Home Makala Diplomasia ya kutatua migogoro duniani yazidi kufeli  

Diplomasia ya kutatua migogoro duniani yazidi kufeli  

624
0
SHARE

NA HILAL K SUED

INAVYOONEKANA hakuna mtu amemwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry, kwamba enzi ya kusuluhisha migogoro duniani inayoyoma.

Katika harakati za kutatua migogoro duniani  Waziri huyo amekuwa  wa kwanza katika historia kusafiri zaidi ya kilometa 1.9 milioni akiwa ametembelea nchi 88, huku nchi nyingine akiwa amezitembelea zaidi ya mara moja, na hivyo kuwa hewani ndani ya ndege kwa zaidi ya siku 111.

Sasa hivi bado ana miezi minne hadi kumaliza kipindi chake ili aweze kuvunja rekodi ya mtangulizi wake katika nafasi hiyo – Hillary Clinton ya kutembelea nchi 112, inagawa alisafiri kilometa chache kufanya hivyo.

Wiki iliyopita Kerry alikuwa Geneva, Uswisi akiwa na waziri wan je wa Urusi Sergei Lavrov, wakijaribu kuweka vipengele vya mwisho vya makubaliana katika kupambana na Dola ya kiislamu (ISIS).

Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden piaametumia muda mwingi nchi za nje kuliko makamu marais wengi, hivi karibuni akisaidia kuleta maelewano baina ya Israel na Uturuki. Na huu, kwa kiasi kikubwa, ndiyo umekuwa msimamo katika sera ya utawala wa Barack Obama ambao umewekeza sana kupitia ‘nguvu laini’ ya Marekani.

Hapa suala muhimu ni: safari nyingi hizi za nchi za nje zimeleta nini? Hakuna shaka kwamba mkataba uliofunganisha nchi kadha kuhusu usitishwaji wa mpango wa nyuklia wa Iran usingefikiwa bila ya Kerry kufanya ziara za mara kwa mara katika miji mikuu ya nchi mbali mbali husika na mikutano ya hadi usiku wa manane katika mahioteli ya Austria na Uswisi. Lakini kwingineko, tija iliyopatikana haijaonekana vizuri.

Katika miaka ya 70, jitihada kubwa za Henry Kissinger waziri wa nje wa Marekani kutafuta upatanishi kuhusu mgogorowa Mashariki ya Kati baina ya Israel, Syria na Misri ndiyo zilikuwa mwanzo wa kinachoitwa ‘shuttle diplomacy’ – yaani diplomasia ya kusafiri safari na hadi leo diplomasia ya aina hii ndiyo inatumika katika jitihada za Marekani kutafuta suluhu ya mgogoro wa siku nyingi baina ya Israel na Wapalestina.

Jitihada hizo ziliendelea hadi katika utawala wa Obama, uliomhusisha Seneta wa zamani Geiorge Mitchell akiwa kama mjumbe maalum kwa kazi hiyo hadi mwaka 2011, akiwa chini ya Waziri wan je Hillary Clinton, na baadaye John Kerry mwenyewe alipomrithi Clinton mapema mwaka 2013.

Lakini staili hii pia imekuwa kaburi la  ‘kidiplomasia’ au tusema ari ya kidiplomasia. Makubaliano yamezidi kwenda mbali na haitarajiwi katika miezi yake mine hii iliyobaki Kerry anaweza akafanya chochote.

Syria pekee ndiyo itachukuwa muda wake mwingi na nguvu katika kipindi chake kilichobaki. Mgogoro unaozidi kuzama katika tope unatajwa kuwa ni janga kubwa la Karne hii ya 21. Kwani pale watawala na wanadiplomasia wakikutana katika mahoteli ya Geneva Uswisi, mauaji na ghasia zazidi kushika kasi nchini Syria, kitu ambacho kimeibua maswali kuhusu faida ya kufanya diplomasia, ile ya kusafiri safari au nyingine.

Wajumbe nguli watatu wa Umoja wa Mataifa wamejaribu kutafuta ufumbuzi: Kofi Anan, Lakhdar Brahimi na sasa hivi ni Staffan de Mistura. Lakini jitihada za hawa hazikufika popote.

Katika siku za hivi karibuni De Mistura alilazimika kusitisha kikosi kazi cha misaada cha Umoja wa Mataifa kwa sababu hakunna kanvoi za misaada zilizokuwa zinaruhusu kuingia katika maeneo yaliyozingirwa nchini Syria.

Na kwa kiwango kikubwa, kushindwa huku kumetokana na staili ile ya mivutano ya wakati wa Vita Baridi – Urusi na Iran upande mmoja, na nchi za Magharibi na nyingine nyingi za Kiarabu upande mwingine – kuhusu hatima ya Bashar al-Assad na utawala wake. Wachnguzi wa masuala ya mgogoro huo wanasema al-Assad anadumu kutokana na misaada mikubwa ya kijeshi anaopata kutoka Urusi na Iran.

Lakini kiini hasa cha kudorora katika kupata ufumbuzi ni kipya na cha zamani. Aidha ni dalili za kukatika kwa diplomasia kutokana na vikundi vingi vinavyopigana nchini humo ambavyo havishirikishwi katika meza za majadiliano.

Hivyo kwa wasuluhishi kusafiri na kukutana Geneva au Vienna kunaonekana hakuzingatii hali halisi ya mauaji yanayoendele nchini Syria. Kuingia ndani ya ndege, kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na pia kuendesha vikao vya upatanishi kumeshindwa kubadili mambo.

Usuluhishi wa migogoro ya kimataifa unatatizwa na suala linalotokana na kizazi kipya. Tangu enzi ya msuluhishi wa kwanza wa Umoja wa Mataifa Count Folke Bernadotte alipopelekwa iliyokuwa Palestine mwaka 1948, sasa hivi umri wa wastani wa wasuluhishi wa umoja huo ni miaka 64. Brahimi alikuwa ana umri wa miaka 80 na De Mistura sasa ana miaka 70.

Kati ya wasuluhishi 52 katika kipindi chote kile ni watatu tu ndiyo walikuwa wanawake. Sababu hapa ni kwamba wasuluhishi wa umri mkubwa wanavutia heshima.

Hivyo kutuma wasuluhishi ambao ndani yao kuna watu wenye umri mdogo au wanawake hauwezi kupambana na changamoto za kuleta amani katika maeneo ambayo wapiganaji ni watu wa itikadi kali na harakati zao kubwa ni ghasia na vurugu tu.

Isitoshe shughuli za usuluhishi zimekuwa hatari tangu zamani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld aliuawa mwaka 1961 huko Congo (sasa DRC) akiwa katika ziara ya kutafuta ufumbuzi wa amani nchini humo. Kifo chake, ingawa kilitokana na kuanguka kwa ndege, lakini kiliibuwa maswali mengi na hadi sasa Umoja wa Mataifa inaendelea kufanya uchunguzi.

Na takriban miaka 10 iliopita katika migogoro ya Mashariki ya Kati, Bara la Afrika na Yugoslavia, wasuluhishi wa nguvu walikuwa Wamarekani ambao walikuwa na silaha ya ‘akiba’ ya kiuchumi na kijeshi iwapo usuluhishi wa kawaida utashindikana.

Kwa ujumla, diplomasia, pamoja na upotevu wa kilometa nyingi za kusafiri safari na kukaa mahotelini ni gharama kubwa, lakini gharama hizi ni ndogo sana ukilinganisha na gharama za kuendesha vita.

Angalia kwa mfano yanayotokea huko Yemen. Usuluhishi wa kidiplomasia hauwezi kuleta matokeo mara moja, lakini kwa sababu hakuna jitihada madhubuti za kuzishirikisha Saudi Arabia na Iran ambazo zinasaidia kijeshi pande zinazokinzana nchini humo ni suala linalosikitisha sana.