Home Makala Kimataifa China ni soko jipya au nchi inayoendelea?

China ni soko jipya au nchi inayoendelea?

1485
0
SHARE

xi-jinping_2399584kNA ABDULLAH MBAROUK ABDULLAH

CHINA ni nchi inayoendelea au la? Swali hili ni miongoni mwa maswali yaliyojadiliwa sana na jumuiya ya kimataifa katika miaka kadhaa.

Baadhi ya nchi zilizoendelea zinaona kuwa China imekuwa kundi kubwa la pili la uchumi duniani, hivyo zimeanza kusimamisha utoaji msaada kwa China. Vilevile nchi kadhaa zinaona kuwa China inapaswa kubeba majukumu makubwa zaidi katika mambo ya kimataifa.

Nchini China vyombo vikubwa vya habari vinashikilia kusema China bado nchi inayoendelea, ambayo inabeba majukumu ya kimataifa yanayoambatana na kiwango chake cha maendeleo. Katika kipindi hiki cha uchumi na maendeleo,tutajadili suala hilo.

“Nchi zinazoendelea” si dhana isiyobadilika. tangu miaka ya 60 ya karne iliyopita, mabadiliko yametokea ndani ya nchi na sehemu zinazoendelea. Korea Kusini, Singapore, Hongkong na Taiwan za China zimewakilisha mfumo wa Asia Mashariki, na Brazil, Mexico na Agentina zimewakilisha mfumo wa Latin Amerika, nchi na sehemu hizo zote zimepata maendeleo ya kasi katika mambo ya uchumi.

Takriban miaka 30 iliyopita, uchumi wa nchi hiyo umepata maendeleo ya kasi, hivyo sasa China imekuwa kundi kubwa la pili la uchumi duniani. wakati huo huo uwezo wa jumla wa China umeongezeka, na sauti ya China kwenye jumuiya ya kimataifa pia imeongezeka. Njia ya maendeleo ya China inaitwa kuwa mfumo wa China.

Hivi karibuni Shirika la Kimataifa la Fedha – IMF na Benki ya Dunia – WB, zimetoa ripoti kwa nyakati tofauti kuhusu hali ya maendeleo ya uchumi wa nchi mbalimbali. Katika ripoti yake, IMF limegawa nchi mbalimbali katika makundi ya aina mbili. Mosi; makundi ya uchumi yaliyoendelea na soko jipya Pili; ni makundi ya uchumi yanayoendelea.

Soko jipya ni la aina mpya, kiwango cha maendeleo ya uchumi na kiwango cha viwanda cha nchi za soko jipya ni cha juu kuliko kile cha nchi zinazoendela za kawaida. Kwa upande wa maendeleo ya jumla ya uchumi na jamii, hasa wastani wa mapato kwa kila mtu kwa nchi za soko jipya ni ya chini zaidi kuliko ule wa makundi ya uchumi yaliyoendelea.

Hivyo nchi za soko jipya kihalisi ni nchi zilizoko mbele kiuchumi katika nchi zinazoendelea. Katika ripoti ya IMF, China inawekwa katika nchi za soko jipya na makundi ya uchumi yanayoendelea, ripoti hiyo haielezi China ni soko jipya au nchi inayoendelea.

Kutokana na wastani wa mapato kwa kila mtu, WB imegawa makundi mbalimbali ya uchumi kuwa makundi ya aina tatu; makundi ya mapato ya chini, mapato ya katikati na ya juu. Hadi kufikia Julai 1, 2011 makundi ya mapato ya chini ni yale ambayo wastani wa mapato kwa kila mtu ni chini ya dola Marekani 1,005; makundi ya mapato ya katikati ni ambayo wastani wa mapato kwa kila mtu ni dola za Marekani 1,006 hadi 3,975; yale ambayo wastani wa mapato kwa kila mtu ni dola za Marekani 3,976 hadi 12,275 ni makundi ya mapato ya katikati ya juu; na wastani wa mapato kwa kila mtu ni dola za Marekani 12,276 ni yale ya mapato ya juu.

Katika ripoti ya WB, makundi yenye mapato ya chini na mapato ya katikati yamewekwa katika makundi ya uchumi yanayoendelea. Mwaka 2010 wastani wa thamani ya uzalishaji wa China ulikuwa wa dola za Marekani 4,700, hivyo WB imeiweka China katika makundi ya nchi zenye mapato ya katikati, hivyo China ni nchi inayoendelea.

Baadhi ya mashirika mengine huhusisha China na nchi mpya zinazoinuka kiviwanda. Wizara ya biashara ya Marekani inaona kuwa makundi 10 ya uchumi ni ya soko jipya, yakiwemo pamoja na China, India, Korea Kusini, Mexico, Brazil, Agentina, Afrika Kusini, Poland, Uturuki na Jumuiya ya nchi za Asia Kusini Mashariki. Gazeti la wanauchumi la Uingereza limeweka nchi na sehemu 25 kuwa za makundi mapya ya uchumi, zikiwemo China, Hongkong, Taiwan, India, Korea Kusini, Agentina, Israel, Ureno, Afrika Kusini na Russia.

Katika vigezo mbalimbali vya ugawaji vilivyotajwa hapo kabla, mgongano mkubwa ni kuhusu China ni nchi ya soko jipya, au nchi inayoendelea? Kabla ya kujibu suala hilo, ni lazima tueleze umaalumu wa makundi mapya ya uchumi. Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Uchumi cha Nankai He Zili ameona kuwa, kulinganishwa na makundi yaliyoendelea na nchi zinazoendelea, makundi mapya ya uchumi yana umaalum wake wa aina tano.

Kwanza; makundi mapya ya uchumi si nchi zilizoendela, na mengi yako katika Asia, Ulaya ya kati na ya mashariki na Latin Amerika. Pili; wastani wa mapato yao wako katika kiwango cha katikati au kiwango cha juu, na watu wengi wameondokana na umaskini, na maendeleo ya utamaduni, elimu, afya, michezo, sayansi na teknolojia yamefikia kiwango fulani cha juu.

Tatu; nchi za makundi mapya ya uchumi zimejenga mfumo kikamilifu wa uchumi wa soko huria, na zina utaratibu mzuri wa soko, na mlango wa soko umefunguliwa wazi zaidi, ambayo yamekuwa sehemu muhimu ya utaratibu wa kimataifa kuhusu majukumu tofauti ya utengenezaji na mfumo wa biashara wa kimataifa. Nne; makundi hayo yamepata ongezeko la kasi la uchumi, na uwezo wao wa usafirishaji bidhaa nje ni mkubwa, na yana uwezo fulani katika soko la dunia. Tano; makundi hayo yanafanya juhudi kushiriki kwenye mambo ya siasa, uchumi na jamii duniani, na hali ya maendeleo yao inaweza kuhimiza maendeleo ya uchumi wa dunia.

Zili amesema kimsingi China imetatua masuala yanayozikabili nchi zinazoendelea kuhusu maendeleo ya uchumi na jamii yako nyuma. Hivyo anaona China imegeuka kuwa nchi ya soko jipya kutoka nchi inayoendelea, hivi sasa inafanya juhudi kujiendeleza ili kufikia kiwango cha maendeleo ya nchi zilizoendelea.

Ikiwa nchi ya soko jipya, China inakabiliwa na majukumu magumu ya maendeleo ya uchumi na jamii, na wastani wa mapato ya kila mchina wako nyuma sana duniani. Anaona kuwa China inapaswa kuonesha umuhimu mkubwa zaidi katika mambo ya kimataifa, kwa mfano, China inapaswa kubeba majukumu ya lazima katika masuala makubwa kuhusu uchafuzi wa mazingira, kuongezeka kwa joto duniani, uchimbaji wa maliasili usio na mpango na ongezeko la idadi ya watu kwa kasi ya kupita kiasi.

Hivyo China inapaswa kuendelea kuweka mkazo katika kuendeleza uchumi, kuimarisha mageuzi, na kuhimiza uvumbuzi, ili kuifanya China igeuke nchi yenye uchumi wa kisasa kutoka nchi ya soko jipya.

Wasikilizaji wapendwa, mnaendelea kusikiliza kipindi cha uchumi na maendeleo kutoka Radio China Kimataifa.

Mwanauchumi mkuu wa IMF Olivier Blachad hivi karibuni ametoa onyo kuwa, kutokana na hali ya mwisho wa mwaka 2011, ni vigumu zaidi kwa uchumi wa dunia kufufuka na kurudi kwenye njia ya kawaida. Amesema mwanzoni mwa mwaka 2011 uchumi wa dunia ulianza kufufuka, ingawa ulikabiliwa na changamoto nyingi, lakini hali ilikuwa inaweza kudhibitiwa kuliko hali ya hivi sasa.

Tangu mwaka huu, uchumi wa makundi mengi yaliyoendelea haufufuki, na uchumi wa dunia kwa hivi sasa unakabiliwa na hali mbaya zaidi kuliko mwaka 2008.

Mwanauchumi huyo amesema tunapaswa kuzingatia mambo manne. Kwanza; mzunguko wa fedha si kama tu unaathiri hali ya benki, pia unaathiri hali ya serikali. Kama hakuna mzungumzo wa fedha unaoweza kuhakikisha mikopo na faida za benki zinadumishwa kwenye kiwango kizuri, hatari itakuwepo siku zote.

Pili; kama sera zilizotolewa na serikali hazitatekelezwa kihalisi, na matumaini ya wawekezaji hayatatimizwa, basi hali ya mambo itakuwa mbaya zaidi. Tatu; serikali za nchi mbalimbali zinapaswa kurekebisha sera za fedha kwa utaratibu na utulivu.

Nne; kama soko zima litafikia maoni ya pamoja, kwa mfano kama wakisema fedha za Euro hazitatumika, basi maoni kama hayo hayataondolewa kirahisi.

Hivyo mwanauchumi huyo amezitaka nchi mbalimbali zishirikiane na kuchukua hatua ili kuimarisha sera za fedha, kuongeza mzunguko wa fedha, na kutekeleza sera halisi.

EMAIL Dullahmendhry@yahoo.com

contact 0657310184..