Home Habari Baba amkaribisha nyumbani muuaji wa mwanae

Baba amkaribisha nyumbani muuaji wa mwanae

1680
0
SHARE

Eddy Hekman na mkewe waliishi katika kijiji kimoja nchini Uholanzi karibu na bahari ya kaskazini.

Wakiwa katika eneo hilo waliishi maisha ya ukimya ambayo ni kama yale ya wanandoa walistaafu isipokuwa: Mara moja kwa mwezi wanakutana na mtu ambaye alimuua mwanao wa kike.

Na sio hilo pekee, wao huzungumza naye kupitia simu kila Jumapili.

Na Hekman aliandika kitabu pamoja naye.

Hekma aliambia BBC kwamba yeye na mkewe walimchukulia muuaji wa mwana wao kama mmoja wao katika familia yao.

Je hili linawezekanaje?

Hekman alitoa hadithi yake kwa Neal Razell. Mwanawe wa kike alizaliwa 1982.

Alikuwa ni mtoto mwenye furaha chungu nzima , alicheka sana lakini pia alikuwa akiona haya, alipenda sana maswala asli , alipenda kutaka kujua mambo mapya na alisafiri sana, babake anakumbuka.

Renske alisomea baiolojia na kufanya kazi katika eneo takatifu nchini Uholanzi.

Alipendelea kuwaaangalia wengine, alisema babake. Yeye na wazazi wake walikuwa na uhusiano wa karibu.

Wakati wakisafiri walikuwa akiandamana naye hadi katika kituo cha treni ili kumuaga.

Mwaka 2008 mwezi Novemba , msichana huyo aliye na umri wa miaka 20 na, alisafiri kuelekea Switzerland, ambapo alifanya kazi kama muelekezi wa kuteleza barafuni.

Hekman anakumbuka kwamba ni wakati huo ambapo alikutana na Alasam Samarie , mtu ambaye baadaye alimuaa.

Alipanda katika gari na hapo akakutana na Samarie, walianza kuzungumza na kutusalimia wakati treni ilipoanza kuondoka, anakumbuka.

Hivyo ndivyo uhusiano huo ulivyoanza. Walikuja sana kututembelea wikendi , anasema Hekman.

Wote walienda nje pamoja wakitembea na mwao wao na kupenda soka sana.

Wanangu wawili walicheza , Renske na Samarie walipendana sana kwa hivyo tuliwapenda sana sisi kama familia.

WANANDOA

Licha ya kutoka dunia tofauti , Hekman na mkewe walihisi kana kwamba mwanao na mpenziwe walikuwa wapenzi wazuri sana.

Samarie alikuwa mkimbizi nchini Uholanzi .

Alikua mzaliwa wa Benini, Afrika magharibi. Aliwasili katika taifa hilo la Ulaya 2002 na baada ya kuishi katika vituo kadhaa vya wakimbizi alifanikiwa kupata eneo na kuanza maisha.

Kama kijana , Samarie alifanya kazi katika shamba la ndizi nchini Benin.

Yalikuwa maisha magumu na alitaka kuyasahau hivyobasi akaamua kupanda meli moja ya mizigo ambapo alijificha na kusafiri umbali wa kilomita 8000 hadi Uholanzi.

Samarie alikuwa mtu mwenye roho nzuri na mtulivu, anasema Hekman, ambaye anasema hakuonyesha ishara zozote za kupenda kupigana ama uchochezi hata walipocheza pamoja.

Renske aliendelea kuishi katika kijiji cha Baflo, karibu na eneo takatifu ambapo alikuwa akiishi.

Samarie alikuwa akimtembelea mara kwa mara.

Mnamo mwezi Aprili tarehe 213 2011, wakati wanandoa hao walipokuwa pamoja kwa miaka miwili, mamake Renske alisalia macho hadi usiku wa manane akitazama habari na kugundua kwamba kuna kitu kibaya kilichofanyika katika eneo la Baflo.

Yeye na mumewe hawakuchukua muda mrefu kabla ya kugundua kwamba kile kilichofanyika kilimuhusisha mwanawe.

Kulikuwa na habari katika mitandao kwamba mwanamke mchanga alikuwa ameuawa na mwanamume aliyekuwa na rasta kichwani, anakumbuka Hekman.

Baflo ni eneo dogo na lilikuwa na mtu mmoja ambaye alikuwa na rasta, hivyobasi nilijua lazima ni Samarie na kwamba msichana huyo angekuwa Renske, anasema.

Ilikuwa vigumu kuelezea ni nini kilichofanyika haswa.

Alitaka kusubiri hadi pale atakapothibitisha. Aliwapigia simu maafisa wa polisi saa kumi na moja alfajiri lakini hawakuweza kumwambia chochote.

Na ilipofikia mwendo wa saa tano ndiposa maafisa wawili wa polisi waliwasili nyumbani kwao , bila kujua ni nini haswa kilichotokea.

Walituambia kwamba Renske na Samarie walizozana na kwamba alimpiga kichwani na kifaa cha kuzima moto.

Samarie baadaye aliondoka nyumbani na kuanza kuelekea katika kituo cha treni .

Afisa wa polisi aliyekuwa amevalia nguo za raia alimfuata na katika hali isioeleweka Samarie alitoa bunduki yake na kuanza kumpiga risasi.

Maafisa wengine walimkabili na baada ya kumpiga risasi mara tano walimkamata.

Daktari aliokoa maisha yake. Na ndio hadithi yake ikaanzia hapa.

Kwa sababu hata baada ya kugundua kwamba mwana wao ameuawa , Eddy Hekman hakuwa na hasira.

Kile kilichokuwepo ndani ya hadithi ni kwamba siku moja kabla, mnamo mwezi Aprili 12, Ombi la Samarie la kutaka kusalia nchini Uholanzi kama mkimbizi lilikataliwa anasema.

Hekman hakuweza kuelewa ni nini kilichotokea.

”Sikuweza kufikiria kwamba ni mtu niliyekutana naye” , alisema kuhusu kifo cha mwanaye.

Hekman na familia yake ilijaribu kuendelea na maisha yao kwa uwezo wao.

”Tunajaribu kuendelea na maisha, anakumbuka. Kujaribu kuelewa kile kilichofanyika, wanadoa hao walimuandikia samarie miezi miwili baadaye mnamo mwezi Juni. Walimtumia barua katika jela iliokuwepo karibu na Hague ambapo kijana huyo anaendelea kuzuiliwa wakitaka kumuuliza ni nini kilichofanyika”.

MKUTANO WAO

Mkutano wao ulifanyika Septemba.

”Alijawa hisia, mtaalamu wetu alikuwepo pamoja na wakili wake sote tulikuwa tumeketi katika chumba kidogo na baadaye akaingia”, anasema.

Tulilia, anakumbuka.

Haki miliki ya picha Eddy HekmanTulizungumzia kile alichofikiria kilifanyika na kwa nini kilifanyika, kwetu sisi kilikuwa kitendawaili.

Hekman hakumbuki iwapo Samarie alitumia neno msamaha lakini bila shaka alikuwa ni kitu alichokuwa akihisi.

Kijana huyo aliwaambia kwamba yeye mwenyewe hakujua kile kilichofanyika.

Licha ya kila kitu, Hekman anasema kuwa hakuwa na hasira, hakuwa na hasira na Samarie.

lakini nilitaka kuelewa ni vipi mtu ambaye alionekana kuwa mzuri na aliyekuwa na mapenzi chungu nzima aliweza kubadilika na kuwa mnyama kwa ghafla.

Alitembelea chumba ambacho Samrie aliishi ili kuchukua vitu vyake.

Ilikuwa balaa, anakumbuka lakini licha ya yote hayo alipata dawa. Ni wakati huo ambapo ukweli ulibainika, anafichua.

DAWA ZA MSONGO

Samarie alikuwa akitumia dawa za kukabiliana na msongo wa mawazo kwa jina SSRI na wakati wa kifo cha Renske dawa zake zilikua zimeisha.

Hekman anaamini kwamba hali hiyo ilimuathiri.

”Mimi sio daktari lakini naelewa mengi kuihusu na naamini inawezekana”, anasema.

Fikra zake ni kwamba dawa pamoja na wasiwasi aliokuwa nao wa kutaka kusalia Uholanzi ulichangia pakubwa kwa yeye kuzua vurugu.

Idara ya mahakama ya Uholanzi ilimfunga Samarie miaka 28 jela. Lakini kutokana na hali yake kifungo hicho kilipunguzwa hadi miaka mitano na nusu.

”Tayari ametumikia kifungo chake na sasa yuko katika taasisi ya kisaikolojia ambapo haruhusiwi kuondoka”, anasema Hekman ambaye humtembelea kila mwezi pamoja na mkewe.

KITABU CHAO

Hekman aliandika kitabu pamoja naye ili kumpatia kitu kizuri atakachokumbuka wakati akiendelea kuzuiliwa.

Anasema kuwa kimemsaidia , ndivyo alivyokuwa akijituliza wakati wa hali mbaya.

Wakati wa mikutano hiyo na mazungumzo yao kila Jumapili walizungumzia vitu vya kawaida katika maisha yao na vipindi vya runinga.

”Mara ya kwanza tulikuwa tukizungumza kuhusu kile kilichotokea usiku huo lakini hayo yalikuwa yamepitwa na wakati” .

”Mara nyengine tulikuwa tukikumbuka vile walivyoishi , mara nyngine hisia zilirudi lakini zinaendelea kuisha kila muda unapopita”.

Hekman anaamini kwamba mwanawe angeunga mkono uhsiano walio nao na Samarie.

”Alikuwa hivyo, alikuwa mpenzi, yeye mwenye asingelielewa kila kitu kilichofanyika”.

Na licha ya kile kilichotokea, Hekman na mkewe bado walimpenda Samarie ijapokuwa wanajua ni kitu kisicho cha kawaida.

Baada ya muda unalazimika kufanya maamuzi.

Kwa kweli sio uamuzi ambao ungefanywa na wengi lakini tunaamini kwamba ndio uamuzi mzuri kwetu.

BBC SWAHILI