Home Makala Kimataifa MAZUNGUMZO YA AMANI BURUNDI VURUGU TUPU

MAZUNGUMZO YA AMANI BURUNDI VURUGU TUPU

438
0
SHARE

NA HILAL K SUED

Mapema mwezi huu, vikao vya mazungumzo kuhusu amani kuhusu Burundi yalivunjika ghafla bila ya kuwepo makubaliano yoyote.

Serikali ya Burundi ilikataa kukubali kwamba kulikuwapo mgogoro wowote uliohitaji kupatiwa suluhu. Serikali hiyo ilidai kwamba tayari ilikuwa imeshatayarisha rasimu ya uchaguzi wa 2020 huku viongozi wa upinzani (inaowatambua) ukitoa michango ya mapaendekezo na kukataa kusikiliza viongozi wa upinzani wanaowakilisha mazungumzo hayo.

Kuvunjika kwa mazungumzoi hayo hakukushangaza. Yalikuwa ni duru la nne la mazungunzo yasiyozaa matunda tangu Aprili 2015 pale nchi hiyo ilipotumbukia kwenye ghasia kubwa baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaz kugombea muhulu wa tatu.

Wengi waliona hatua hii ilikuwa ni ukiukwaji wa katiba ya nchi na kinyume cha Makubaliano ya Arusha ya mwaka 2000. Kulizuka maandamano makubwa katika mitaa ya Bujumbura na miji mingine na pia jarbio la jeshi kutaka kupindua serikali.

Hata hivyo Julai mwaka huo kulifanyika uchaguzi huo wa utata na kama ilivyotarajiwa Nkurunziza alishinda na kuanza muhula wa tatu wa urais.

Kuanzia hapo ghasia za kisiasa ziliongezeka. Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti za misuguano ya kikabila, makaburi ya halaiki ya watu waliouawa na ukiukwaji mkubwa wa haki ulikuwa ukifanywa na vyombvo vya dola.

Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afrika (African Union Commission on Human and Peoples Rights) ilipendekeza kuundwa kwa tume maalum ya kuchunguza uhalifu wa kivita. Raia zaidi ya nusu milioni walikimbilia na kuomba hifadhi nchi za jirani.

Oktoba mwaka huu Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) iliagiza kufanyika uchunguzi rasmi kuhusu jinai iliyodaiwa kufanywa na utawala wa Burundi na wawakilishi wake dhidi ya raia.

Ilikuwa ni kutokana na hali hii ndipo Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) ilipamua kuanzisha mazungumzo ya kutafuta amani miongoni mwa makundi yanayokinzana. Uganda na Tanzania zikachaguliwa kuongoza mazungumzo hayo chini ya uenyekiti wa Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa.

Wakati ghasia zikiendelea nchini Burundi, mazungumzo ya amani chini ya usimamizi wa kikanda umeshindikana na sababu zinaeleweka.

Wakati wa vita ya wenyewe ya wenyewe ya awali nchini Burundi (1993-95), Makubaliano ya Arusha (Arusha Accords) yaliyomaliza vita hiyo yaliungwa mkono na watu wengi na ndiyo maana yalifanikiwa.

Makubaliano hayo ya amani yalisaidia kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 13 na kusababisha vifo vya watu 300,000.

Lakini haya mazungumzo ya sasa yamekuwa yakikabiliwa na changamoto kadha kuanzia ‘upendeleo’ unaoonyeshwa na wasuluhishi hadi katika kubaini chanzo cha mgogoro.

Mazungumzo ya sasa hivi yamekuwa na lengo finyu kwani yamekubali kwamba uchaguzi wa 2015 ulikuwa halali. Aidha Desemba 2016 Mkapa aliwatuhumu wale waliokuwa wakihoji uhalali wa utawala wa Rais Nkurunziza kwamba walikuwa “wanapoteza muda tu.”

Badala yake mazungumzo yamekuwa yakiangalia tu hali ya mzozo wa sasa hivi na kutokana na maneno ya Mkapa mwenyewe “ili kuweka hali nzuri ya kuwezesha kufanya uchaguzi mwaka 2020.”

Msimamo huu umeonekana kuwatenga wapinzani wengi ambao wamekuwa wanawaona wasuluhishi kuwa na upendeleo. Na mtazamo wao huo umetiwa nguvu na hatua ya Tanzania na Uganda kupinga uamuzi wa ICC kuanza uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi.

Wakati hayo yakijiri Rais Pierre Nkurunziza amezindua kampeni ya kufanyika kwa kura ya maamuzi ambayo inatazamwa na jaribio la kutaka kusalia madarakani hadi 2034.

Mpango huo unahusisha kuidhinishwa kwa rasimu ya katiba ambayo itamuwezesha kuwania urais kwa mihula miwili zaidi ya miaka saba kila muhula. Muhula wa sasa wa Bw Nkurunziza unamalizika 2020.

Rais huyo aliwaambia wafuasi wake wiki iliyopita katika kijiji cha Gitega kwamba wale wanaopinga juhudi zake “kwa maneno au kwa vitendo” watakuwa wameuvuka “mstari mwekundu”.

Kampeni hiyo imeanzishwa baada ya serikali kuzindua juhudi za kuchangisha fedha za maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Shirika la habari la AFP linasema mchango huo, ambao serikali inasema ni wa hiari, umeshutumiwa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu ambayo yamesema ni kama “wizi kwa mpango”.