Home Makala Aliogopwa kisha akaigopa CCM

Aliogopwa kisha akaigopa CCM

1586
0
SHARE

NA  VICTOR MAKINDA

Mjadala kuhusu Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani kada aliyelelewa na kukulia ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadae kuamua kukihama chama hicho kwenda Chadema na kuwania urais, kisha kurudi tena CCM,  ni mjadala mpakana.

Kwangu kufukuzwa ubunge Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, hakuwezi kunifanya kuacha kujadili juu ya Lowassa na kuhamia mjadala wa Nasari kupoteza ubunge kusudi.

Watanzania ndivyo tulivyo. Kila siku linapozuka jambo jambo hulirukia jambo hilo na kulifanya kuwa mjadala mpana hata kama mjadala uliotangulia ungali wa moto na una tija kuujadili.  Ukweli Ulivyo kujadili kuhusu kitendo cha Lowassa kuhama CCM na kuhamia Chadema na kisha kuhama Chadema kurudi CCM ni mjadala muhimu kwa ujenzi wa demokrasia ya vyama vingi.

Upana na ukubwa wa mjadala huu ni kutokana na umaarufu wa Lowassa na namna alivyojaaliwa uwezo mkubwa wa ushawishi na kuzichanga vyema karata za siasa. Nachelea kumtambua Lowassa kuwa ni gwiji wa siasa Tanzania. Ndio,ni gwiji na mjuzi wa namna sahihi ya kuifanya siasa. Ni  mwenye ushawishi kwa makundi yote, kuanzia vijana, wazee na akina mama. Ameonesha uwezo mkubwa wa ushawishi  ndani ya chama CCM na katika vyama vyapinzani.

Hatua ya  Lowassa kuhama CCM kwenda upinzani na kisha kurudi tena CCM na kupokelewa kwa kishindao na heshima kubwa, imewaacha baadh midomo wazi kwa mshangao. Wapo walioitarajia lakini wengi imeakuja ghafla  na kuwaachia mshangoa kwa kuwa hawakujua kama kuna siku Lowassa ama atahama CCM kwenda upinzania au atahama upinzania kurudi CCM. Hii ni kutokana na vile wana CCM walivyomtaja Lowassa na kumuhusisha na kashfa mbali mbali  na vile wapinzania walivyoungana na wana CCM kumhusisha na kashfa zinazofanana.Ukweli Ulivyo kuna kipindi taswira ya Lowassa ilichafuliwa pande zote. Ndani ya CCMna kwa vyama pinzani.

Lowassa kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015

Alikuwa ni mwanachama mtiifu ndani ya Chama licha ya kupata misuko suko mingi ukitanguliwa na ule wa kashfa ya kufua umeme wa dharura maarufu kama Richmond mwaka 2008. Taswira ya Lowassa kisiasa ilianza kuchafuliwa wakati ule kwa kashfa ya Richmond hali iliyopelekea wabunge wa CCM na upinzani kuungana kwa pamoja kumtupia mawe mpaka pale alipoamua kujiuzuru nafasi ya uwaziri mkuu.

 Wakati alipojiuzuru, Lowassa akilihutubia bunge alisema wazi wazi kuwa tatizo ni uwaziri mkuu wake na sio vinginevyo. Alimaanisha kuwa yeye hakuwa muhusika wa kashfa hiyo ya Richmond bali kashfa hiyo ilitengenezewa mazingira mahususi kuonekana kuwa yeye kama waziri mkuu hakuwajibika ipasavyo kwa lengo la kutaka kumuharibia na kumng’oa katika nafasi yake.

Swali ni kwa nini aliundiwa kashfa kumng’oa uwaziri mkuu hakufafanua lakini sasa linaweza kupatiwa majibu. Majibu ni kwamba alionesha kasi na uwezo mkubwa wa kiutendeaji, kasi iliyowatisha wana CCM wenzake hasa mahasimu wake kisiasa wakihofu kuwa itamuwia raisi kutwaa madaraka makubwa zaidi kwani utendaji wake ulionesha kukonga mioyo ya wengi. Akiwa waziri Mkuu Lowassa alitenda kwa kasi  na uafanisi uliotishia kesho ya wana mtandao kinzani ndani ya chama na serikali.

Baadhi tulidhani kuwa baada ya msukosuko ule Lowassa angelihama CCM na kuhamia upinzani kwani wana CCM wenzake aliowaamini walimsurubisha msalabani bila huruma na kufanikiwa kumng’oa kitini. Lowassa hakuhama CCM, aliendelea kubaki akiwa mwanachama mtiifu na mkimya huku baadhi ya wana CCM wakiendelea kumtupia mawe wakiwa wameungana na wapinzani. Ukweli Ulivyo nguvu za wapinzani kumchafua Lowassa zilikuwa zinajengwa na wana CCM wenyewe. Sababu walikuwa wanamwogopa kuwa angekuwa tishio kwa kesho yao kisiasa.

Pamoja na misuko suko hiyo ndani ya chama chake, Lowassa aliendelea kujijengea umaarufu na ngome kubwa zaidi ndani ya CCM kwa minajiri ya kuja kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015. Sote tu mashahidi kuwa kama CCM isingelibadili namna ya kumpata mgombea urais, Lowassa ndiye ambaye angelikuwa mgombea wa chama hicho kwani alipata uungwaji mkono mkubwa kwa wanachama wa chama hicho.

Tutakumbuka Lowassa wakati anapita kutafuta wadhamini katika mikoa mbali mbali nchini, maelfu ya wanachama wa chama hicho walijitokeza kumdhamini. Tunakumbuka pia wajumbe wa NEC ya CCM walivyokuwa wakiimba kuwa wana imani na Lowassa wakati wa kupitisha jina la mgombea urais kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma. Zaidi ya nusu ya wajumbe wa chama hicho waliungana kwa pamoja kuimba kuwa wana imani na Lowassa.CCM iliendelea kumwogopa Lowassa.

Hatimae Lowassa akatemwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM na kuhamania Chadema-Ukawa ambako alipita moja kwa moja kuwa mgombea urais wa Chama hicho ambacho kilikuwa moja ya vyama vilivyounda UKAWA.

 Ninakumbuka kauli ya mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe baada ya Lowassa kujiunga na chama hicho kuwa, wapinzani walikuwa wakisubiri kwa hamu CCM imkate Lowassa kuwania urais ili iwawie wepesi wao kutwaa nafasi hiyo. Mbowe alisema wazi kuwa alikuwa anaiogopa mno nguvu ya Lowassa ndani na nje ya CCM hivyo endapo kama Lowassa angeliwania nafasi hiyo kupitia CCM ni wazi kuwa wapinzani wangelikuwa na kazi nzito.

 Lowassa alipokuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema Ukawa, kila mmoja wetu atakuwa ni shahidi namna CCM ilivyoweweseka na kukumbwa na kihoro kwa hofu kuwa huenda Lowassa akashinda nafasi hiyo. Hii ilitokana na kuwa Lowassa hakuondoka peke yake CCM. Aliondoka na makada nguli na muhimu kabisa wa chama hicho ambao kwa pamoja alijiunga nao upinzani. Lakini pia ndani ya CCM aliwaacha wanachama na makada muhimu walio endelea kuwa na imani naye na kuumunga mkono.

 Ushawishi wa Lowassa ndani ya CCM na ndani ya upinzani uliwapa shida sana wana CCM. Wengi walijawa na hofu, woga na kihoro juu ya namna matokeo ya uchaguzi mkuu 2015 yatakuwa. Bahati iliyo njema CCM ilisimamisha mgombea ambaye hakuwa na kashfa yoyote na hakuwa mwana mtandao. Hii iliwawia ugumu wapinzania kumsema vibaya Dkt John Pombe Magufuli mgombea wa CCM kwa lolote baya. Hoja ikawa tu CCM ni chama kibaya na hoja nyingine nyepesi. Wapinzani walishindwa kumgusa moja kwa moja mgombea wa chama hicho kwa kashfa ya moja kwa moja. Uchaguzi ukapita na CCM ikashinda kiti cha rais na viti vingi vya wabunge na madiwani.

Pamoja na ushindi huo, Ukweli Ulivyo, CCM iliteseka sana katika uchaguzi mkuu 2015 tangu historia ya vyama vya upinzania nchini. Nguvu ya Lowassa haikuwa ya kitoto. Kura zaidi ya milioni 6 alizozivuna Lowassa haikuwa  kazi ndogo. Ushindi wa CCM ukahama toka ushindi wa kishindo mpaka ushindi mwembamba. Tafsiri yake nini nini? Tafsiri ni kwamba Lowassa aliendelea kukubalika ndani ya CCM hata baada ya kuhama na alikubalika upinzani. Wengi walikuwana imani naye. Laiti kama Lowassa angeendelea kubaki upinzania angeisumbua tena na tena CCM. CCM ilikuwa inamwogopa  na kuziogopa mno nguvu za Lowassa wakati akiwa CCM na alipokuwa upinzani.

 LOWASSA KURUDI CCM

Mioyo ya wapinzania ipo juu juu. Presha zina wapanda na kushuka. Hawajui waseme nini tena kwa mwanasiasa huyu nguli. Hawawezi tena kumwita fisadi.Hawawezi tena kumwita dhaifu. Wapinzani walio wengi wanakiri kuwa Lowassa amewasaidia kupata  vingiviti vya bunge, madiwani  na kura za urais. Amewaongezea ruzuku inayotokana na kura za urais na viti bungeni. Wanahofu kesho yao na nini Lowassa atafanya dhidi yao. Wanamwogopa na kuihofu nguvu yake kisiasa kwani tunaona hata sasa anaondoka na wengi kurudi nao CCM.

CCM wamefurahisana Lowassa kurudi chamani, japo wapo wachache ambao wamenuna huku wakihofu nguvu ya mwanasiasa huyu kwa mustakabari wao wa kisiasa. Wapo wana CCM walioanza kujijengea mitandao. Kurudi kwa Lowassa kumewavuruga kabiasa.

 Ukweli Ulivyo wengi wa wana CCM sasa wanapata usingizi. Walikuwa hawalai wakuiihofu nguvu ya Lowassa. Kurudi kwake chamani kumewapa ahueni kubwa .CCM  sasa wanaiona njia nyeupe ya kutwaa majimbo mengi zaidi na kushinda kiti cha urais kwa kura za kishindo.

Ukweli Ulivyo Lowassa naye ana amani tele kurudi CCM. Kuhama kwake ilikuwa ni hasira tu za muda mfupi. Sasa hasira zimemwisha na amerudi nyumbani. Sote tunafahamu jinsi mtu aliyekaa mbali na nyumbani kwa muda mrefu anavyofurahi pindi anaporudi nyumbani. Lowassa ana amani tele kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote kwani amefanikiwa si tu kurudi nyumbani kwake bali kuwaziba midomo ugenini na nyumbani. Lakini hilo halipingani na ukweli kuwa Lowassa alipokuwa upinzania alikuwa anaiogopa sana CCM huku CCM nayo ikimuogopa yeye.Kwa nini Lowassa alikuwa anaigopa CCM… Tukutane Alhamisi ijayo ijayo