Home Makala Kimataifa BUNGE LA MAREKANI LACHUNGUZA UNUNUZI WA NDEGE ZA KIJESHI KENYA

BUNGE LA MAREKANI LACHUNGUZA UNUNUZI WA NDEGE ZA KIJESHI KENYA

1241
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU,

Wachambuzi wa mambo ya kijeshi wameibua maswali mazito kuhusu athari za baadaye za mikakati ya mifumo miwili ya zana za kijeshi ambazo Kenya imeruhusiwa kununua kutoka Marekani katika mapambano yake na kikundi cha wapiganaji wa AlShabab nchini Somali.

Serikali ya Kenya iko mbioni kutumia takriban Dola za Kimarekani 671 milioni kununulia ndege 12 za aina ya helikopta za mashambulizi (attack helicopters), pamoja na idadi hiyo hiyo ya ndege zingine za matumizi ya kilimo lakini zitarekebishwa na kuewekewa silaha.

“Ingawa Kenya imekiri kutokuwa na uwezo wa mashambulizi ya anga, hatujui athari za muda mfupi za zana hizi za kijeshi,” anasemea Dr Nan Tian, mtafiti wa masuala ya zana za kijeshi kutoka taasisi ya International Peace Research Institute (Sipri) yenye makao yake Stockholm, Sweden.

Suala hili tayari limeibua mjadala mkubwa katika ulingo wa siasa nchini Kenya wakati huu wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu Agosti 8, hasa kutokana na fedha nyingi serikali ya ya nchi hiyo imetenga.

Tayari Kamati ya Bunge ya Baraza la Wawakilishi la Marekani inachunguza madai ya Mbunge wao mmoja kuhusu Kenya kupunjwa katika dili hii.

Ununuzi wa aina zote hizo mbili za ndege zinajumuisha upelekwaji wa wataalamu kutoka makampuni ya Marekani yatakayozitengeneza ambao watawapa mafunzo wanajeshi wa Kenya namna ya kuzitumia na masuala mengine ya kiufundi.

Lakini bado haijajulikana iwapo marubani wa Kenya watapewa mafunzo ya kutosha kurusha helikopta aina ya MD 530F Cayuse Warrior na ndege aina ya Air Tractor AT-802L, anasema Dr Tian.

Mtaalamu huyo anasema ubora wa zana hizo katika hali ya mapambano ya Somalia bado haujawekwa sawa.

“Helikopta hizo na ndege za kunyunyuzia madawa mashambani zilizorekebishwa kwa matumnizi ya jeshi zinaweza kushambuliwa kirahisi na mifumo ya kujihami ya AlShabab,” anasema Dr Stig Jarle Hansen, mtunzi wa kitabu kuhusu historian a itikadi ya kikundi hicho cha wapiganaji.

Katika mahojiano na gazeti la Sunday Nation la Kenya Stig alisema ndege hizi hazina kasi ya kuruka na zimewekewa silaha ndogo ndogo tu na kwamba zinaweza hata kudunguliwa na bunduku za kawaida.

Inadaiwa AlShabab wanamiliki mizinga ya kudungulia ndege, na mizinga mingine aina ya “man-portable air defence systems (Manpads)” inayobewbwa na mtu mmoja mmoja na ambayo ina uwezo wa kuzidungua hata zile ndege zinazoruka juu zaidi.

Wanamgambo wa Somalia wamewahi kutumia maroketi (rocket-propelled grenades – RPGs) kuzitungua ndege mbili aina ya helikopta za marekani mjini Mogadishu mwaka 1993. Na mwaka 2002, wapiganaji wa AlShabab walifyatulia ndege ya abiria ya Israel roketi mbili aina ya Manpad katika uwanja wa ndege wa Moi, mjini Mombasa. Hata hivyo ndege hiyo ilinusurika.

Hata hivyo inasadikiwa manunuzi ya sasa ya ndege ambazo Marekani imeiruhusu Kenya kununua kutoka kampuni za L3 Technologies ya New York na MD Helicopters ya Arizona hayawezi kukamilika na ndege kuanza kutumika katika muda mfupi ujao.

Mkuu wa kampuni shindani huko huko Marekani iliyoko jimbo la North Carolina ameshauri kwamba inaweza kuchukua miaka miwili kwa kampuni hiyo ya New York kumaliza kutengeneza na kuzituma hizo ndege.

Dili hii, iliyotangazwa mwezi Januari bado haijakamilika, huku Mbunge mmoja wa Bunge La Congress la nchi hiyo akidai kwamba Kenya inalazimika kulipa hela nyingi bila halali kwa zana za kijeshi ambazo hazijajaribiwa katika mapambano. Kamati moja ya Bunge hilo linachunguza tuhuma hizo.

Mtaalamu mwingine wa mambo ya ulinzi na usalama katika Pembe ya Afrika, Abdullah Boru anasema kuzidisha kwa nguvu za uwezo wa kijeshi pekee hakuwezi kuwamaliza AlShabab. Anasema njia pekee ni kuliongezea uwezo jeshi la Somalia.