Home Makala Kimataifa DUNIANI KUNA MAMBO: ABIRIA ASHITAKI ETIHAD KWA KUWEKWA KITI KIMOJA NA ABIRIA...

DUNIANI KUNA MAMBO: ABIRIA ASHITAKI ETIHAD KWA KUWEKWA KITI KIMOJA NA ABIRIA MNENE

605
0
SHARE

Raia mmoja wa Australia amefungua kesi katika mahakama moja mjini Brisbane Australia dhidi ya shirika la ndege la Abu Dhabi Etihad – akidai alipwe fidia kutokana na maumivu ya mgongo aliyopata baada ya kupangiwa kukaa kiti cha karibu na msafiri mnene ambaye alikuwa akikohoa sana.

Mtu huyo James Andres Bassos anadai fidia ya Dola za Kimarekani 227,000 kutoka shirika hilo – ambazo ni fedha za gharama ya matibabu na kukoseshwa mapato katika hali ya kitoweza kufanya kazi hadi sasa.

Katika hati ya madai iliyowasilishwa na mawakili wake Bassos anadai kwamba abiria huyo aliyekaa naye alikuwa mnene wa kupindukia kiasi kwamba alikuwa anambana sana bila yeye kujigeuza kwa muda wa safari yote ya masaa 14 kati ya Sydney, Australia hadi Dubai.

Alidai kwamba abiria huyo kutokana na ukubwa wa mwili wake alikuwa anamuingilia katika kiti chake na anapokohoa maji maji meupe yalikuwa yanamtoka mdomoni.

Baada ya masaa matano wakiwa angani Bassos aliwaomba wahudumu wa ndege wampatie kiti kingine lakini walikataa wakisema kulikuwa hakuna kiti cha ziada kwani ndege ilikuwa imejaa.

Nusu saa baadaye Bassos alilalamika tena na wahudumu wakamhamishia kwenye moja ya viti katika sehemu ya wahudumu hao.

Hata hivyo mahakama ilielezwa kwamba Bassos alilazimika kukirejea kiti chake na kuketi kwa saa moja, lakini alirudishwa tena kukaa kwenye kiti cha mhudumu. Baadaye tena alirudishwa kwenye kiti chake kwa dakika 90 za mwisho za safari kutokama na kile kilichoitwa na wahudumu kuwa sababu za kiusalama.

Bassos anadai fidia kutokana na kuumia binafsi – kwamba kwa vile alikuwa anabanwa na mnene huyo alilazimika kujigeuzageuza kwa vipindi virefu vya safari ili asigusane naye na hivyo kumpatia maumivu ya mgongo ambayo yaliendelea kumsumbua.

Shirika la ndege la Etihad liljaribu kuishawishi mahakama kuitupilia mbali shauri hilo likisema ni kitu cha kawaida kuwa na biria waliozidi kwa unene ambao huchukua nafasi kubwa ya kiti, au abiria wanaokohoa.

Hata hivyo Jaji Fleur Kingham aliyekuwa kusikiliza kesi hiyo alikataa kuitupilia mbali kwa kusema hajaridhika bado kwamba kwamba mleta mashitaka hakuwa na nafasi ya kushinda kesi hiyo.

Jaji huyo amemtaka Bassos aende hospitalini kuchukuliwa vipimo vya afya yake na ripoti ya uchunguzi iwasilishwe mahakamani.

Hata hivyo shirika hilo la ndege limesema linadhamiria kupambana na shauri hilo hadi mwisho, hata ikibidi kukataa rufaa katika mahakama zajuu za Australia.