Home Kisima cha Babu Bulembo kielelezo cha wenye uchu wa kuvuruga amani

Bulembo kielelezo cha wenye uchu wa kuvuruga amani

1515
0
SHARE

YANGU moto wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uanze kuwashwa na vyama mbalimbali vya siasa nchini vilivyosimamisha wagombea wao katika nafasi za udiwani, ubunge na urais, tumeshuhudia mengi, ila kauli tata za viongozi wa Chama Cha Mapinduzi – CCM zimezidi kushika hatamu. Mbali na sera tamu za wagombea wa vyama viwili vinavyoshikana mashati katika kipindi hiki yaani CCM na Chama cha Demokrasia na Maendeleo – Chadema, kumekuwapo pia na rafu za hapa na pale ambazo katika mchezo wa kampeni za uchaguzi, nyingine hujitokeza kunogesha mchezo huo wa siasa lakini nyingine huwa ni hatari kwa ukomavu wa demokrasia nchini.

Mojawapo ya kauli ambayo imedhihirisha kuwa CCM ni chama kisichokubali kushindwa, ni ile iliyotolewa Septemba 17, mwaka huu mjini Kigoma na Mwenyekitiwa CCM wazazi Taifa, Abdallah Bulembo. Kada huyo mkongwe kwa kutumia nafasi aliyopewa kwenye jukwaa la kumnadi mgombea wake Dk. John Magufuli, alisema, “CCM imefanya mambo mengi, na yapo mengi ambayo haijayafanya, na ambalo kamwe haitofanya ni kuwapa Ukawa nchi,” mwisho wa kumnukuu. Katika kauli hiyo ambayo imezua tafsiri pana yenye dhana ya kushinda kwa namna yoyote ile kutokana na maandalizi ambayo chama hicho imeyaandaa, ni dhahiri kuwa hii ni kauli ambayo imeenda mbali zaidi ya ile ya goli la mkono ambayo ilitolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi – CCM, Nape Nnauye. Kauli tata kama hizizimekuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali wa CCM hasa baada ya maji kuanza kuwafikia shingoni, yamkini hawakutegemea ushindani unaojitokeza sasa ndio maana wameamua kufunguka bila kupima athari za tafsiri ya maneno yao au bila kuweka akiba ya maneno wanayoyatamka pindi wanapopandishwa ‘mzuka’ na wanachama wanaowashangalia kwenye mikutano.

Kwa sababu hiyo tunaona katika kauli hiyo kuwa kamwe CCM haitokabidhi nchi kwa upinzani, inaashiria kwanza kabisa chama hicho kimejipanga kwa mbinu safi na chafu ambazo zaweza kuvuruga amani. Hii ina maanisha kuwa pamoja na mbinu safi kukubalika ili kufuata mkondo wa demokrasia nchini, bado mbinu chafu za chama hiki zinaashiria wazi kuwa kipo tayari kwa lolote kuliko kukubali kushindwa jambo ambalo katika nchi zinazoheshimu demokrasia na kutunza tunu ya amani, hakikubaliki.

Tumeona yaliyotokea katika nchi za wenzetu ambao walikataa kukabidhi nchi baada ya upinzani kushinda, kwa mfano mwaka 2007/08, Kenya ilitumbukia katika machafuko yaliyopoteza maisha ya Wakenya wasiokuwa na hatia. Pia upepo huo uliikumba Zimbabwe ambayo mpaka leo, kiongozi wake Robert Mugabe licha umri kumtupa mkono bado ameendeelea kung’ang’ania madaraka. Kwa mantiki hiyo, hapa sizungumzii suala la mtu binafsi ndani ya CCM kung’ang’ania madaraka bali ni mfumo mzima wa CCM kutokukubali matokeo iwapo wakishindwa katika Uchaguzi Mkuu Ambao utaamuliwa na sanduku la kura ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.

Ni jambo lisilovumilika kuendelea kusikia kauli za vitisho kama hizi zinatolewa na viongozi wakubwa wa CCM. Chama ambacho kimepewa heshima ya kipekee kwa kutunza amani iliyopo nchini. Sasa inashangaza kuona zimwi gani limekikumba chama hiki kwa sababu chama ni watu na watu wanaongozwa na viongozi ambao sasa wameamua kutumia ubabe usio kifani aidha, kwa kuwatisha wananchi au kwa kutoa matamko yanayoashiria kutokubaliana na matokeo mabaya kwao pindi uchaguzi utakapokamilika.

Hii ni hali ya hatari ambayo kamwe vyombo vya usalama havitakiwi kuvumilia, hii ikiwa ni pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa sababu pamoja na yaliyotokea bado NEC wamekuwa wakisema hivyo ni vionjo vya siasa. Hakika vionjo vya aina hii havitakiwi kuvumilika na iwapo kukitokea vurugu au uvunjifu wowote wa amani pindi uchaguzi utakapomalizika na kuangukia pua, viongozi wa aina hii wanatakiwa kuwa wa kwanza kuhojiwa kwani waliweka wazi kile watakachokifanya pindi