Home Makala HISTORIA YA BOMU LA ATOMIKI NAGASAKI, HIROSHIMA

HISTORIA YA BOMU LA ATOMIKI NAGASAKI, HIROSHIMA

924
0
SHARE

NA JOSEPHAT NYAMBEYA


BOMU la nyuklia ni silaha inayosababisa mlipuko mkubwa sana na ni silaha hatari na yenye nguvu kuliko silaha yoyote iliyowahi kupatwa kutengenezwa katika historia ya silaha duniani.

Mabomu haya ya atomia hutengenezwa kwa kutumia madini yaitwayo uraniamu au plutoni.

Pindi lipigwapo bomu hilo husababisha kuondoa kila kinachokutwa katika uso wa dunia na kugeuza eneo hilo  kuwa jangwa.

 

Teknolojia ya kufyatua mabomu ya nyuklia

Kuna namna mbili za kufikisha mabomu haya panapolengwa; njia ya kwanza ni kutumia ndege za kivita na njia ya pili ni kutumia roketi.

Pia kuna mabomu madogo yanayoingizwa katika makombora ya mizinga.

Nchi ya Japani, haitaweza kusahau tukio la kupigwa bomu la nyuklia katika miji yake ya Hiroshima na Nagasaki ikiwa vita ya pili ya dunia ikielekea kufika ukomo.

Japani ilijikuta ikipata kipigo hicho kitakatifu kutoka kwa Marekani ambayo iliamriwa kufanya hivyo na Rais wake Harry S. Truman, kupiga mabomu hayo mfululizo kutokea Agosti 6 hadi  9 mwaka 1945.

Bomu hilo ambalo lilipewa jina la ‘Little Boy’ liliporomoshwa jiji la Hiroshima siku ya Jumatatu, Agosti 6, 1945, hadi Agosti 9 likamaliziwa na Nagasaki na kuandika historia ambayo haitasahaulika duniani.

Mlipuko huo ndiyo uliosababisha kupinga utengenezaji wa mabomu ya aina hiyo kwani ulifanya maangamizi makubwa kwa kuua jumla ya watu 140,000 huko Hiroshima na 80,000 wa Nagasaki mwishoni mwa mwaka 1945.

Siku chache baada ya kumalizika kwa tukio hilo inakisiwa kuna asilimia kati ya 15 na 20 ya watu waliopoteza maisha kutokana na majeruha waliyoyapata kutokana bomu hilo.

Wapo waliofariki kutokana na hewa ambayo ilikuwa ya sumu kutoka katika bomu hilo, wengine walikufa kutokana na mionzi yake na wengine kansa.

Kutokana na uwezo wa mabomu hayo siku sita ya kupigwa kwake huko Nagasaki, Agosti 15, Japani ilitangaza kusalimu amri na Septemba 2 ikasaini kuachana na vita hivyo.

Mradi huu uliopewa jina la ‘The Manhattan Project’ ulikuwa wa kwanza kutengenezwa ukiwa chini ya ushirikiano kati ya wataalamu kutoka Marekani, Uingereza na Canada.

Kihistoria mji wa Hiroshima ambao uliathiriwa na bomu la nyuklia ni mji Mkuu wa Mkoa wa Hiroshima.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2009, mji una wakazi wapatao milioni 1.2 wanaoishi katika mji huu. Mji huu uko kwenye kisiwa kinachojulikana kama Honshu.

Mji umekuwa maarufu duniani kwa sababu ilikuwa mji wa kwanza katika historia iliyoshambuliwa kwa bomu ya nyuklia.

Mji huu ulijengwa upya baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Katika mji huu kuna gofu ambalo linajulikana kama ‘Kuba ya bomu ya nyuklia’ ni gofu la nyumba linalohifadhiwa kama kumbukumbu ya mlipuko, na jengo hilo limeingizwa katika  orodha ya urithi wa dunia.

Kabla ya kushambuliwa mji huu ulikuwa na msongamano wa watu waliokuwa wakifikia 381,000 lakini baada ya vita kuisha idadi hiyo ilipungua na kufikia kiasi cha watu 255,000.

Mji mwingine ulikumbwa na shambulio la mabomu hayo ulikuwa Nagasaki ambao nao unapatikana katika kisiwa cha Kyushu.

Mji huu nao umejizolea umaarufu kutokana na shambulio hilo la mwaka 1945 na kwa sasa unatumiwa kama mji wa pili wa kihistoria baada ya Hiroshima.

Mji huu ulipopigwa na bomu ulisababisha mauaji ya watu 36,000 hapo hapo na wengine waliokadiriwa kuwa kati ya 70,000 na 100,000 kufariki baadaye kutokana na maradhi yaliyotokana na nyuklia.

Kabla ya angamizi hilo Nagasaki ilikuwa kitovu cha Ukristo katika Japani mnamo mwaka 1600 na imani hii ya Kikristo ilipigwa marufuku na serikali ya Japan.

Agizo hilo la kupigwa marufuku kwa Ukristo ilisababisha wakristo wengi kuuawa katika miaka iliyofuata na wapo walitunza imani hiyo kwa siri hadi kurudishwa kwa uhuru wa kuabudu katika karne ya 19.

Kanisa lililokuwa maarufu la Kikatoliki huko Nagasaki linalojulikana kama, Urakami Tenshudo liliharibiwa na bomu la nyuklia Januari 1946.

Pia katika mauji hayo inadaiwa asilimia 90 ya madaktari waliuawa ikiwa ni pamoja na asilimia 93 ya wauguzi wa Hiroshima.  Makala kwa hisani ya Techbrain