Home Makala KHADIJA SIMBA: WANAWAKE TUAMKE UJASIRIAMALI NDIO ‘DILI’

KHADIJA SIMBA: WANAWAKE TUAMKE UJASIRIAMALI NDIO ‘DILI’

238
0
SHARE
Khadija Simba

NA HARRIETH MANDARI,

INAPOTAJWA orodha ya majina ya wanawake wamiliki wa viwanda kwa miaka mingi hutakosa jina la Khadija Simba, mmiliki wa kiwanda cha Kays hygene Products Limited ambacho hutengeneza taulo za kike aina ya Jassy, Jassy Kipepeo, na bidhaa za pamba za Kaywool.

Siri kubwa kwa mjasiriamali anayetaka mafanikio kabla ya  kuanza biashara ni kufanya utafiti juu ya soko la bidhaa hiyo, aina ya wateja wake, gharama za biashara hiyo na pia iwapo kutafuta fursa za  kupata mkopo.

Katika mazungumza na RAI wiki hii Khadija anasema wazo la kuanzisha kiwanda hicho ambacho kilianza uzalishaji mwaka 1982, lilitokana na  nia ya dhati ya kujikomboa kiuchumi kama mwanamke pia kumtoa mwanamke katika matumizi ya vitambaa.

Kutokana na matumizi hayo ya njia za kizamamni husababisha magonjwa mbalimbali ya njia za uzazi hasa ikizingatiwa kuwa matumizi hayo huhitaji mtumiaji kuwa na maji ya kutosha, lakini maeneno mengi nchini kuna uhaba wa maji

Khadija ambaye ni mke wa Iddi Simba alizaliwa mwaka 1944 na akajaliwa kupata watoto watatu na wajukuu sita, anasema baada ya kumaliza masomo yake ya Ukutubi Muhktasi  nchini Nigeria mwaka 1964 katika chuo cha Federal Training Centre mjini Lagos na kurejeja nchini ambapo baadaye aliolewa na Iddi Simba. Alifanya kazi Serikalini kwa muda mfupi  na baadaye alikwenda nchini Marekani kumfuata mumewe aliyekuwa anafanya kazi huko.

Baada ya kutoka Nigeria:

Baada ya muda yeye na familia yake walihamia nchini Uganda ambapo mumewe alipata kazi ya kusimamia benki ya Afrika Mashariki.

“Wakati huo mimi nilikuwa nafanya kazi katika Shirika la Customs la Africa Mashariki nikiwa kama katibu  na pia Kamisha na nilijiendelelza kimasomo katika chuo kikuu cha Makerere nikisomea biashara na uchumi kwa muda wa mwaka mmoja.

“Maisha nchini Uganda yalivurugika pale Rais wa nchi hiyo alipopinduliwa na hayati Iddi Amin kupindua serikali hivyo ikawalazimu kurudi nchini Tanzania.

“Nikiwa mjini London Uingereza, wakati huo watoto walikuwa tayari wamekua na wako shuleni na hapo ndipo ndoto yangu ya kufungua ofisi ilijulikana kama Engaline Ltd. wakala wangu nchini Uingereza alikuwa kiunganishi kati ya bara la Ulaya na Afrika kibiashara na nilikuwa nikilipwa kamisheni,” anasema.

Baadaye mama huyo anasema walihamia nchini Kenya ambako mumewe alichaguliwa kuwa mwakilishi wa Benki ya Afrika hivyo kumlazimu kuhamishia kampuni yake mpya nchini humo.

Anasema wakati anarejea Tanzania mwaka 1982, lengo lake hasa lilikuwa ni kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vitasa na bawaba kutokana na kuwa  nyumba nyingi za Watanzania kwa wakati huo zilikuwa ni za kawaida hivyo kupata soko, lakini bado anaamini bidhaa hiyo ina soko zuri.

Fursa zilizopo katika awamu hii ya tano

Anasema wasichana na wakina mama wasibweteke      kwani zipo fursa nyingi sana ambazo zikichangamkiwa zitawakomboa wanawake kiuchumi.

“Fursa ni nyingi nchini kwa mfano ukiangalia hadi sasa hatuna kiwanda hata kimoja cha kutengeneza nguo za ndani zote huagizwa kutoka nje ya nchi na nyingine zikiwa zile zilizotumika (mitumba), wanawake changamkieni hizo fursa jamani,” anasema Hadija.

Anasema tatizo la vijana wengi hasa wa kike ni waoga kudadisi juu ya masuala ya biashara na wakati huo huo wale waliofanikiwa ni wachoyo kuhamasisha na kutoa ushauri kwa wajasiriamali chipukizi.

“Ndiyo maana unakuta kwa wale waliosoma wanang’ang’ania kutafuta ajira badala ya kuanzisha biashara matokeo yake wanajikuta wamekaa bure mtaani bila kazi kutokana na ugumu wa ajira,” anasema.

Kero zinazowakumba wafanyabiashara nchini

Anasema moja ya kero kubwa zinazowakera wajasiriamali nchini ni wingi wa kodi na kuiomba serikali kuweka muundo mzuri wa ulipaji kodi badala ya kila taasisi kuwasumbua wakati wa utozaji kodi.

“Yaani mwanangu sisi wafanyabiashara  tuna shida sana kila wakati tunatembelewa na watoza kodi ukikaa kidogo anakuja mwakilishi kutoka Zima moto, kidogo tena anakuja mtu kutoka wizara ya afya, mara wengine wanataka kupuliza mbu basi inakuwa kero tu ni vyema ukawepo mfumo mmoja wa ulipaji kodi bila kubugudhi mfanyabisahara,” anasema Hadija.

Ndoto yake

Aidha, anasema matarajio yake ni kuona Kampuni  inaendelela kukua zaidi hadi kufikia kiwango cha kuingia kwenye soko la mitaji na hivyo kuweza kuuza hisa.

“Iwapo nitafanikiwa kufika huko basi nina uhakika wa kuboresha zaidi bidhaa zangu na kuongeza bidhaa mpya zikiwemo Pampasi kwa ajili ya wagonjwa watu wazima, kutengeneza mipira ya mikononi (gloves), ili kukidhi soko la Afrika Mashariki.

Wito wake kwa Serikali

Pamoja na mambo mengine anaiomba kuwepo kwa ushirikiano mzuri kati ya wajasiriamali hasa wanawake na taasisi za kiserikali zikiwemo wizara mbalimbali ambapo kwa upande wake anasema angependa kushirikiana na wizara za Afya, wizara ya Elimu na pia wizara ya  Ulinzi.

“Ili niweze kupanua soko la bidhaa zangu ninahitaji kushirikana na wizara hizo ambapo nitaweza kusambaza kwa wafungwa, mahospitalini hasa wodi za wazazi, na pia mashuleni,” alisema.

Wito wake kwa wanawake

Amewataka kuwa na uthubutu wa kuanzisha biashara hata kama wana mtaji mdogo na pia kutokuwa na haraka ya kupata faida tabia ambayo  amesema wajasiriamali wengi wanaochipukia wanayo.

Lengo lake

Anasema lengo lake kubwa ni kuhakikisha anauza bidhaa hizo kwa bei ya chini na zikiwa katika ubora wa kimataifa na kuwataka watanzania kuthamini bidhaa zinazotengenezwa nchini zaidi.

Soko lake kwa sasa

Anasema kwa sasa kiwanda chake kina uwezo wa kutengeneza taulo 400 kwa dakika moja na hivyo akipata soko zaidi ataweza kukidhi mahitaji ya soko la ndani ya nchi.

Bidhaa zake anauza zaidi nje ya nchi na ndani  nchi  ikiwemo  hospitali za Aghakhan, maduka makubwa ya Shoppers Plaza, wateja wengine wapo visiwani Zanzibar, migodini, mashirika ya kimataifa,  T-Mark,  na pia anasema  mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete alikuwa akinunua kwa ajili ya kusaidia shule za watoto wa kike yatima.

“Iwapo nitapata ushirikiano mzuri nina uhakika wa kutoshelelza mahitaji ya watanzania kwa asilimia 60 kwani tuna mtambo wa kisasa unaotumia teknolojia ya kisasa kutoka Ujerumani.