Home Habari DK BISIMBA: KUZINGATIA SHERIA KUTAMALIZA UKATILI

DK BISIMBA: KUZINGATIA SHERIA KUTAMALIZA UKATILI

205
0
SHARE

Na JOHANES RESPICHIUS

NI maswali mengi ambayo unaweza kujiuliza pale unaposikia vitendo vya ukatili hasa kwa wanawake na watoto vinazidi kuongezeka katika jamii ilihali Asasi, Taasisi na Mashirika mbalimba ambayo kila kukicha yamekuwa yakifanya shuguli za utetezi pamoja na kutoa elimu juu ya masuala hayo.

Ukatili ni kitendo kinachoweza kusababisha madhara, maumivu, kulazimisha, kunyima uhuru, bila kujali vimefanyika kisiri ama kwenye kadamnasi.

Kundi la wanawake na watoto ndiyo yamekuwa yakifanyiwa vitendo vcya ukatili kwa kiasi kikubwa jambo ambalo limekuwa likiwasababishia athiri nyingi ikiwamo kuathirika kisaikolojia, kupata majeraha, ulemavu wa kudumu na hata vifo.

Miongo kadhaa iliyopita vitendo vya ukatili vilikuwa kwa kiasi kikubwa ambapo yalishuhudiwa matukio mengi ya mauaji ya vikongwe, watu wenye ualbino ambayo mengi yalikuwa yakiripotiwa kutekelezwa hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Lakini vitendo hivi katika miaka ya hivi karibuni vilionekana kupungua hiyo ikichangiwa msukumo mkubwa wa serikali na wadau wa utetezi wa haki za binadamu kuamua kushirikiana kwa pamoja katika mapambano dhidi ya matukio hayo.

Hali hii imekuwa tofauti kwa mwaka huu ambapo inaripotiwa kuwa vitendo vya ukatili ikiwamo ubakaji, ulawiti, unajisi na usafirishaji haramu wa binadamu umeongezeka.

Ripoti iliyotolewa wiki iliyopita na Jeshi la Polisi nchini iliyotolewa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, kuhusu matukio mbalimbali ambayo yametokea kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu inaonyesha vitendo hivyo kuonezeka.

Katika ripoti hiyo jeshi hilo linasema  matukio ya ubakaji, ulawiti na kunajisi watoto yameongezeka kwa kiasi kikubwa ambapo katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2017 makosa ya kulawiti, mauaji, kutupwa kwa watoto na usafirishaji binadamu yameripotiwa matukio 11,620 ukilinganisha na 11,513 ya mwaka jana.

Boaz anasema kuwa makosa ya ubakaji yalilipotiwa 7,460 kutoka 6,985 mwaka jana huku makosa ya kunajisi yakiwa ni 25 kati ya 16 mwaka jana.

“Makosa yanazidi kuongezeka kuliko matukio mengine yoyote ambapo inaripotiwa kuwa yanaonekana kusababishwa na mmomonyoko wa maadili, ushirikina na tamaa za kimwili,” anasema Boaz.

Jambo la kushanganza ni kuwa wakati matukio ya ulawiti, ubakaji na ujajisi yakiongezeka makosa ya jinai ikiwemo ujambazi wa kutumia silaha, uvunjaji ,wizi wa magari pamoja n mifugo yamepungua kutoka 34,830 mwaka 2016 hadi kufikia 29,677 sawa na asilimia 14.8.

Swali linakuja Je matukio haya ya ubakaji na ulawiti yanaongezeka kutokana na jamii kupata uelewa wa kutosha hivyo  kuweza kuyaripoti kwenye vyombo vya usalama?.

Au watu wanaofanya vitendo hivyo vya kikatili bado wapo kwenye ulimwengu wa kuamini ushirikina au bado kuna kulegalega kwenye utelezaji wa sheria mbalimbali.

Hivyo watu wanaamua kujichukulia sheria mkono pasipo kuzingatia utawala wa kishreia au bado wanaamini ule msemo wa kwamba sheria zinawekwa ili zivunjwe, kama hali iko hivyo nguvu kubwa kutoka kwa serikali, wadau na mashirika mbalimbali inahitajika hususan kwenye utoaji wa elimu.

Kutokana na hali hiyo RAI limemtafuta, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC, Dk Helen Kijo-Bisimba ili kujua ongezeko hili linaashiria nini hasa katika kipindi hicho ambacho utandawazi umetawala.

Dk Bisimba anasema masuala ya maadili na ulinzi kwa watoto sio mzuri katika jamii zetu kitu ambacho kinatakiwa kuangaliwa kwa jicho la tatu.

“Hata katika kipindi cha nyuma tumekuwa tukionesha namna gani tatizo hilo linavyoendelea kukua na sasa hivi unaona kweli limekua hivyo kuna kazi kubwa ya kufa nya kuhakikisha tunaondokana na tatizo hili.

“Mfano suala la maadili, kuchukua hatua stahiki za kijinai kwa watu wanaofanya ukatili huu kwa watoto. Pia ongezeko hili linaweza kusababishwa na kwamba watu na jamii kwa ujumla wamepata uelewa wa kutosha kuhusu suala hili hivyo kuwa na mwamko wa kutosha wa kuyaripoti matukio hayo kwenye vyombo vya usalama.

“Nyakati za nyuma watu wengi walikuwa bado hawajajua umuhimu wa kuripoti vitendo hivi pale vinapotokea kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ya kujua wapi wanaweza kuyaripoti, kukwepa aibu pamoja na kuogopa vitisho hivyo kuamua kuyamaliza kimya kimya,” anasema Dk Bisimba.

Anasema licha ya watu wengi kupata uelewa juu ya vitendo ya ukatili hivyo kuchukua hatua ya kwenda kuyaripoti katika vyombo vya sheria ili hatua zaidi zichukuliwe lakini kuna ongezeko la matukio yenyewe.

Matukio haya yanatokea kwa watoto kwa sababu unaweza kukuta mtoto anachiwa analala na watu wakubwa, kuachwa kwenda kucheza sehemu ambayo mzazi anaweza asiwe karibu naye.

“Kwahiyo kuwa karibu na watoto kuwafuatilia ili zikianza kuonekana dalili waweze kuchukua hatua za haraka kabla mtoto ajaathiriwa zaidi jambo ambalo linaweza kumletea matatizo makubwa ili wahusika wachukuliwe sheria stahiki,” anasema Dk Bisimba.

Aidha kwenye upande wa serikali amoja na wadau wengine, elimu iendelee kutolewa kwa kiasi kikubwa zaidi ili kuongeza uelewa wa masuala hayo, pia kuhakikisha wale wanaopatika na hatia kwa makosa ya kuhusika kufanya vitendo vya ukatili wachukuliwe hatua kali na kwa haraka.

“Kwa sababu watu wengine wamekuwa wakienda wanaambiwa wamnalizane kindugu kwa sababu wanaogopa kama ni ndugu ametenda ukatili huo atachukuliwa hatua kubwa kwahiyo wanaamua kufuta kesi badala ya kuchukua hatua za kisheria.

Hali hii ndiyo maana watu wengine wamekuwa wakifanya vitendo hivi kwa makusudi wakijua wakienda mahakamani wataambiwa wayamalize kindugu hivyo wamekuwa hawaogopi kama kuna sheria,” anasema Dk Bisimba.

Anasema sheria zilizowekwa zisipofuatwa panakuwa hakuna utawala wa kisheria kwahiyo kila mtu hufanya anavyotaka hivyo ni muhimu vyombo vya sheria kufuata sheria na kufanya kila kitu inavyopaswa.

Aidha anasema kuwa imefika wakati wa kila mtu kutekeleza majukumu yake kulingana na nafasi aliyonayo katika ulinzi wa mtoto, kwa wazazi kuhakikisha wanawalinda watoto wao na vyombo vya dola kusimamia sheria zilizowekwa.