Home Makala MAKUNDI YA WHATSAPP YANAVYOWEZA KUWA KICHOCHEO CHA KUKUZA KISWAHILI SANIFU

MAKUNDI YA WHATSAPP YANAVYOWEZA KUWA KICHOCHEO CHA KUKUZA KISWAHILI SANIFU

306
0
SHARE

NA CAESAR JJINGO, JOHANNESBUGR, AFRIKA KUSINI

MAENDELEO ya Teknolojia yamekuja na changamoto nyingi hasa katika matumizi ya lugha sanifu. Lugha zote zimekumbana na chanagamoto kubwa ya kuraribiwa kaytika maandishi, lakini pamoja na changamoyo hiyo teknolojia hasa mindandao ya kijamii kama WhatsApp na mingine ikitumiwa vyema inaweza kuwa kichochoe kikubwa katika kukuza lugha sanifu hasa Kiswahili.

Kiini kikuu cha makala haya ni mvutano wa kimawazo unaojitokeza mara kwa mara kati ya wajumbe  wa kundi la Whatsapp waliopo kwenye kundi moja waliomaliza darasa la saba mwaka 1991 katika moja ya shule zilizipo wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam Tanzania.

Kama makundi mengine mengi ya Whatsapp, kundi hili halina katiba. Shughuli za kundi hili zinaongozwa kutokana na tabia walizojijengea wanakundi kama raia yeyote mwema katika jamii. Hali hii pia inajitokeza kwenye matumizi ya lugha. Hakuna sehemu ambapo zimeorodheshwa lugha zinazopaswa kutumika kundini, ila Kiswahili na mara chache sana Kiingereza hutumika.

Kiswahili hutumika kama lugha ya mawasiliano ya kila siku. Kiingereza mara nyingi hutumika kwenye kuweka msisitizazo juu ya jambo. Kwa upande wa lugha ya Kiingereza, kwenye kundi hili, kuna sehemu kuu tatu ampapo lugha ya Kiingereza hujitokeza; (a) wakati wa kusalimiana asubuhi.

(b) Endapo kuna matini (zikiwepo matini sikilizi, picha na katuni) zimeletwakundini kutoka kwenye kundi jingine. Uwepo kwa matini za Kiingereza kundini huwagawa wanaWhatapp kama mara tatu hivi; (i) Ni wale wachacha watakaoisoma na kuielewa matini hiyo; (ii) wale watakaoshindwa kuisoma matini hiyo kutokana na urefu wa matini au ugumu wa lugha kwenye matini; (iii) kuna watakaoisoma na kuelewe aidha kwa juu juu au kwa Kiswahili ila hushindwa kuijadili matini hii kwa Kiingereza kama ilivyoandikwa;

(c) Sehemu kuu ya mwisho ambapo Kiingereza hujitokeza kwenye kundi hili ni pale; (i) Mwanakundi  anapoamua kugeuza au kichanganya misimbo ya lugha kati ya Kiswahili na Kiingereza pasipo kuzingatia uasilia wa neno au maneno yatakayoundwa na maana zitakayojitokeza. (ii) Pale mwanakundi anapoamua kuandika sentensi sahili za Kiingereza bila kujali muundo na maumbo yanayosanifisha sentensi za Kiingereza na maana zinazotarajiwa.

Kwa kifupi, lengo kuu la makala hii fupi ni kujaribu kuibua na kuchochea fikra za kujijengea mtazamo mpya baina ya wafuasi wa mitandano ya kijamii, hususani wale waliopo kwenye makundi ya Whatapp na kuibua fikra binafsi ambazo wanaWhatapp huzitumia pasipo kutambua kuwa zina mchango kwa namna moja au nyingine kwenye kukuza au kuzorotesha utumiaji wa lugha sanifu katika makundi ya Whatsapp na hata nje ya makundi hayo kwa maana katika matumizi ya kawaida ya lugha.

Lakini je watumiaji wa lugha ya Kiswahili wanawezaje kukuza matumizi ya lugha sanifu? Kuna mitazamo kadhaa innayochagiza matumizi sahihi ya lugha sanifu ya Kiswahili kwenye makundi ya WhatsAppha ukiwemo mtazamo wa kumsahihisha mzungumzaji au mwanakundi aliyechangia kama amefanya makosa.

Mtazamo huu ni muhimu lakini unahitaji maarifa mahususi kwa maana mkosoaji anapaswa kuwa ni mtu anayeifahamu vyema lugha, mtu ambaye anauelewa wa matumizi sahihi ya maneno katika muktadha husika na si hivihivi tu.

Katika makundi mengi ya WhatsApp hakuna kanuni za matumizi ya lugha, lakini baadhi ya makundi yenye msimamo  na mtazamo wa kukuza Kiswahili kwa mfano kuna watu wenye maarifa juu ya lugha ya Kiswahili na anaweza kumsahihisha mwanakundi mwingine aliyekosea?

Usahihishaji unaozungumziwa kwenye makala hii ni ule wa mwanakundi kummsahihisha mwingine kwenye lugha kama Kiswahili hasa Kiswahili cha maandishi. Tunakubaliana kuwa nchini Tanzania, lugha ya Kiingereza ni lugha ya nyongeza. Hapa lugha ya nyongeza inatumika kama lugha moja au zaidi ambazo mtu hujifunza baada ya au wakati ameshaanza kuzungumza lugha yake ya kwanza. Kwa watanzania wengi haswa waishio mijini, lugha yao za kwanza ni lugha ya Kiswahili.

Makundi mengi ya WhatsApp yamefikia kiwango cha kitaifa na Kimataifa kwa maana ya kwamba yanajumuisha watu walipo ndani ya Tanzania na hata nje ya mipaka ya Tanzania, Watanzania wazawa na wasio wazawa wa Tanzania, kama ilivyo kwa mwandishi wa makala haya.

Kwenye makundi mengi, hasa ya wasomi kwa mfano, kumekuwa na mchanganyiko mkubwa wa matumizi ya lugha huku wengi (wasomi) wakiona pengine ni ufahari sana kutumia Kiigereza katika kuonyesha hadhi za usomi wao.  Itaendelea wiki ijayo

Mwandishi wa Makala haya ni Mwanafunzi wa Uzamivu wa Lugha, Chuo cha Stellenbosch, Afrika Kusini.