Home Makala ELIMU INAHITAJIKA KUKABILI KESI ZA WATOTO

ELIMU INAHITAJIKA KUKABILI KESI ZA WATOTO

3936
0
SHARE

NA WILLBROAD MATHIAS


Kanuni za Mwenendo wa Mahakama ya Watoto za Mwaka 2014, ni  tangazo  la  Serikali  Na. 270,  ambalo lilitolewa Julai   25, 2014. Tangazo hili ni tafsiri  rasmi  iliyosanifiwa  na Ofisi  ya  Mwanasheria  Mkuu  wa Serikali,  na kuchapishwa  kwa  mujibu  wa  Kifungu  cha  84  cha  Sheria  ya Tafsiri ya Sheria Mbalimbali

Lengo  la  Kanuni  hizi  ni  kuanzisha  mfumo  wa utendaji  na  mwenendo  unaowiana  wa Mahakama za Watoto  za Tanzania Bara, na kuhakikisha kuwa haki za mtoto chini ya sheria  zinazolindwa.

Kanuni hizi inaelezwa wazi kwamba Mahakama katika kutekeleza    mamlaka yoyote yaliyotolewa kwake, chini ya Kanuni hizi, au katika kutafiti kanuni yoyote, itazingatia lengo la Mahakama ya Watoto.

Kila Mahakamaya watoto chini ya Sheria hii, itatambulika kwa jina lake mahsusi na mahali au eneo.

Mbali na hilo, kanuni hizo zinaeleza jinsi mambo kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na Jengo la Mahakama ya mtoto linavyotakiwa kuwa, mazingira, uendeshaji wa mashauri, lugha ya Mahakama, masharti ya wakalimani, kuendesha kesi kwa faragha na uamuzi kuhusu umri.

Baadhi ya ya mambo mengine ambayo yameahinishwa  katika kanuni hizo ni pia utoaji wa taarifa kwa mtoto kuhusu utaratibu, msaada wa kisheria na misaada mingine inayofaa, uteuzi wa mlezi, mamlaka ya hakimu kuendesha kesi, mambo ya kuingizwa katika jalada la kesi ya jinai, mambo ya kuingizwa katika jalada la shauri la madai na kupata na uchambuzi wa kumbukumbu za Mahakama mambo mengine ambayo yameahinishwa pia katika kanuni hizo ni Mwenendo wa Mahakama, kutolewa kwa hati ya wito, kukamatwa kwa mtoto, hati ya ukamataji, hati ya mashitaka, mahudhurio ya wazazi, walezi au waangalizi, mzazi, mlezi au mwangalizi, shauri kutoendeshwa bila uwakilishi wa mtoto, dhamana, kuwekwa mahabusi, tathmini ya awali ya mtoto, mapitio ya amri ya kuwekwa mahabusu ni nyingine nyingi zinazohusu mwenendo mzima.

 

Kanuni nyingine ni jinsi ya kujibu shitaka, pale ambapo mshtakiwa ana kubali kosa, muda wa kuendeshwa kwa kesi ya jinai, ushiriki wa mtoto katika mwenendo, jukumu la kuweka wazi kesi ya upande wa mashtaka, usikilizwaji wa awali, kuahirishwa kwa shauri kutokana na kutohudhuria kwa wahusika au mashahidi, ushahidi wa upande wa mashtaka, kupokelewa kwa ushahidi wa kitabibu na kupokelewa kwa ushahidi wa maungamo kanuni nyingine ni ya utetezi. ushahidi mkuu wa  mtoto mshitakiwa Mamlaka ya  Mahakama kuamuru utolewaji wa ushahidi, udadisi wa mashahidi, mtoto kutiwa hatiani, taarifa ya uchunguzi wa kijamii kabla ya hukumu na hadi hukumu.

Hata hivyo, pamoja na kanuni hizo kutafsriwa vyema na kwa umakini wa hali ya juu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wadau wanaona bado kuna haja ya watendaji na jamii kwa ujumla wanahitaji kupigwa msasa zaidi ili waweze kuzifahamu vyema na kuzingatia ili kupunguza changamoto zinazowakabili watoto wanaojikuta katika ukinzani wa sheria.

 

Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) ni kati ya wadau hao ambao wanasema kwamba kama elimu itatolewa kwa watendaji wa idara hiyo  ya mahakama na wana jamii itaweza kuwasaidia kukabiliana na changamoto hiyo ya watoto waliopo katika ukinzani kisheria.

Katika taarifa yao ya hivi karibuni TAWLA wanasema kuwa katika maeneo mbalimbali ya nchi ambayo wamefanikiwa kuyazungukia wanaona bado kuna changamoto kubwa hususan kwa jamii na watendaji katika masuala yote yanayohusu uendeshaji wa kesi za watoto.

Wanasema changamoto hizo ndizo zinazowafanya baadhi ya watoto kujikuta wakisota muda mrefu mahabusu bila kupata msaada na huku baadhi yao kesi zao zikiendeshwa katika mazingira ambayo sio rafiki.

“Kwa mafano katika kanuni ya sita kifungu (1) ambayo inaeleza kuhusu jengo la  Mahakama ya  mtoto inaeleza wazi kwamba pale  ambapo hakuna  jengo  mahsusi  la Mahakama zaidi ya jengo la kawaida   linalotumika kwa ajili ya usikilizwaji wa  kesi kwa ajili au dhidi ya watu wazima,  mahakama itakaa  katika  chumba  cha Mahakama kilichotengwa au katika chumba cha hakimu; au kwa   kadri  itakavyowezekana,   itakaa katika   muda tofauti  na  wa mahakama ya  watu  wazima  ambao  utapangwa   na     Hakimu     Mkazi  Mfawidhi,”wanafafanua wanasheria hao.

Hata hivyo wanasema kuwa pamoja na kanuni kuagiza hivyo, changamoto bado ni kubwa kutokana na uhaba na miundo mbinu mibovu ambayo inazikabili mahakama nyingi kwa hapa nchini.

TAWLA wanasema pia mbali na hilo changamoto pia ni kubwa kutokana na uhaba wa watumishi katika mahakama hizo kutokana na mrundikano wa kesi nyingine ambazo zinatakiwa kusikilizwa na watumishi hao.

Wanasema hali hali hiyo imekuwa ikisababisha kesi zinazowakabili watoto kukaa muda mrefu ama kulazimika kusafirishwa hadi wilaya na hata mkoa mwingine kwa ajili ya kusikilizwa kesi zao.

“Kifungu kingine ambacho kinagusia eneo hilo ni kile namba saba ambacho  kinaelezea Mpangilio wa Mahakama na utaratibu wa usikilizwaji wa  mashauri, kikileza kuwa  kwa  kadri itakavyowezekana  itakuwa  kwa  mujibu wa kifungu cha 7 ambapo ni kwamba Pale   ambapo Mahakama

Inakutana katika  jengo hilo hilo  la  Mahakama linaloendesha  kosa  dhidi  ya  watu  wazima, Afisa Msajili atahakikisha watoto wanaohudhuria Mahakama hiyo hawatumii    chombo    hicho    hicho    cha    kusubiria    au    eneo linaloshikilia watu wazima wanaotuhumiwa makosa ya jinai,”wanasema TAWLA.

Hata hivyo wanasema jambo hilo pia kwa sasa ni vigumu kutokana na sababu ambazo wamezitaja hawali za uhaba na majengo, watumishi na vitendea kazi.

Wanasema ukiachilia na upungufu huo ambao wameubaini, pia kwa upande wa jamii nako kuna changamoto zao hususan katika kuelewa mwenendo mzima wa kanuni za mahakama za watoto.

Wanasema katika utafiti wao wamebaini kwamba pia jamii imekuwa haina uelewa wa kutosha hali ambayo imekuwa ikiwafanya wajikute wakati mwingine nao wakiingia matatani, badala ya kumsaidia mtoto.

TAWLA wanasema kifungu cha  25 (1) cha Kanuni za Mwenendo wa Mahakama ya Watoto kinaeleza wazi kuhusu mahudhurio ya wazazi, walezi au waangalizi watoto.

Wanasheria hao wananukuu kifungu hicho wakieleza kuwa kinasema wazi kwamba pale ambapo mzazi, mlezi, au mwangalizi aliye na taarifa  ya  shauri  la  mtoto  kashindwa  kuhudhuria  katika  shauri  la  jinai  linalomhusu  mtoto  huyo, Mahakama inaweza  kutoa  hati  ya wito    kumtaka    mzazi,    mlezi    au    mwangalizi kuhudhuria Mahakama ni kwa muda uliopangwa, isipokuwa kama (a)haitakuwa  kwa  maslahi  ya  mtoto,  mzazi,  mlezi  au mwangalizi kuhudhuria; (b) haiwezekani    kwa    mzazi,    mlezi    au    mwangalizi kuhudhuria.

 

Wanasema kwa mujibu wa kanuni hiyo   Ikiwa  mzazi,  mlezi  au  mwangalizi  aliyepokea  wito kwa  mujibu  wa  kanuni  ndogo  ya  (1)  kashindwa  bila  sababu  ya

msingi  kuhudhuria Mahakamani, Mahakama inaweza  kutoa  wito  mtu  huyo  aletwe Mahakamani  katika  muda  na  mahali  kama itavyoelekezwa katika hati hiyo.

“Sehemu ya tatu ya kanuni hiyo inaeleza pia   Ikiwa Mahakama itajiridhisha kwa ushahidi wa kiapo  kwamba  mzazi,  mlezi  au  mwangalizi  hawezi  kuhudhuria  shauri

Mahakamani   linalomhusu   mwanawe isipokuwa   mpaka   kwa shinikizo, Mahakama hiyo  inaweza  kutoa  hati  ya  kukamatwa  na kumfikisha  shahidi  mbele  ya Mahakama katika  muda  na  mahala patakapo ainishwa katika hati hiyo ya kukamatwa,”wanabainisha wanasheria hao.

Wanasema pia katika kanuni hiyo kifungu cha (4) inaeleza kuwa pale    ambapo wazazi,    walezi    au    waangalizi  hawakufahamishwa    ndani    ya    muda    wa    kutosha    kuweza kuhudhuria,  au  wameshindwa  kuhudhuria  kwa  sababu  za  msingi, Mahakama  kwa   dhumuni   la   kuhakikisha   haki   inatendeka, inaweza kutengua maamuzi au amri yoyote.

Hivyo wanashauri ni lazima jamii nayo pate elimu kuhusu kanuni hizo ili iweze kupata mwanga kuhusu kanuni hizo na kuisaidia kujiingiza  katika msuguano na sheria kwa kuanzisha kesi nyingine, baada ya kushughulikia ambayo inawakabili watoto.