Home Makala Kimataifa CARL GUGASIAN: MHALIFU WA BENKI MWENYE AKILI KULIKO WOTE-2

CARL GUGASIAN: MHALIFU WA BENKI MWENYE AKILI KULIKO WOTE-2

1053
0
SHARE

WIKI iliyopita tulidadavua namna mwaka 2021 ulimwengu utakavyoshuhudia Mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani, baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi Serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka 115 mpaka miaka hiyo 17.

Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69, jina lake anaitwa Carl Gugasian au maarufu kama ‘The Friday Night bank robber’! Mhalifu aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki pasipo kukamatwa, kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashtaka wa Marekani ‘kumsifu’ kuwa ndiye mhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa zaidi katika historia ya Marekani (the most prolific bank robber).

Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa ‘mashabiki’ wakiitaka Hollywood watengeneze ‘movie’ kuhusu maisha ya ‘The Friday Night Bank Robber’! endelea..

UTEKELEZAJI WA TUKIO

Matukio yote ambayo Carl aliyafanya, alikuwa anayetekeleza Oktoba au Novemba, ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama mapema!
Pia matukio yake yote aliyatekeleza Ijumaa na hii ndiyo iliyomfanya apewe jina la ‘The Friday Night Bank Robber’.
Uchaguzi wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa faida kadhaa.. Kwanza kipindi cha baridi na vuli, jua linazama mapema kwa maana ya kwamba katika saa zile zile ambayo benki zinakuwa zinafungwa, lakini katika kipindi hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo inampa mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio Ijumaa ilimaanisha kuwa ndio siku nzuri kwa benki kuwa na kiwango kikubwa cha fedha. Lakini pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa Ijumaa wafanyakazi wanakuwa mshawasha kutokana na wikendi kuanza hivyo umakini hupungua.

Kwahiyo alichokifanya Carl kwanza ni kupaka ‘harufu’ kwenye nyumba zote zilizo karibu na benki ili kuwachanganya mbwa wa polisi wakija kujaribu kutafuta trail ya alikoelekea!

Siku ambayo Carl alikuwa anafanya tukio alivaa kinyago cha kutisha usoni ambacho kilifiti sawa sawa kabisa ili kuficha ngozi yake na! Pia alivaa nguo nyingi ili kuleta mwonekano kwamba ni mnene. Na alikuwa akiingia ndani ya benki, alitembea dizaini kama amechuchumaa mfano wa Kaa (crab)! Vitu vyote hivi alivyovifanya watu walihisi labda alikuwa na matatizo ya akili lakini hawakujua kuwa alivifanya kwa kusudi kabisa. Alivaa kinyago cha kutisha ili kuleta madhara ya kuogofya na kuficha tone ya ngozi yake, pia alivaa nguo nyingi ili kuficha umbo la mwili wake na alitembea kama kaa akiwa kama amechuchumaa ili kuficha urefu wake! Hii ilimsaidia sana kwani kwa miaka 30 FBI walishindwa kung’amua mtu wanayemtafuta alikuwa wa saizi gani, urefu gani au rangi gani ya ngozi?

Carl alikuwa anasubiri dakika 5 kabla benki haijafungwa ndipo alikuwa anavamia! Hii ilimpa uwezekano mzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanyakazi pekee au wateja wachache sana wamebakia. Akishavamia benki alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na wasimwangalie! Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda kutokana na mazoezi ya karate), Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye droo za ‘ma-teller’ na kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi ule ule aliruka tena mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa msisitizo wasimwangalie na kabla hawajang’amua kinachoendelea, Carl alikuwa tayari ashatoka nje ya benki na kutokomea katika msitu ulio karibu.

Inaelezwa kuwa katika matukio yake yote, aliyatekeleza ndani ya muda usiozidi dakika mbili! Yani chini ya dakika mbili alikuwa tayari amevamia, amekomba hela na ameshatokomea msituni.

Carl anaeleza mwenyewe kuwa akiingia ndani ya msitu, alikuwa anakimbia kwa dakika kadhaa kama 10 hivi mpaka mahali ambapo anakuwa ameficha baiskeli kisha anaendesha mpaka ndani kabisa ya msitu kulipo na handaki lake, akifika kwenye handaki kila kitu anakiacha hapo; fedha alizoiba, masks, nguo, gloves kisha anavaa nguo nyingine za kawaida anaendesha baiskeli anaondoka! Carl anasema kuwa ataendesha baiskeli kwa muda wa kama dakika 20 au zaidi mpaka upande wa pili wa msitu ambapo kuna barabara na hapo kunakuwa kuna gari amepaki linamsubiri ndipo anaweka baiskeli ndani ya gari anaendesha kama raia wa kawaida na kuelekea nyumbani.

Carl anasema alikuwa anaacha wiki au miezi ipite mpaka stori kuhusu tukio la ujambazi zianze kufifia ndipo anarudi kwenye ule msitu na kuchukua ‘hela zake’. Baada ya hapo maisha yanaendelea na anaanza ‘tafiti’ kwa ajili ya tukio linalofuata.

#4

KUKAMATWA NA MAZINGAOMBWE YA HUKUMU

Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno!
Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa. Baada ya kuifungua ndani walikuta bastola na vitu vingine kadhaa vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao wakashauri vipelekwe Polisi! Baada ya vitu hivyo kupelekwa polisi, vikachunguzwa na kukakutwa ramani. Polisi walipoifuatilia ile ramani ikawapeleka moja kwa moja kwenye handaki dogo ndani ya msitu! Kutokana na vitu vilivyokutwa ndani ya handaki hilo, polisi wakapata wasiwasi kuwa inawezekana ‘wanadeal na ishu serious’ kuliko uwezo wao, hivyo wakawataarifu FBI! Baada ya FBI kuwasili iliwachukua saa kadhaa tu kung’amua kuwa vitu hivyo vinahusiana moja kwa moja na jambazi wanayemtafuta kwa miaka 30, The Friday night bank robber.

FBI walitumia alama za vidole walizozikuta kwenye ile handaki na pia walitumia kijarida kidogo kinachohusu kituo cha mafunzo ya karate kumtafuta Carl mpaka wakampata.
Siku Carl anakamatwa alikutwa ‘ofisini kwake’ Maktaba ya Philadelphia Free Library akiwa anafanya ‘tafiti’

Baada ya kukamatwa na kesi kufikishwa mahakamani, ilikuwa ni dhahiri kuwa Carl atahukumiwa kifungo cha maisha au aghalabu miaka 115 pasipo uwezekano wa kupata parole kutokana na mashtaka yanayomkabili, lakini mwisho wa siku Carl alikubaliana ‘dili’ na FBI kuwa awaeleze nukta kwa nukta kuhusu matukio yote 50 aliyoyafanya, pia akubali kushirikiana na FBI kutengeneza programu maalumu kuwasaidia maofisa wa FBI kutambua namna ya kuwabaini ‘serial criminals’ na pia awaelekeze kuhusu saikolojia ya ku-plan matukio ya uhalifu yaliyo dhahiri!
Carl akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu yake kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole.

Hivyo basi ikifika 2021, Carl Gugasian anarudi uraiani! Inaelezwa kuwa huko gerezani Carl ni mtu mnyoofu mno na ni mfungwa wa kuigwa na ameendeleza desturi yake ya kupenda mazoezi, hivyo yuko katika afya njema sana na wengi wanaamini atafika 2021 akiwa salama salmini na anaamini kabisa Hollywood wanaomba usiku na mchana atoke salama ili wamfanye celebrity na watupe bonge la muvi!