuanza kujiandaa na uchaguzi huku kukiwa na mikutano ya mara kwa mara yenye kuleta mashinikizo kwa tume ya uchaguzi sambamba na kambi hizo hasimu kuanza kuunganisha nguvu.

Rais Uhuru aliweka bayana kwa waandishi wa habari waliokutana naye katika Hiteli ya Sagana iliyopo Nyeri akasema, hawezi kamwe kung’ang;ania kubakia madarakani kama atashindwa katika uchaguzi huo na kwamba atakubaliana na maamuzi ya wananchi.

“Nitaheshimu maamuzi ya Wakenya baada ya uchaguzi huo Agosti 08. Utawala wa sheria na maamuzi ya Wakenya lazima ndivyo vibakie juu kuliko  kitu kingine chochote,” alisema.

Uhuru anaingia katika uchaguzi huo akiwania kipindi cha pili kupitia chama cha Jubelee ilhali wapinzani wake hadi sasa hawajaweka bayana jina la mgombea wao atakayrekabiliana na Uhuru katika uchaguzi huo.

Rais Uhuru anaonesha kujiamini na kwamba ana uhakika kuwa atashinda uchaguzi huo kutokana na rekodi zake za maendeleo aliyoyafanya tangu achaguliwe kuwa rais wa Kenya mwaka 2013.

Kwa upande wa upinzani wanaweza kuwa nao na wakati mgumu hasa katika suala la kukubaliana kuhusu mgombea wao. Lakini katika hali nyingine kambi hiyo inazidi kuimarika hasa baada ya kuundwa umoja mpya maarufu kama NASA. Umoja huu mpya kama utafanikiwa kuingia katika uchaguzi bila kushindwana mbeleni, unatoa mwanya kwa wapinzani kuwa katika mazingira mazuri ya kuchukua nchi. Pia hali ya uwepo wa tumeya uchaguzi ambayo inahusisha makundi mbalimbali na ambayo imepitia mchujo wa kuidhinishwa na bunge unaweza kuwa ni sababu ya kuwepo kwa uchaguzi huru na haki.

Lakini pia hali ya Kenya kwa sasa na namna jamii ilivyogawanyika, uchaguzi wa mwaka huu unaweza kuwa ni mtihani mkubwa kwa taifa hilo lenye uchumi mkubwa katika nchi za Afrika Mashariki.