Home Makala DATA HAZIDANGANYI CCM, CHADEMA WANA NAFASI SAWA 2020

DATA HAZIDANGANYI CCM, CHADEMA WANA NAFASI SAWA 2020

849
0
SHARE

Rafiki yangu na Ndugu yangu Gulatone Masiga ametoa idadi ya ya mashina ya muundo mpya wa CCM yatakuwa 2,22,230 nchi nzima ambapo kila moja likiwa na wanachama 50 hivyo kufanya kuwa na jumla ya wanachama 11,111,500 nchi nzima. Kwa hiyo hizi ndio kura za wanaCCM za kuanzia 2020. Ila sikubalini naye kuwa ndiyo gurantee ya kusema kuwa CCM itashinda moja kwa moja tuna kazi ya kufanya bado.

Mwaka 2015 kwa jumla, wapiga kura wote walikuwa 23,253,982. Kwa kutumia uchaguzi ule wa mwaka 2015 chukua idadi ya wapiga kura wote ambao walijiandikisha toa idadi ya wanaccm kwa kutumia muundo huu mpya utagundua kuwa wanaobaki ni wengi kuliko wanaccm twende kimahesabu 23,253,982 hawa walijiandikisha 2015 toa 11,111,500 hawa ni wanachama wa CCM kwa muundo huo mpya unapata watanzania ambao si wana CCM 12,142,482.

Kwa kuwa nimetumia uchaguzi wa mwaka 2015 kutafuta tofauti hiyo basi 2020 watakaojiandikisha tunatarajia kuongezeka zaidi ya waliojiandikisha 2015. Kama ni hivyo basi idadi ya watanzania ambao watakuwa si wanaCCM itaongezeka zaidi. Twende kisayansi zaidi.

Tanzania kila baada ya miaka kumi ya Sensa ongezeko la watu huongezeka kwa asilimia 11. Mfano toka 1992 hadi 2002 ongezeko la watu lilikuwa asilimia 10, mwaka 2002 hadi mwaka 2012 ongezeko la watu lilikuwa asilimia 21. Kwa hiyo utaona kila baada ya miaka 10 ya sensa kuna ongezeko la watu asilimia 10 hadi 10+.

Asilimia hizi za ongezeko la watu huongezeka kwa kila kundi kwa hiyo ukichukua waliojiandikisha 2015 ambao walikuwa wapiga kura 23,253,982 halafu ukatafuta asilimia 11 yake hizi asilimia 11 kundi hili la wapiga kura litapata ongezeko la watu 2,557,938.02. Inawezekana idadi hii ikaongezeka zaidi kwa kuwa death rate ya mtanzania inaongezeka kwa sasa kwa maana hiyo naiacha data hiyo hivyo hivyo kwa kuwa itakuwa imebaki miaka miwili ifike mwaka wa Sensa wa 2022.

Ongezeko hili ukalijumlisha na wale walio jiandikisha 2015 utapata jumla ya kadirio la watakaojiandikisha 2020 ambao ni jumla ya wapiga kura 25,811,920.02.

Idadi hiyo sasa toa hapo idadi ya wanaCCM wote kutokana na muundo huo mpya wa matawi ya CCM. Chukua 25811,920.02 idadi ya wapiga kura watakaojiandikisha 2020 toa 11,111,500 idadi ya wanaccm kwa kutumia muundo huu mpya wa matawi ya CCM utapata tofauti ya wasio wanaCCM 14,700,420.02.

Kwa kutumia data hizo nani atakuwa na wapiga kura wengi?

Kuna factor nyingi sasa hapa tunatakiwa tuziangalie. Hakuna gurantee yeyote iliyowekwa kuwa wanaCCM wote hapo wataipigia CCM kura. Labda kama kura hiyo itakuwa ni ya wazi. Na hakuna Gurantee yoyote kuwa CCM imepoteza kura zote za wasiokuwa wanaCCM hapo juu ambao ni idadi inayozidi wanaCCM wenyewe.

Kwa CCM

Kama CCM itakumbwa na lile jini lake la Makundi 2020 basi ni dhahiri kuwa hii idadi ya wanachama itapasuka. Sioni kama kutakuwepo na makundi sana kwenye ngazi ya Uras kwa kuwa kwa utamaduni wetu mgombea hubadilishwa kila baada ya miaka 10. Tatizo litakuwepo kwenye kura za maoni kwa wabunge na Madiwani. Kama CCM haitatengeneza mazingira mazuri ya kura hizi za maoni huku chini basi kutakuwa upungufu mkubwa wa Kura hapa.

Kama CCM haitakamilisha ahadi zake kubwa kubwa kama ile ya Milioni hamsini itakuwa pia ngumu kwa CCM kujieleza jukwaani.

Kuna tatizo lingine la msingi sana hapa kama Vijana wengi watajiandikisha kupiga kura na wakajitokeza kupiga kura itazipunguza kura za CCM. Ukosefu wa ajira kwa vijana umewatia uchizi kabisa na kama Serikali haitachukua jitihada za makusudi kuhakikisha wanaligusa kundi hili tutegemee kuadhibiwa 2020.

Kwa CHADEMA

Sijui kama mgombea wao atakuwa ni yule yule au watambadilisha. Kama watamsimamisha Lowassa kilichotokea 2015 kitajirudia atakaribia kushinda ila hatashinda. Sio siri kwamba Lowassa kapunguza umaarufu na hata nguvu za kufanya siasa nazo zimepungua. Makandikando yake bado anatembea nayo na sioni mahali atakapojisafishia kabla ya 2020.

Kama wakimbadilisha mgombea CCM inaweza kupata wakati mgumu zaidi. Kura ya turufu ikimwangukia Lisu wataisumbua sana CCM kwa kuwa katika kipindi hiki cha awamu ya Tano ndiye mwanasiasa pekee toka upinzani aliyeweza kuisumbua CCM.

Kama akigombea anaweza kupata kura karibia asilimia 90 ya watu ambao hawana nasaba na CCM jambo ambalo litatusumbua sana.

Kama watakuja na plan B ya namna ya kushughulikia sera ya vijana Bungeni na kuwapigia Kelele basi watawakamata kweli. Na mtunga sera wao na mtunga Ilani ya Chadema kama atawekeza kutafiti zaidi kuhusu matatizo ya vijana na kuonyesha kwa kina ni namna gani watawashughulikia basi watanufaika mno na eneo hilo.

Kutokukamilika kwa ahadi nyingi kubwa kubwa za CCM itakuwa ni kicheko kwao kwa maana hiyo CCM ina kazi kubwa kweli kuwekeza zaidi kwa yale waliyoyatamka jukwaani kuliko yale ambayo hawakuyatamka.

Upinzani unatakiwa kuungana sasa na kuwa kitu kimoja kama kweli adui yao ni mmoja. Kitendo cha kuwa na utitiri wa vyama ni ugonjwa ambao utawatafuna daima.

Hitimisho

Kwangu bado naona kila chama kina nafasi kama kitachanga karata zake vizuri.

Ole Mushi.