Home Makala Kimataifa Chanzo halisi cha majina ya Tanganyika,Afrika

Chanzo halisi cha majina ya Tanganyika,Afrika

1879
0
SHARE

Na Mwandishi Wetu

KABLA ya mwaka 1920 hakukuweko na nchi iitwayo Tanganyika. Kwa kuwa chini ya utawala wa Kijerumani Tanzania Bara iliitwa Deustche Ost-Afrika, ilikuwa lazima Waingereza kutafuta jina jingine baada ya kushika utawala.

Awali katika mwaka 1920, yalipendekezwa majina kadhaa, yakiwemo, “Smutsland”, “Ebumea”, “New Maryland”, “Windsorland”, na “Victoria”, ambayo hata hivyo yalikataliwa yote na Serikali ya Uingereza kutokana na sababu mbalimbali.

Baadaye Serikali ya Uingereza ilielekeza yapendekezwe majina ya kienyeji, ndipo yakajitokeza majina “Kilimanjaro” na “Tabora”, ambayo yalifikiriwa lakini hayakuchaguliwa.

Hatimaye jina “Tanganyika Protectorate” lilipendekezwa na msaidizi wa makoloni na likakubaliwa na Serikali. Inafahamika kwamba, kabla ya ujio wa wageni kutoka Ulaya, wenyeji katika maeneo ya Magharibi mwa nchi waliliita ziwa kubwa lililopo eneo hilo “Ziwa Tanganyika”. Inaelekea hiyo ndiyo sababu kubwa iliyofanya maofisa wa serikali kulikubali jina la Tanganyika kwa sababu lilikidhi matakwa ya sera kwa kuwa lilitokana na majina ya kienyeji.

Hatimaye neno “Protectorate” liliondolewa kutoka jina rasmi la ‘Tanganyika Protectorate’, na badala yake likawekwa neno “Territory”. Kwa hiyo, kuanzia mwaka 1920 hadi uhuru nchi ikajulikana kama “Tanganyika Territory”.”

MCHANGANUO WA NENO ‘AFRICA’

Hebu sasa nieleze chanzo cha neno AFRICA. Kwa Leo Nitachanganua Neno ‘AFRICA’ kwa kuangalia kila herufi Ina maana gani kwa Bara la Afrika. Japo mchanguo upo katika lugha ya Kiingereza ila ufafanuzi utakuwa kwa lugha ya Kiswahili.

AFRICA                        

A-Association (Ushirikiano):

Neno hili linasisitiza kuwa waafrika hawawezi kuendelea kama hawana ushirikiano. Na endapo Waafrika watakuwa na ushirikiano katika nyanja zote za kimaisha kama uchumi na kijamii, bara hili litaweza kupiga hatua za kimaendeleo. Na tumeaona kuna ushirkiano mkubwa unatokea miongoni mwa nchi za kiafrika.

F-Federation (Shirikisho):

Ni kwamba kupitia shirikisho Waafrika wanaweza kuungana na kuwa kitu kimoja. Na kwa msisitizo ndani shirikisho Waafrika wanaweza kupata umoja ambao utawawezesha kufikia malengo yao kwa kizazi cha sasa na cha baadae.

R-Reunion (Kuunganika Tena):

Kabla ya ukoloni Waafrika waliishi pamoja na kila mmoja alimtegemea mwenzie licha ya kila jamii kuwa na mpaka wake.

Baada ya mkutano wa Berlin (1884/1885 ambao uligawa tena bara hili liliweza kuwatenganisha Waafrika. Hivyo baada ya nchi zote kupata uhuru, zinapaswa kuungana tena kwa maendeleo ya kizazi. Na mfano mzuri ni muungano wa Tanganyika na Zanzibra(1964), japo changamoto kibao.

I-intermarriage (Ndoa ya Mseto):

Ifahamike kuwa Waafrika tunatakiwa tuishi kwa kuungana, itakuwa kitu cha ajabu kama tunaungana huku watu wakiwa na makabila yao na ukabila ukipamba moto. Hivyo kupitia ndoa za mseto Waafrika tunaweza kuondoa ukabila ambao Wakoloni waliukuza. Hivyo kupitia ndoa za mseto Waafrika tunaweza kujenga bara letu.

C-Combination (Mchanganyo au Muunganiko):

Kwamba bara la afrika lina lasili mali nyingi sana, kuna mali asili zinazopatikana kwenye kila nchi na kuna maliasili ambazo zinapatika kwa nchi moja moja, kwa mfano madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu.

Sasa basi kama Waafrika tukaunganisha au kuchanganya mali asili zetu na tukazitumia kwa manufaa ya Waafrika, basi tutaweza kukombo jamii zetu katika dimbwa la Umaskini. Leo hii kuna mtanzania hajawahi kuona hata chembe ya madini ya Tanzanite licha ya kuwa yanazalishwa hapa hapa.

A-Agreeing ( Kubaliana au Kupatana).

Mwisho wa siku Waafrika lazima wakubaliane kwa kila jambo. Yaani hapa Waafrika lazima wakubaliane kwa kuishi kwa uapendo, kufanya kazi kwa bidii, kupigana juu ya uovu. Mambo haya hayawezi kufanyika kama hakuna hali ya kukubaliana.

Hivyo ni wakati sasa kwa Waafrika kukubaliana kwa mambo yenye kujenga bara letu.