Home Makala JANETH: MWILI UNAHITAJI VIRUTUBISHO KUONDOA SUMU

JANETH: MWILI UNAHITAJI VIRUTUBISHO KUONDOA SUMU

167
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU


Asilimia 80 hadi 90 ya magonjwa katika mwili wa binadamu husababishwa na sumu mwilini (Free Radicals).

‘Free radicals’ ni kemikali ambazo husababisha magonjwa sugu kama vile saratani na magonjwa ya moyo.

Mtaalamu wa Afya ya Jamii na Mkufunzi wa maisha kutoka Kampuni ya Trevo, Dk. Janeth Massawe, anaelezea namna ‘Free Radicals’ husababisha magonjwa mbalimbali mwilini na njia bora za kuziondoa.

Dk. Janeth anasema sumu katika mwili wa binadamu hupatikana wakati mwili unapotengeneza nishati yake kwa kutumia Oxygen.

Anafafanua kuwa sumu au ‘Free radicals’ ni muhimu katika miili kwa sababu zinapambana na magonjwa ambukizi mbalimbali yanayotokana na bakteria, fangaz na vidudu (parasites).

Pia kwa upande mwingine sumu ya mwilini ni hatari sana endapo ikizalishwa kwa wingi kulingana na uhitaji wa mwili.

Anafafanua kuwa sumu ikizalishwa mwilini inadhibitiwa na virutubisho vinavyotokana na vyakula tunavyokula ambavyo vinaitwa ‘antioxidants nutrients’.

“Sasa kama uzalishaji wa ‘free radicals’ ni mkubwa kuliko kiwango sahihi kinachohitajika kwenye mwili, mwili ndio unaanza kupata maradhi mbalimbali,” anasema Dk. Janeth.

“Kwa mfano kama ni kwenye mishipa ya damu, mtu atapata matatizo ya moyo au kwenye tumbo atapata vidonda vya tumbo,” anafafanua.

Anasema kama ni kwenye ngozi mtu anapata saratani ya ngozi au kunyauka kwa ngozi na maradhi mengine mengi ambayo hutegemea na sehemu ya mwili ambayo sumu zimezidi kiwango.

Kwa hali ya uhalisia kuna vitu vilivyotajwa hapo juu ambavyo ni rahisi kuepuka lakini kuna vingine ni vigumu kuepukika kama vyakula, kupigwa na mionzi ya jua kutokana na changamoto mbalimbali za maisha.

Kwanini kuna ulazima wa kila mtu kunywa trevo?

Watu wengi siku hizi wanahangaika kutafuta tiba na matibabu ya kupambana au kuondoa ‘free radicals’ hizi mwilini ambapo watu wengi hutumia madawa mbalimbali katika kupunguza tatizo hili.

Kwa upande wa Dk. Janeth, anasema tiba nzuri kuliko zote ni virutubisho vya vyakula mbalimbali ambavyo ni salama zaidi.

Anafafanua kuwa kuna virutubisho vinavyopatikana katika kinywaji cha Trevo ambacho kimetengezwa kwa mimea, matunda, mbogamboga na mizizi ya asili.

“Trevo ni kirutubisho cha mwili cha kipekee ambacho hakijapata mshindani wa kulingana nacho hadi sasa,” anasema.

Ni mchanganyiko uliobuniwa na kufanikiwa kwa kiwango cha juu kurudisha, kukarabati na kuamsha afya ya mtu iliyodorora.

“Mchanganyiko huu hufanya kazi kwa kuupa mwili virutubisho vyote ambavyo umekosa kutokana na kula chakula cha kisasa kinachokosa virutubisho muhimu,” anaongeza.

Ni mchanganyiko unaofanya kazi vizuri kwa mtu wa umri wowote kuanzia mtoto wa miaka miwili hadi mtu mzima kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo anasema Trevo ina uwezo wa kupambana na ‘free radicals’ zisizopungua 400,000.

“Binadamu wa kawaida anapaswa apate angalau virutubisho 90 vyenye uwezo wa kupambana na ‘free radicals’ visivyopungua 7,000 (orac rate),” anasema.

Hivyo, mtu anayetumia virutubisho vya Trevo anakuwa kwenye nafasi nzuri kiafya kwani anapitiliza kwa kupata 13,000 orac rate kwa siku.

Anaelezea kuwa hata mtu ambaye anakula milo yote vizuri, ukweli ni kwamba hakuna mwanadamu anayeweza kufikisha mahitaji  hayo ya mwili kwa sababu mwili hauna uwezo wa kufyonza virutubisho vyote vinavyotokana na vyakula tunavyokula.

“Faida kubwa ya kirutubisho cha Trevo ni kuwa na chembechembe ndogondogo, hivyo mtu akitumia inaenda moja kwa moja kwenye mfumo wa damu, hakuna kinachopotea,” anaongezea mtaalamu huyo.