Home Makala Dhana ya kufanya vibaya, vizuri kwa mashirika ya umma

Dhana ya kufanya vibaya, vizuri kwa mashirika ya umma

845
0
SHARE

Kwa siku kadhaa kumekuwa na sakata la baadhi ya taasisi za umma kutokuwa na hati nzuri katika mahesabu yake. Naomba nikiri nimepata taarifa hizi kupitia mtandao ya kijamii, lakini jambo lililonivutia zaidi ni kuhusisha yanayotokea katika mashirika ya umma na utendaji wa kamati za Bunge.

Hii ni dunia huru hivyo watu wana uhuru wa kutoa maoni lakini cha kustaajabisha wasomi wamekuwa mbele kupotosha ama kwa kujua au kwa nia ovu.

Kimsingi ni vizuri tukajifunza misingi ya kidemokrasia ambayo na nchi yetu inajitahidi kuifuata, moja ya msingi huo ni mgawanyo wa majukumu , madaraka nadhani nitakuwa nimetumia kiswahili fasaha yaani “separation of power”.

Sio nia yangu kuwarudisha katika stadi za urai lakini katika dhana ya separation of power tunakuwa na executive wing ambapo ndipo hayo mashirika ya umma na mkondo mzima wa utendaji wa serikali upo, pili tuna Bunge lenye kazi ya kuisimamia hiyo executive wing na serikali kwa ujumla halafu tuna mahakama wenye mamlaka ya kutoa haki.

Katika yanayoendelea katika mitandao ya kijamii naona kwamba leo kamati za bunge zinachukuliwa kama auditing and performance monitoring /evaluation committee badala ya kuchukuliwa kama oversight committee ambapo zinafanyia kazi taarifa ya taasisi nyingine zilizopewa nguvu kisheria kufanya kazi hizo za auditing pamoja na performance evaluation na hapa ndipo tunapata taasisi kama National Audit Office.

Moja ya mambo yanayo pigiwa chapuo sana na sisi waumini wa mifumo ni kwamba kuna haja sana ya kuwa na check and balance tena iwe in real time na ndipo hapo tunaona umuhimu wa kuimarisha vyombo kama mahakama, NAO, PCCB, Jeshi la Polisi kwa upande mmoja na taasisi kama Presidential Delivery Bureau pamoja na tume ya mipango kwa upande mwingine. Hiyo PDB naona kama inaelekea huko inaloelekea.

Kazi ya kamati za bunge kama oversight committe ni kupitia kazi zilizofanywa na executive part of our government sasa kama kuna ufisadi umefanyika halafu kamati ya bunge ya kisekta haikuuona hapo sioni kama ni shida.

Itakuwa ni tatizo pale tu endapo taarifa hizo zilikuwepo kwenye vyombo halali vya kisheria kama ripoti za CAG halafu kamati fulani ya Bunge kwa makusudi kabisa wakafumbia macho maovu hayo, hapo kweli lazima tuwamulike au pengine kulikuwa na public cry katika jambo fulani kuhusu taasisi fulani na kamati ya kisekta ya Bunge akalifumbia macho then hapo kuna kila sababu ya kuwamulika.

Kwa hoja hiyo naona tunazionea bure kamati hizi za kisekta za bunge na endapo kuna mtu mwenye ushahidi kwamba masuala yanayo zungumziwa leo kuhusu taasisi yoyote yalikuwemo katika ripoti za CAG ambapo wajumbe wa kamati hizo pamoja na mwenyeviti wa kamati husika za bunge walilifumbia macho basi wenyeviti hao pamoja na kamati zai basi itakuwa vyema ushahidi huo ukawekwa hadharani na hapo tutapata njia ya kuweza kushughulikia kadhia hii.

Nadhani namna bora ya kuweza kumsaidia Rais Magufuli katika kuelekea Tanzania ya viwanda ni lazima tuwe wa kweli na kweli tupu, tujitahidi kuweka ukweli mbele badala ya ukeleketwa.

Lazima tuwe ni Taifa la watu wazalendo na wenye kutumia weledi, nje ya hapo hakuna aliye salama na tutatumia muda mwingi kujadili watu badala ya kujadili masuala ya maendeleo.

Nikutakieni siku njema