Home KIMATAIFA KURA YA SIRI NA TUHUMA DHIDI YA ZUMA

KURA YA SIRI NA TUHUMA DHIDI YA ZUMA

109
0
SHARE
President Jacob Zuma officially opens the National House of Traditional Leaders (NHTL) at the Old Assembly Chambers, Parliament, Cape Town. South Africa. 27/02/2014. Siyabulela Duda/GCIS.

President Jacob Zuma officially opens the National House of Traditional Leaders (NHTL) at the Old Assembly Chambers, Parliament, Cape Town. South Africa. 27/02/2014. Siyabulela Duda/GCIS.
President Jacob Zuma officially opens the National House of Traditional Leaders (NHTL) at the Old Assembly Chambers, Parliament, Cape Town. South Africa. 27/02/2014. Siyabulela Duda/GCIS.

CAPE TOWN, SOUTH AFRICA

Siku moja kabla ya Bunge la Afrika ya Kusini kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma Jumanne iliyopita, Mnadhimu Mkuu wa chama chake cha ANC Jackson Mthembu alisema haitajalisha chochote iwapo kura hiyo itafanywa kwa uwazi au kwa siri, kwani Wabunge wa ANC hawatapiga kura kuunga mkono kura hiyo dhidi ya rais wao.

Kura hii ya sasa ya kutokuwa na imani na rais zuma itakuwa ni ya saba na sita zilizopita alishinda. Harakati za vyama vya upinzani, zikiongozwa na mwanasiasa machachari Julius Malema wa chama cha Economic Freedom party (EFF) vilikuwa vinadai kwamba Zuma alikuwa anashinda kwa sababu kura ilikuwa inapigwa kwa siri, na kuongeza kwamba iwapo itafanyika kwa uwazi atang’oka tu.

Kwa upande wake Spika wa Bunge hilo Bi Baleka Mbete alidai kwamba anazuiwa kikatiba kufanya kura ya siri jambo ambalo baadaye liliamuliwa na Mahakama Kuu ya Katiba ya nchi hiyo mwishoni mwa mwezi Juni katika uamuzi kwamba Spika hafungwi kikatiba kuendesha kura ya siri – ni uamuzi wake tu na iwe kwa masilahi mapana ya taifa na kukuza demokrasia.

Katika uamuzi wa wengi katika jopo la majaji waliosikiliza shauri lilopelekwa na vyama vya upinzani, Jaji Mkuu Mogoeng Mogoeng alisema kwamba si kweli kwamba Spika Mbete, kama anavyodai, hana madaraka kikatiba ya kuamua upigwaji wa kura ya siri.

Uamuzi ule ulikuwa na maana kwamba iwapo wapinzani wataomba ipigwe kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma, Spika Mbete hataweza tena kutoa hoja kwamba anafungwa kikatiba kuruhusu kura ya siri.

 

Tuhuma dhidi ya Zuma

Zuma ambaye aliingia madarakani mwaka 2009 amekumbwa na kashfa nyingi za ufisadi, wakati ambapo uchumi wa nchi hiyo ukiporomoka na ukosefu wa ajira ukiwa tatizo sugu.

Kabla ya kuingia madarakani zuma alikutwa hana hatia katika kesi ya ubakaji ya mwaka 2006, dhidi ya mwanamke aliyekuwa wa umri mdogo na aliyekuwa amethibitishwa kuwa na virusi vya ukimwi.

Ushindi huo iliegemea ushahidi wake mwenyewe kwamba tendo lile la ngono lilikuwa la ridhaa ya wawili. Aidha alishangaza wengi aliposema kwamba baada ya tendo lile la ngono alioga ili asijiambukize na virusi vya ugonjwa ule.

Zuma pia ameibua tuhuma nyingi kuhusu maisha yake ya kuwa na wake wengi – kwani sasa hivi ana wake wanne na kwamba anao watoto kadha aliowapata nje ya ndoa.

Na sasa hivi kuna harakati za kuzirejesha mahakamani tuhuma 783 za ufisadi ambazo zilifutwa muda mchache tu baada ya kushinda urais mwaka 2009.

Tuhuma hizo zinahusiana na sakata lile la ufisadi katika mkataba wa ununuzi wa silaha uliotiwa saini mwaka 1999 wakati Zuma akiwa Naibu Rais. Tuhuma hizo zilifutwa na waendesha mashitaka ambao walidai kwamba madai yale yalisukumwa na mambo ya kisiasa. Wengi walipinga kuondolewa tuhuma hizo wakisema ilikuwa ni njia ya kumsafishia njia ya kushinda uchaguzi.

Ukarabati wa makazi ya Nkhandla

Lakini hakuna kashfa ya ufisadi iliyokuwa mbaya zaidi kwake kama kama ile iliyohusu ukarabati wa makazi yake binafsi ya kijiji chake cha Nkhandla, katika jimbo lake la Kwazulu.

Mwaka 2014 mkuu wa taasisi ya kupambana na ufisadi nchini humo Thuli Madonsela, baada ya uchunguzi wa kina alisema Zuma alitumia fedha za walipa kodi kukarabati makazi yale yaliyogharimu Dola za Kimarekani 22 milioni.

Aprili mwaka jana Zuma alipona mchakato wa kutaka kushitakiwa na Bunge (impeachment) kutokana na kashfa hiyo, lakini hata hivyo aliamriwa na Mahakama Kuu ya Katiba na hazina ya nchi hiyo kulipa serikali rand 7.8 milioni – sawasa na Dolaarekani 588,000.

Kashfa kuhusu familia ya Gupta

Aidha Zuma anakabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi zinazoihusisha familia ya kibiashara ya Gupta, familia ambayo ilikuwa inapewa zabuni kubwa kubwa kutoka serikalini na pia ilikuwa na ushawishi mkubwa kwa rais katika uteuzi wake wa mawaziri na watendaji wakuu wengine wa serikali.

Mwaka jana mkuu wa taasisi ya kupambana na ufisadi nchini humo Thuli Madonsela alitoa ripoti iliyotoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa kina katika tuhuma hizi.

Mwezi Mei mwaka huu maelfu ya barua pepe zilivuja kwenye vyombo vya habari zilizoonyesha mahusiano ya karibu sana kati ya Zuma, maswahiba wake na ndugu watatu wa familia ya Gupta.

Barua pepe hizo zilionyesha kwamba wanafamilia hao wa Gupta walikuwa wanawakaribisha majumbani mwao mawaziri na wakurugenzi wa mashirika makubwa ya kiserikali na kuungano nao katika safari za anasa hadi kwao Dubai.

Aidha zuma alikanusha habari kwamba familia hiyo ya Gupta ilikuwa inamtayarisha makazi yake ya pili kule Dubai.

Desemba 2015 Zuma alimuachisha kazi Nhlanhla Nene, waziri wake wa fedha aliyekuwa kpenzi cha wengi na kumuweka Mbunge mmoja asiyejulikana. Wengi walipinga hatua hiyo na hatimaye alimuondoa na kumuweka Pravin Gordhan.

Machi mwaka huu alimfukuza kazi Gordhan, hatua ambayo ilizidi kudhoofisha imani ya wawekezaji. Aidha hatua hiyo iliirudisha chini uwezo wa Afrika ya Kusini kukopesheka kimataifa.

Mikwaruzano na Mahakama ya ICC

Machi mwaka jana Mahakama Kuu ya Rufaa, katika uamuzi wake ilishikilia hukumu kwamba serikali ya Zuma ilikiuka sheria kwa kushindwa kumkamata rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye anatakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, wakati alipokuwa anhudhuria mkutano wa nchi za Umoja wa Afrika (AU) Johannesburg Julai 2015.