Home Habari 2018/19 mwaka wa neema sekta ya Afya

2018/19 mwaka wa neema sekta ya Afya

1413
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU

Sekta ya Afya nchini yapata mafanikio makubwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/19. Nieleze kwa kifupi mambo machache ambayo ni pamoja na;-

1. Idadi ya Watu wenye Virusi vya UKIMWI (WAVIU) ambao wamepima na kutambua hali zao imeongezeka kutoka watu 1,038,603 mwaka 2017/18 hadi kufikia watu 1,126,366 mwezi Machi 2019. 

– idadi ya WAVIU wanaotumia dawa imeongezeka kufikia 1,103,026 ambayo na sawa na asilimia 98 ya WAVIU waliopima na kutambua hali zao.
– WAVIU wanaotumia ARVs na ambao wana kiwango cha chini cha VVU (yaani Virusi vimefubazwa) ni asilimia 84 kutoka asilimia 88 mwaka 2017. 

2. tumeweza kutoa huduma za chanjo kwa watoto chini ya umri wa mwaka mmoja ili kuwakinga na magonjwa kwa kiwango cha asilimia 98. Katika kila watoto 100, watoto 98 nchini wanapata chanjo. Hakuna Mkoa au Halmashauri yoyote iliyoripoti kuishiwa chanjo za watoto au vifaa vya kutolea chanjo. 

3. Idadi ya kaya zenye vyoo bora imeongezeka kutoka asilimia 45.7 hadi asilimia 55.4. Na Kaya ambazo hazina vyoo kabisa zimepungua kutoka asilimia 5.8 hadi kufikia asilimia 2.7.

4. Huduma za Mama na mtoto zimeendelea kuboreshwa ikiwemo ujenzi wa Miundombinu (vituo vya Afya 352) pamoja na kuimarisha upatikanaji wa dawa muhimu na vifaatiba ili kuviwezesha kutoa huduma bora za uzazi na mtoto ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni. Tumeokoa maisha ya kina mama na watoto wao. Matokeo chanya yanaonekana. Mfano: wanawake wajawazito wanaohutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango wameongezeka kutoka asilimia 35 hadi asilimia 39.
– wanawake wajawazito wanaohudhuria klinic angalau mara 4 wakati wa ujauzito wameongezeka kutoka asilimia 51 hadi asilimia 69.4.
– idadi ya wanawake wajawazito wanaojifungulia ktk vituo vya kutoa huduma imeongezeka kutoka asilimia 68.5 hadi asilimia 79.2.

5. Katika kipindi hiki watu 29 walipata huduma za kupandikiza figo (Renal transplant) nchini na hivyo jumla ya watu 38 wamenufaika toka huduma hizi zianzishwe Hospitali ya Taifa Muhimbili mwaka 2017/18. tumeokoa maisha lkn pia fedha nyingi.

6. Ktk Mwaka 2018/19, watoto 11 wamepata huduma za kupandikiza vifaa vya kusaidia usikivu kwa watoto (cochlea implants) kwa watoto na hivyo kufanya jumla ya watoto 21 kupata huduma hii toka ilipoanzishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili mwaka 2017 .