Home Habari KKKT NAO WAWASOMEA ‘ALBADIR’ WALIOMPIGA LISSU

KKKT NAO WAWASOMEA ‘ALBADIR’ WALIOMPIGA LISSU

208
0
SHARE

NA OSCAR ASSENGA, TANGA


ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini- Mashariki, Dk. Stephen Munga ameadhimisha ibada maalumu ya kulaani mashambulizi yaliyofanywa na ‘watu wasiojulika’ dhidi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. RAI linaripoti.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni wiki chache zimepita baada ya baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu mkoani humo kusoma dua maalumu maarufu kama ‘Ibada ya Albadir’ kwa ajili ya watu hao wasiojulikana.

Akizungumza katika ibada hiyo iliyofanyika mjini Tanga hivi karibuni Askofu Munga yupo tayari kutengwa na kama

akionekana ameegemea upande wowote kwani amani haina chama wala itikadi za kisiasa.

Alisema mtaji mkubwa wa watu wanaohangaika na maisha yao ni amani hivyo pale suala hilo linapotoweka hata mihangaiko yao inakuwa maradufu jambo ambalo linakwamisha fursa za kujiingizia kipato.

“Tanzania ni nchi yetu, nyumba yetu ambayo Mungu ametujalia tuishi lakini nyumba hiyo hivi sasa imeingia joka na amani hakuna tena zaidi ya kuishi kama wakiwa. Watanzania lazima watambue kuwa amani haina chanzo na bila kuangalia itikadi za kisiasa za CCM na Chadema kila mmoja anapaswa kuidumisha “ alisema.

Alisema matukio ya watu kuvamiwa kama ilivyotokea kwa Lissu na kupigwa risasi yamekuwa matukio ya kawaida kwa sababu amani imetoweka.

“Kuwepo kwa kadhia hiyo lazima watu tuongee kupitia kwa Mungu ili kuifanya nyumba iweze kuwa na amani ambayo ndio msingi mkubwa wa maendeleo. Hatuhitaji jambo lolote kwa Serikali au vyombo vya dola zaidi ya amani ndio maana tunalipa kodi, hawa watu wasiojulikana wasiokamatwa ni chanzo cha nyumba yetu kutokuwa na amani“ alisema.

Aidha, aliliomba Jeshi la Polisi kutumia weledi wake kuhakikisha hali ya usalama inarejea nchini ili watu waishi kwa amani kwa maendeleo ya Taifa.

“Lakini pia niwaambie tusicheze na Mungu wetu linapokuja hitaji kwa ushabiki wa aina yoyote ile kwani Tanzania tokea uchaguzi kuisha kumekuwa na kutokuelewana. Viongozi waliopo madarakani wanakazi kubwa ya kuliunganisha Taifa hili  kwa kuwa umoja na mshikamano ndio chanzo cha kuwa na amani ambayo

ndio nguzo kuu ya mafanikio kwa nchi yoyote dunia.

“Tumekuwa na mivutano ya kisiasa ambayo imetufikisha hapa. Mivutano hii haijatutoka kwenye usingizi, visa na visasi vya uchaguzi inabidi tumuombe Mungu atuondolee hali hiyo kwani sio nzuri “ alisema.

Alisema kazi ya Rais ni kuunganisha Taifa hivyo lazima Serikali itoemwelekeo mmoja kwani hata huko kunyoosheana vidole sio jambo nzuri kwa mustakabali wa nchi.

“Lakini pia hatuna umoja, mgawanyiko ndio joka kubwa ambalo limeingia hapa nchini kwani hakuna uzalendo pasipokuwa na umoja ndani ya nchi ya namna hiyo hakuna amani.

“Watu wanasema Askofu hauogopi lakini kwa jambo ambalo linazungumzia suala la amani tuombe tukamwambie Mungu nchi iweze kubadilika kwani jambo hilo hata Yeremia alisema atalihubiri bila kuchoka“ alisema.

Anasema watu wanataka amani na umoja katika Taifa kwani Bunge linaweza kuzungumza mambo yake kama Bunge lakini pia tumemchagua Rais atuunganishe na mataifa na kuendelea amani iliyokuwepo “ alisema.