Home Latest News CHAGUZI HAZIENDANI NA VIPINDI VYA URAIS BOTSWANA

CHAGUZI HAZIENDANI NA VIPINDI VYA URAIS BOTSWANA

5675
0
SHARE
NA HILAL K SUED    |   

Machi 31 mwaka huu, aliyekuwa Rais wa Botswana, Ian Khama aliachia madaraka na siku iliyofuata Mokgweetsi Masisi aliapishwa.

Katika eneo la Bara la Afrika ambako kumeshuhudiwa marais wa nchi mbili waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi – Robert Mugabe (miaka 37) na José Eduardo dos Santos (miaka 38) kuondoka madarakani, uamuzi wa Ian Khama kuheshimu ukomo wa vipindi na kuondoka baada ya miaka kumi madarakani ulipongezwa na wengi.

Chama tawala cha nchi hiyo cha Botswana Democratic Party (BDP) ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1966 kinakabiliwa na uchaguzi katika muda wa miezi 18 ijayo, hivyo kwa nini Khama ajiuzulu muda wote huo kabla ya uchaguzi?

Kwa kawaida, barani Afrika marais walio madarakani ndiyo hushinda wanapoamua kugombea. Rais aliye madarakani anapokabiliwa na mgombea kutoka upinzani, upinzani huzoa asilimia 12 ya kura. Lakini iwapo mgombea wa urais wa upande wa upinzani anapambana na mgombea ambaye siyo rais aliye madarakani, upinzani huzidisha kura zake mara nne hadi kufikia asilima 48.

Marais walio madarakani hushinda mara kwa mara kutokana na ile hali ya ‘kuwa madarakani’ kwani marais wana uwezo wa kupzipindisha taasisi za umma kumpendelea, mara nyingi hupewa muda mwingi katika vyombo vya habari vya umma, hutumia nyadhifa zao na hata fedha ya umma ili kujihakikishia uaminifu (loyalty).

Na mara nyingi rais aliye madarakani hutumia mali na nyenzo za umma kufanyia kampeni na hivyo kupora uwanja mkubwa wa demokrasia. Hivyo Ian Khama kumuachia urais Masisi mwaka mmoja na nusu kabla ya uchaguzi, unamuongezea rais huyo (Masisi) nafasi ya kuchaguliwa mwaka ujao (2019) na hivyo kukiongezea uhai chama tawala cha BDP

Vipindi vya uchaguzi nchini Botswana haviendani na ile mizunguko ya miaka mitano mitano – hali iliyoanza baada ya rais Ketumile Masire alipoanzisha, mwaka 1998, ukomo wa vipindi baada ya yeye kuwa madarakani kwa miaka 18.

Hali hii si kiashirio cha kukua kwa demokrasia, bali ni mfumo uliowekwa kimakusudi kuhakikisha ushindi wa siku zote wa chama tawala cha BDP ambacho kipo madarakani tangu 1966.

Historia inamuweka Masire katika mwanga mzuri, lakini lengo lake la kupishana kwa vipindi vya urais na vile vya Bunge lilikuwa ni hilo tu.

Mwaka 1997 alipobadilisha Katiba, ilikuwa ni kutokana na kupungua kwa umaarufu wa chama chake kilichokuwa kinakumbwa na kashfa nzito nzito za ufisadi, na hasa hasa ilifanyika kuepukana na uwezekano wa kushindwa uchaguzi wa mwaka 1999.

Kabla ya kujiuzulu kwa Ian Khama mwezi uliopita, hali ya siasa nchini humo ilianza kuchukua sura ya ilivyokuwa katika miaka ya mwishoni ya utawala wa Masire katika miaka ya 90. Utawala wa Khama umekuwa ukishutumiwa kuwa wa kibabe, uliozama katika ufisadi, na uminyaji wa haki za raia.

Wachunguzi wa mambo nchini humo wanasema baada ya miaka 52 kuwa madarakani, Wabotswana wengi wameanza kukichoka chama hicho. Chama hicho kiliponea chupuchupu katika uchaguzi uliopita wa 2014 kilipopambana na upinzani uliounganika. Kilishindwa kupata zaidi ya nusu ya kura pale kilpopata asilimia 46.5 tu huku vyama vya upinzani kati yao vilipata jumla ya asilimia 53.5 ya kura zote.

Miezi 18 ijayo utampa Masisi fursa ya kukishikilia vyema chama na kushughulikia masuala ya ufisadi, ukosefu wa ajira, hali ambayo ilianza kuwa mbaya chini ya utawala wa Khama.

Botswana ni nchi huru iliyoko Kusini mwa Afrika . Jina rasmi ni Jamhuri ya Botswana.
Mji mkuu wa Botswana ni Gaborone .

JIOGRAFIA YA BOTSWANA
Botswana haina pwani kwenye bahari yoyote. Imepakana na Zambia,
Zimbabwe , Afrika Kusini na Namibia . Mpaka baina ya taifa la Botswana na Zambia ni mita 700 tu na ndio mfupi kuliko mipaka yote ulimwenguni .

HIFADHI YA TAIFA CHOBE

Kuna pia feri ya moja kwa moja kati ya Botswana na Zambia kuvuka mto Zambezi .
Jangwa la Kalahari linafunika theluthi mbili za eneo la Botswana.
Moja ya maeneo muhimu nchini Botswana ni delta ya mto Okavango . Delta ya Okavango ni delta kubwa kabisa duniani, maana yake mdomo wa mto si baharini bali kwenye nchi kavu, maji yakiishia jangwani.

HISTORIA
Historia ya Botswana inaanzia kwa wakazi wa kwanza ambao huaminiwa kuwa ni
wawindaji wa jamii ya Wasani.
Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa
kilimo na uhunzi .

SIASA
Botswana imekuwa na mfumo wa
demokrasia kwa miaka mingi, ikiwa na viongozi ambao huchaguliwa kwa kura ya wananchi wote.
Rais wa jamhuri ni Festus Mogae .

WATU

Msichana akikusanya chakula katika Delta ya Okavango .
Watu wa Botswana hujiita Batswana kutokana na jina la kabila kubwa kabisa nchini (79%). Kuna wakazi takriban milioni 1.6. Kwa sababu nchi ni kubwa msongamano wa watu kwa kilometa za mraba ni 3.4 pekee. Idadi hiyo ndogo imetokana na sehemu kubwa ya nchi hiyo kuwa jangwa.

Lugha inayotumiwa na wakazi walio wengi ni Setswana (Kitswana ) pamoja na Kiingereza.

Upande wa dini, wakazi wengi (73%) ni Wakristo , wakiwemo Waprotestanti (66%) na Wakatoliki (7%). Wafuasi wa
dini asilia ya Kiafrika ni 6%. Asilimia 20 haina dini yoyote.

UCHUMI
Uchumi wa Botswana umekuwa imara kwa miaka mingi na hali ya maisha imeendelea kuwa bora kila mwaka tangu uhuru.

Utajiri wa nchi unatokana hasa na migodi ya almasi, pamoja na machimbo ya shaba na minerali kama vile chumvi.

Watalii wanaongeza pato la taifa hasa kwa sababu ya uzuri wa delta ya Okavango .
Fedha ya Botswana huitwa Pula (yaani
mvua ). Ina thebe (=” ngao “) 100.