Home Habari VIONGOZI WENGI HAWAJUI UMUHIMU WA TAFITI NA UTENDAJI WAO NI WA...

VIONGOZI WENGI HAWAJUI UMUHIMU WA TAFITI NA UTENDAJI WAO NI WA KIMAZOEA

258
0
SHARE

NA THADEI OLE MUSHI

ULISHAWAHI kujiuliza makabati yaliyo kwenye ofisi za maprofesa wetu na madokta Wetu kwenye vyuo vikuu yana nini? Si makabati ya nguo yale au ya vyombo vya nyumbani.

Kama ulilikuwa hujui basi leo nakujuza kuwa ni tafiti zilizofanywa aidha na wao wenyewe au wanafunzi wao waliokuwa wanawasimamia katika kipindi cha kufanya tafiti kama mojawapo ya requirements ya kuhitimu level flan ya elimu.

Kwa kawaida na kitaalamu huwa tunapofanya tafiti zetu, zote huangukia kwenye moja ya malengo matano ya kiutafiti yaliyopo kitaalamu.

Pindi unaposikia mtu yeyote anafanya utafiti basi lazma mwisho wa utafiti wake utaangukia kwenye moja ya malengo yafuatayo:-

Ugunduzi (exploration)- Je mtafiti alifanya utafiti kwa lengo la kugundua kitu? mfano wapelelezi wengi waliokuwa wanakuja barani Africa kupeleleza walifanya tafiti ya aina hii.

Description – Je mtafiti anafanya utafiti kwa lengo la kufahamu tabia za jambo kitu fulani? Mfano unataka kufahamu tabia za mnyama fulani au hali ya hewa ya mahali nk utaufanya huu.

Explanation – Je Mtafiti anataka kufahamu kwa nini jambo fulani limetokea? Mfano kuibuka kwa kipindupindu mtaalamu wa utafiti anaweza kufanya utafiti kuelezea sababu za kuzuka kwa ugonjwa huo.

Prediction:- Je mtafiti anataka kufahamu jambo litakalotokea hapo baadaye? Mfano wizara kuwapa wanafunzi mitihani ya mock kabla ya national exams lengo nikupata picha ya baadaye.

Control – Je Mtafiti ana lengo la kutoa mbinu za kukabiliana na tatizo flani lililotokea? Mfano utafiti wa kubaini njia nzuri za kudhibiti ueneaji wa malaria.

Hakuna utafiti unaoweza kutoka nje ya malengo haya matano niliyoyaainisha hapa kitaalamu.

Malengo haya ndiyo yanayoipa taaluma utafiti umuhimu mkubwa sana kwa kuwa kwa kutumia malengo hayo tunaweza kutabiri jambo jema au baya linaloweza kujitokeza baadaye, tunaweza kuzuia jambo baya lisitokee, tunaweza kufahamu kwa nini jambo fulani limetokea, tunaweza kufahamu tabia na mienendo ya mambo, na mwisho kabisa tunaweza kugundua vitu vyenye manufaa.

Ndiyo malengo yanayoweza kutuambia mbegu bora ya pamba au kahawa ni ipi, ndio malengo yanayoweza kutuambia ni lini tatizo la njaa litatokea, ni malengo yanayoweza kutuambia ni njia zipi tutumie kumaliza tatizo la ajira nchinu na kadhalika. Malengo haya yamebeba kila tatizo kwenye maeneo yetu.

Kwa bahati mbaya sana viongozi wetu wa kisiasa wameshindwa kuunganisha taaluma hii ya utafiti na matatizo tuliyoanayo katika jamii katika maeneo yetu.

Viongozi wetu wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea au kwa kutumia tafiti za zamani ambazo haziendani na matatizo tuliyonayo kwa sasa.

Tumekuwa tukisikia viongozi wetu wakifunga safari kwenda nchi za nje kama China na Indonesia kwenda kujifunza ni kwa namna gani wamefanikiwa katika uzalishaji wa mpunga.

Madai yao ni kutaka kufanana na China ambayo ina hali tofauti ya hewa na sisi, wana teknolojia tofauti na sisi na tunataka China tuihamishie pale Kilombero kwa kuitembelea.

Wanaenda mpaka China wakati pale SUA kuna maprofesa wengi tu wa Kilimo na kwenye makabati yao kumejaa tafiti mbalimbali za kilimo na hata za kuboresha kilimo cha mpunga.

Cha kuchekesha zaidi ni kwamba wanaoenda kujifunza jambo nje si watendaji/wataalamu bali ni viongozi wa kisiasa wakisharudi toka kujifunza makarabrasha wanayaweka kwenye makabati na hawayatendei kazi wanaishia kupiga picha na kuzirusha kwenye mitandao ya kijamii wakiwa na umaridadi wa kutosha na mazingira yanayovutia ya hotel za kifahari nje ya nchi.

KWA NINI NIMEYASEMA HAYA?

Kwanza naangalia juhudi za viongozi wetu vijana waliopewa uongozi siku za karibuni.

Kasi yao katika utendaji ni ya hali ya juu kabisa hili sina ubishi nalo na kwa hili nawapongeza sana.

Ni aina ya viongozi ambao hata kama utampigia simu usiku wa manane anaweza kukusaidia. Ni viongozi ambao wana matamanio makubwa sana ya kuacha alama kwenye utendaji wao.

Kitu kimoja wanachokikosa ni kutembea kwenye nyayo zile zile walizotembea wazee wetu katika utendaji wao. Yaani wanatenda kwa kutumia mbinu zile zile za kina Augustino Lyatonga Mrema za kuamka usiku na kuzurura na polisi kwa madai ya kukamata wahalifu.

Nilitegema kizazi hiki kiwasumbue sana wataalamu wa research kufanya tafiti katika maeneo yao ili wapate findings na hatimaye kwa pamoja watengeneze mapendekezo ya kutatua matatizo hayo. Si ajabu kuna viongozi hawana hata namba za simu za maprofesa na madaktari waliojazana kwenye vyuo vyetu.

Maprofesa na madaktari hawa wakikosa kazi ndio hawa unawakuta kila siku wapo kwenye vituo vya Radio na TV wakiisifia serikali au kuiponda kwa lengo la kutafuta mlango wa kuingilia kwenye madaraka.

Kwa mfano nikimwangalia Mkuu wa Mkoa wa Daresalam anavyofanya kazi nafarijika sana ila tatizo hakuna watu technical waliopo nyuma yake wanaomshauri namna bora ya kutumia rasilimali alizonazo kuleta matokeo yenye tija zaidi.

Chukulia mfano tu swala la Ujenzi wa Ofisi katika mkoa wa Daresalam ni jambo jema ila hakuna tafiti za karibuni zinazounganisha tatizo hilo la kutokuwepo kwa ofisi na matokeo/ufaulu wa wanafunzi (hakuna conceptual framework au theoretical framework zinazoliunganisha tatizo na kinachofanyika).

Kwa kuwa utoaji wa elimu bure umesababisha ongezeko la wanafunzi mashuleni basi hapa tungejikita katika ujenzi wa madarasa ili kutatua tatizo linalotaka kujitokeza.

Kwa kutumia sera ya elimu ya sasa kuwa elimu ya msingi ni hadi kidato cha nne tunatarajia siku za usoni uhaba mkubwa wa madarasa katika shule zetu za serikali.

Yote kwa yote nimpongeze kwa uthubutu wa hali ya juu alionao. Ni kasoro ndogo tu zinajitokeza na kama ataamua kizifanyia kazi basi kazi zake zitakuwa bora zaidi.

Nitoe rai kwa vyuo vyetu vikuu kuwa sehemu ya kusaidia utatuzi wa matatizo ya kijamii.

Ni jambo la kushangaza tafiti za Twaweza na RADET zinazohusiana na mambo ya kisiasa kupigiwa kelele sana na kutangazwa kila mahali wakati kila siku vyuo vyetu vinarundika tafiti ambazo zimebeba namna ya utatuzi wa matatizo yetu.

Hawa Twaweza na Radet wamekaa kisiasa sana hivyo ni vigumu kuamini sana tafiti zao ndio maana naweka mkazo kwa vyuo vyetu vikuu ambavyo hupokea fedha kwa ajili ya uendeshaji wa tafiti.

Wasomi wetu waachane na kupika takwimu kwa lengo la kufurahisha wanasiasa badala yake watoe taarifa za kitafiti za kweli ili tuweze kujinasua tulipo na tusiende tena China kujifunza tunawezaje kulima mpunga pale Kilombero.

Viongozi wetu wakubali sasa kubadilika na watumie tafiti hizi na waruhusu zifanyike kwa wingi ili zitusaidie.

 0712702602.