Home Habari Godbless Lema: Natamani kukutana na Rais Magufuli

Godbless Lema: Natamani kukutana na Rais Magufuli

1171
0
SHARE

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

MBUNGE wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema akipata nafasi ya kuzungumza na Rais Dk. John Magufuli atamwelezea kuhusu udhaifu na hofu iliyojaa kwa viongozi aliowachagua.

Lema alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapa jana.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Lema alisema viongozi wengi walioteuliwa kumsaidia Rais Magufuli wamejaa hofu katika maeneo waliyopo.  

“Viongozi walioko madarakani wamejaa hofu kwa sababu ya mtu fulani na hofu iliyopo sasa italigawa taifa na si kujenga taifa.

Akizungumzia kuhusu deni lake ambalo  Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwahi kutangaza bungeni kuwa anadaiwa, Lema alisema hapakuwa na hoja ya kulitaja hadhani kwani wabunge wengi wamekopa na hawajawahi kutolewa taarifa zao hadharani.

Akielezea kuhusu maendeleo yaliyofanyika katika jimbo lake, alisema wamefanikiwa kujenga hospitali ya mama na mtoto, ujenzi wa barabara za lami ndani ya mji wa Arusha na miradi mingine mbalimbali.

Katika mkutano huo aliwaambia wananchi wasio na vitambulisho vya kupiga kura  ifikapo Julai 18 mwaka huu, wajitokeze kuandikishwa ili wapatiwe vitambulisho vyao.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Isaya Doita alisema  mwaka 2010 walikuta Halmashauri ya Jiji la Arusha wakitoa mikopo Sh milion 1.5  lakini kwa sasa wanatoa Sh milioni 5,”alisema