Home Habari MWIJAGE: MAGENDO YAMEUA VIWANDA

MWIJAGE: MAGENDO YAMEUA VIWANDA

202
0
SHARE

NA OSCAR ASSENGA, TANGA.


BIASHARA za magendo zimetajwa kuwa moja ya sababu kubwa ya kuua viwanda vingi nchini na hasa mkoani Tanga.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri  wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alipokuwa jijini Tanga kwa ziara ya kikazi.

Mwijage amesema kuwa biashara za magendo zina madhara makubwa kwa viwanda nchini.

Alisema biashara za namna hiyo hazina tofauti na uhaini na ugaidi na kwamba ili kukabiliana na hali hiyo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Tanzania ya viwanda ni lazima kuwekwe mikakati thamiti na imara ya kuutokomeza mtandao wa wahusika wa biashara za magendo.

Alisema Tanga ni moja ya mikoa iliyokuwa na viwanda vingi nchini, lakini kwa sasa vingi vimekufa kwa sababu  mbalimbali ikiwamo magendo.

“Biashara za magendo ni adui wa viwanda, wote mnajua Tanga ilikuwa na viwanda vya kutosha tu, lakini leo vingi havipo, pamoja na mambo mengine, lakini magendo yamechangia kuviua,”alisema.

Katika ufunguzi wa maonyesho ya biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga, Mwijage alisema uwapo wa bandari bubu mkoani hapa pia unachangia kunyong’onyeza soko la bidhaa za ndani.

Alisema tatizo hilo la Bandari bubu si la Tanga pekee, bali lipo kwenye maeneo mengi yaliyopitiwa na bahari nchini hali inayochangia kudhoofisha bidhaa za ndani.

Mbali na bandari bubu kuchangia kudhoofisha bidhaa za ndani, lakini pia zinaikosesha Serikali mapato, ambayo huenda yangesaidia kuboresha huduma mbalimbali za jamii.

“Mkoa wa Tanga unakadiriwa kuwa na Bandari bubu zipatazo 45 ambazo

zimekuwa zikifanya kazi usiku na mchana katika wilaya za Mkinga,Tanga,Pangani na Muheza.

“ Kazi kubwa ya bandari hizo ni kuingiza bidhaa kutoka

nchi mbalimbali kwa njia za magendo hali inayoathiri bidhaa za ndani na kuikosesha mapato serikali,”alisema.

Alisema bidhaa za magendo zinapoingia nchini zinaondoa ushindani sokoni kwa sababu zenyewe hupatikana kwa bei rahisi kutokana na kutolipiwa kodi.

Anasema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali kuona namna

ya kulipatia ufumbuzi suala hilo, lakini jambo hilo limeonekana kuwa gumu kumalizwa kutokana na kuwa na mtandao mpana.

Hata hivyo aliahidi kuhakikisha Serikali inatafuta dawa ya kukabiliana na tatizo hilo sugu.

“Ukiangalia leo hii viwanda vingi vimekufa ambavyo vilikuwa na uwezo

wa kufanya kazi, lakini sasa havifanyi na ukichunguza kwa umakini utagundua  kuwa  biashara

za magendo zimechangia kuua viwanda kwa asilimia kubwa.

“Ni vema tatizo hili tukaliwekea mipango mizuri ya

kuhakikisha tunatokomeza biashara za magendo ili kuweza kuendana na sera

ya viwanda ambayo itakuwa ni muhimili muhimu wa kufungua uchumi wa

kati ifikapo mwaka 2025 kwa kuufikia kipato cha dola 3000 .

“Bidhaa nyingi zinaingizwa kwa njia ya magendo sana hali inayosababisha

soko la bidhaa za ndani kushuka na huu ni sawa na uhaini

na ugaidi kwa sababu bidhaa za magendo halizipiwi ushuru na madhara

yake ni makubwa sana kwa ukuaji wa uchumi “Anasema.

Katika kuhakikisha suala hilo loinashughulikiwa kwa vitendo, Mwijage alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Tanga na

wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha bidhaa za magendo haziingia nchini kwasababu madhara yake ni makubwa kwa Taifa.

Sambamba na hayo lakini pia Mwijage aliiagiza Mamlaka ya Bandari

Tanzania (TPA) kufanya msako wa kuzibaini na kuzifunga Bandari bubu

Akizungumzia suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella aliahidi kulishughulikia kikamilifu suala hilo.

Aidha alisema ipo haja ya Serikali kuangalia namna ya kuboresha masoko ya bidhaa za Tanzania hatua ambayo itasaidia kuinua na kukuza uchumi wa

mkoa na Taifa kwa ujumla.

Shigela alisema pamoja na mambo mengine, lakini ili tufikie hatua ya kuwa na viwanda vikubwa ni lazima tuanze na viwanda vidogo vidogo ambavyo

Vitaongeza thamani.

“Niwaahamasishe Watanzania na wakazi wa mkoa wa Tanga kuwekeza

kwenye viwanda vidogo vidogo ili kusaidia kuinua maendeleo.”alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Tanga, Deo Luhinda amezipongeza juhudi za Serikali katika kuhakikisha sekta ya

viwanda hapa nchini inaimarika.

Hata hivyo aliiomba  Serikali iongeze nguvu katika kujenga Bandari mbili

mkoani Tanga ikiwemo ya Mwambani kwa madai kuwa hiyo ndio njia pekee inayoweza

kuondoa msongamano kwenye Bandari ya Dar es Salaam.