Home Uchambuzi EAC na changamoto za kukuza sekta ya viwanda

EAC na changamoto za kukuza sekta ya viwanda

2288
0
SHARE

NA LEONARD MANG’OHA

Katika kukuza sekta ya viwanda, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ina sera na mkakati ulioanza mwaka 2012 hadi 2032.

Mkakati huo unalenga kuimarisha uzalishaji wa viwanda ili kuharakisha mabadiliko ya muundo ya uchumi wa jumuiya.

Pia mkakati huo unatilia mkazo uendelezwaji wa minyororo ya thamani ya kikanda miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya ili kuongeza ajira na ubora wa kazi na bidhaa zinazozalishwa.

Sasa ukubwa wa pato la pamoja la mataifa wanachama wa EAC (GDP) ni dola za Marekani bilioni 155.2 zaidi ya Sh trilioni 354.6 huku ukuaji wa pato lake ni wastani wa asilimia 5.8 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Mwaka 2015, EAC ilitajwa kama ukanda unaokuwa kwa kasi zaidi barani Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo ukanda huo ulikuwa na ukuaji wa pato la wastani wa asilimia 6.2.

Nguzo kuu ya jumuiya hii ni pamoja na masoko ya uhakika ikiwamo jumuiya yenyewe ambayo wananchi wake wanafikia milioni 177,  COMESA watu milioni 400, pamoja na mikataba mbalimbali ya baina yake na Umoja wa Ulaya (EU) unaofahami kama ‘EBA’ pamoja na ule unaohusisha EAC na Marekani unaoruhusu uuzwaji wa bidhaa zote zinazozaliswa katika nchi wanachama wa EAC na kwenda Marekani unaofahamika kama AGOA.

Ukanda huu ni miongoni wa maeneo yanayoongoza duniani kwa vivutio vya utalii wa wanyamapori na safari. Lakini pamoja na fursa hizo bado jumuiya hii imeendelea kukua kwa mwendo wa kujikongoja kiasi katika nyanja mbalimbali ikiwamo kilimo, viwanda utalii na nyinginezo.

Kwa mfano licha ya sekta ya viwanda na kilimo biashara kutajwa kama shughuli kuu ya kiuchumi katika jamii miongoni mwa nchi wanachama, bado uchumi wake umeendelea kuwa chini kutokana na uwekezaji mdogo katika sekta hizi na uelewa mdogo wa wananchi juu ya fursa za uwekezaji.

Takwimu zinaonesha kuwa sekta ya viwanda kwa sasa inachangia asilimia 10 tu kwenye pato la jumuiya ikilinganishwa na sekta ya kilimo inayochangia kwa asilimia 34.7 huku sekta ya huduma ikichangia kwa asilimia 44.8.

Kiasi cha ukuaji wa kiwango cha uzalishaji wa viwanda katika EAC ni asilimia 4.7 tu tofauti na kanda nyingine kama vile ECOWAS ambayo ukuaji uzalishaji wake ni asilimia 7.8.

Kutokana na uzalishaji mdogo wa viwanda umeifanya EAC kuagiza hadi asilimia 70 ya mahitaji yake ya bidhaa za viwandani kutoka nje ya jumuiya hiyo jambo linalofanya hali ya biashara na kuendelea kuwa duni.

Gharama kubwa za umeme nazo zinatajwa kuwa kikwazo kingine cha ukuaji wa sekta ya viwanda miongoni wa nchi wanachama kutokana na gharama za uzalishaji ambazo husababisha bidhaa zinazozalishwa katika jumuiya hiyo kuuzwa kwa gharama kubwa.

Katika nchi wanachama wa jumuiya hii gharama za umeme kutoka katika gridi ya taifa ni zaidi ya senti 15 fedha za Marekani kwa unit moja ikilinganishwa na baadhi ya nchi ambazo unit moja huuzwa chini ya senti 10. Mfano ni Marekani ambayo unit huuza senti kwa senti saba, China senti tano sawa na Ethiopia ambayo hata hivyo inatarajiwa kushusha gharama hiyo hadi senti tatu katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Mataifa wanachama wa jumuiya hiyo yamekuwa yakichukua hatua mbalimbali za kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu katika mataifa husika na jumuiya kwa ujumla ili kuwezesha kufikiwa kwa maendeleo ya viwanda baadhi ya juhudi hizo ni pamoja na zile zinazochukuliwa na Tanzania ikiwamo uzalishaji wa umeme wa gesi na mpango wa sasa wa ujenzi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa maji katuika bonde la Mto Rufiji wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2100.

Lengo la jumuiya ni kupunguza pengo la sasa la ukosefu wa nishati ya umeme ili kufikia malengo ya uchumi wa viwanda. Jitihada hizi zinalenga kukabiliana na upungufu wa umeme, kufikia ya kanda mwaka 2018, na kupunguza gharama ya nishati kwa wastani wa Senti nane za Marekani 8 hadi mwishoni mwaka huu.

Eneo linalopewa kipaumbele na jumuiya hiyo ni ujenzi wa miundombinu ambayo ni muhimu kwa ufanisi wa sekta ya viwanda na biashara, ambapo kila inalenga kuwekeza katika uimarishaji wa miundombinu ya barabara, anga na reli, nishati teknolojia ya habari na mawasiliano pamoja na upatikanaji wa maji.

Ili kufikia malengo ya jumuiya hiyo na taifa moja moja ya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2050 ni lazima kuhakikisha sera ya viwanda inasimamiwa kikamilifu kwa kuongezeka uwekezaji katika viwanda na biashara pamoja na kukuza seka ya kilimo ni ambayo inaajiri wananchi wengi miongoni mwa nchi wanachama.

Pia hatua muhimu kama vile maboresho katika uzalishaji bidhaa hususan kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora wa kushindana katika masoko ya kimataifa na kuvutia zaidi uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje ya nchi sambamba na kukuza wataalamu wa ndani wenye ujuzi wa kuendesha viwanda.

Katika kutekeleza malengo hayo jumuia iliamua kutoza ushuru wa asilimia kwa malighafi na bidhaa nyingine zinazotumiwa katika miradi ya uzalishaji na uwekezaji. Baadhi ya bidhaa hizo ni pamoja na mitambo na vifaa vya umeme, bidhaa za dawa na chuma