Home KIMATAIFA EU YAIBANA HUNGARY KWA KUWAKATAA WAHAMIAJI

EU YAIBANA HUNGARY KWA KUWAKATAA WAHAMIAJI

4615
0
SHARE

 NA HILAL K SUED NA MITANDAO


Serikali ya Hungary imesema imedhamiria kuchukua hatua kukabiliana na hukumu ya Bunge la Ulaya dhidi ya yake kwa kukiuka misingi ya demokrasia.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Viktor Orban wiki iliyopita alisema alikuwa anatarajia vita kubwa ya mjadala kuhusu uamuzi huo.

Wabunge wa Bunge la Ulaya kwa kauli walitoa uamuzi wa kuanzisha mchakato ambao utatoa hatua za kuchukua kuiadhibu serikali ya Hungary kwa kukiuka kanuni za kidemokrasia.

Kura hiyo ilipita kwa kura 448, na kura 197 zilipinga, huku wajumbe 48 hawakupiga kura, hivyo kufanya mara ya kwanza kwa Bunge la Ulaya kutumia Kipengele Namba 7 cha Mkataba wa Umoja wa Ulaya kuanzisha mchakato dhidi ya nchi nyingine mwanachama wa EU.

Kipengele hicho cha Mkataba ulioanzisha EU mwaka 1992 kinalenga kulinda maadili ya umoja huo kama iliyoainishwa chini ya Kipengele Namba 2.

Uamuzi huu wa Bunge la Ulaya ambao haujapata kuotokea unaweza kuifanya Hungary kupokonywa haki yake ya upigaji kura. Suala hili sasa litapelekwa kwenye chombo kingine cha EU – Baraza la Mawaziri.

Katika taarifa yake Waziri Mkuu Orban alimtguhumu Kansela (Waziri Mkuu) wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye Alhamisi iliyopita aliziomba nchi za EU kuhakikisha Frontex – wakala wan chi za Umoja wa ulaya wenye jukumu la kulinda mipaka ya nchi za umoja huoa katika kudhibiti uhamiaji haramu – unakuwa na mamlaka ya kutosha kusaidia kupiga marufuku uhamiaji haramu kufuatana na mipango na sera za EU.

Orban alisema inavyoonekana, mpango huo hauwezi kuilazimisha nchi yake Hungary kulazimishwa kuruhusu wahamiaji, hivyo ipokonywe haki yake kulinda mipaka yake.

 

Alilalamika kwa kusema kwamba EU inataka kutuma mamluki kuja kwetu kutoka Brussels na kutwaa kutoka kwa watu wetu madaraka ya ya kulinda mipaka. Alisema kwamba hata hao wataruhusu wahamiaji kuingia.

 

Waziri wa mambo ya Nchi za Nje wa Hungary Peter Szijjarto ameituhumu uamuzi huo wa Bunge la Ulaya kwa kusema ni ulipizaji kisasi wa wanasiasa wanaounga mkono sera ya uhamiaji katika Ulaya.

Amesema uamuzi huu wa kuishambulia Hungary na watu wa Hungary umefanyika kwa sababu watu wa Hungary wameonyesha kwamba uhamiaji siyo mchakato wa lazima na kwamba unaweza kusimamishwa.

Tangu aingie madarakani mwaka 2010 Orban amekuwa akitoa msukumo miubwa kwa mahakama, vyombo vya habari na mashirika yasiyoya kiserikali, pamoja na kukataa kupokea wakimbizi wanaoingia nchini humo kutoka nchi nyingine za Ulaya.

Mwezi Juni mwaka huu Bunge la Hungary lilipita sheria iliyoweka hukumu ya vifungo kwa mtu yoyote yule atakayeonekana kuwasaidia wakimbizi wasiokuwa na hati.

Shgeria hiyo ilipingwa vikali na makundi mbali mbali ya haki za binadamu pamoja na nchi nyingi za Uklaya magharibi na ndiyo chanzo cha hatua ya Bunge la Ulaya kupiga kura kuikosoa Hungary.