Home Makala Kimataifa AFRIKA KUSINI INAHITAJI MAGEUZI MAKUBWA KIUTAWALA

AFRIKA KUSINI INAHITAJI MAGEUZI MAKUBWA KIUTAWALA

508
0
SHARE

 

JOHANNESBURG

Taifa la Afrika ya Kusini linapita katika misukosuko mikubwa kama ilivyonekana wiki iliyopita wakati rais Jacob Zuma alipokwenda Bungeni kulihutubia kwa kutoa hotuba ya kila mwaka ya ‘State of the Union’ inayoeleza hali ya nchi ilivyo.

Kwa kiwango fulani, ukiangalia misuguano na mapungufu ya kiuongozi katika Bunge – mahali ambapo kwa kawaida taifa hujitizama kwa lengo la kujitafakari ili kupata vizheni – ilikuwa kama vile unamuangalia mgonjwa mahututi ndani ya ICU, hali ambayo unayoiona kwa wagonjwa na wengine wote waliomo. Na hapo unajiuliza: je yupo daktari au muuguzi ambaye anaweza kuokoa hali yake?

Aidha mtu hakosi kushangaa iwapo sauti ya mkuu wa nchi ndani ya Bunge hilo lilokuwa na vurugu kubwa nje na ndani ya ukumbi pia inatoa ishara yoyote ya kile kinachokwenda ndivyo sivyo ndani ya nchi, na iwapo kuna ajenda ya kubadili mwenendo wa taifa.

Wakati wa hotuba hiyo, na tukiachilia mbali zile vurugu na ishara nyingine za ovyo, Rais Zuma alitilia mkazo wa kuwepo kwa kwa haraka mageuzi makubwa ya mifumo ya kiutawala, katika asasi na umiliki wa uchumi kwa kutoa upendeleo kwa watu wote wa Afrika ya Kusini, hususan wale masikini, ambao wengi wao ni watu weusi, na zaidi ni wa jinsia ya kike.

Alitoa mpango wenye vigezo tisa, mpango ambao pia amewahi kuutoa katika hotuba yake Bungeni mwaka 2016 na 2016. Hotuba hiyo ilitilia mkazo ukuaji wa uchumi, na pamoja na mengine, maendeleo ya viwanda, kilimo cha kibiashara na uchimbaji madini na hasa kuona ni nani hasa mnufaika wa sekta hizi.

Alisema sekta hizi zinahitaji mapinduzi makubwa na akatangaza kwamba huo utakuwa ukurasa mpya katika kipindi chake cha urais kilichobakia.

Mengi haya si mapya kutoka kinywani kwa Zuma labda lile suala la wanaodai ardhi – kwamba badala yake wapewe fedha kama fidia.

Daima kumekuwepo utata kuhusu suala la ukuaji uchumi  ma hotuba ya Zuma iliongeza tu utata huo. Mwezi mmoja tu uliopita (Januari 8) taarifa ya chama tawala cha ANC kilionyesha kuwepo kwa ongezeko la uchumi (GDP) la asilimia 2.7 kwa mwaka 2017. Zuma aliirejea asilimia hii kwa kwenda chini hadi asilimia 1.3. Shirika la Fedha Duniani (IMF) linatabiri ongezeko la ukuaji wa uchumi la 0.8 tu.

Inawezekana Zuma yu sahihi kwa kuonyesha kwa wananchi haja ya kuwepo kwa mageuzi makubwa katika uchumi ingawa hili hakuliweka bayana. Inavyoonekana, changamoto kubwa kwa watu wa Afrika ya Kusini ni kukosekana kwa haja ya mageuzi makubwa ya nchi.

Nchi yenye misukosuko na migongano mikubwa haiwezi kuleta mageuzi ya kiuchumi mithili ya mgonjwa mmoja kuweza kuwatibu wagonjwa wengine.

Na katika viwango vingine, nchi imepoteza uhalali, na kushindwa kuiweka nchi pamoja bado kunaleta hali ya wasiwasi. Kwa upande mmoja, nchi yenye misukosuko inahitaji msimamizi mwenye busara na ufanisi mkubwa na vizheni isiyotetereka. Kuna ishara tosha sasa hivi kwamba taifa la Afrika ya Kusini lina upungufu wa vyote hivyo.

Lakini swali kubwa ni je, nchi inayozaliwa upya ikoje? Nchi ya namna hii lazima itimize angalau masharti matatu.

Kwanza lazima iwe inaonekana inaendeshwa kwa njia ya kuwajibika. Utumishi wa umma ni utumisho wa wito hivyo hao wanaojiunga katika utumishi wa umma wajione wanaweza kutumikia hata kwa kupitiliza viwango vya uwajibikaji wao.

Pili, mtu mmoja mmoja lazima akubali kuongozwa na maadili kama ndiyo sheria na wajisikie wametenda makosa iwapo watakuwa wametenda makosa. Kama vile Nelson Mandela alivyokuwa akisema – siku zote wakati ni sahihi kwa kutenda kilicho sahihi. Hata hivyo kunatakiwa kuwepo kwa maadili ya kipamoja katika utumishi wa umma.

Na tatu, utawala wa sheria lazima ubakie kama muongozo mkuu wa nchi. Vigogo na watu wa chini lazima wawe sawa mbele ya sheria.

Kwa upande mwingine vita vya kuurithi uongozi wa ANC inazidi kupamba moto, hivyo kuna fursa kwa utawala utakaokuja baada ya 2019 kuleta mageuzi makubwa katika nchi.

Swali la kujiuliza ni iwapo mshindi miongoni mwa ya chama hicho – ambacho bila shaka ndicho kitakachoshinda uchaguzi mkuu ujao – atatoka ndani ANC ile ya kabla ya kupata uhuru.

Jibu la swali hili halijulikani, lakini kinachoonekana wazi ni kwamba iwapo taifa halitabadilika, kuna hatari ya kuteleza chini na pengine hata kufikia kiwango cha ilivyokuwa wakati wa utawala wa kibaguzi. Si kwamba hilo litatokea sasa hivi, lakini ishara zinaonekana.