Home Habari Hakuna aijuae kesho yake

Hakuna aijuae kesho yake

717
0
SHARE

NA MITANDAO

Picha hii ni ya mwaka 2010, yaani miaka nane iliyopita. Wa tatu kwa waliokaa kutoka nyuma ni Mh. Kassim Majaliwa ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji. Majaliwa hakuwa hata mbunge wakati huo.

Nyuma ya Majaliwa ni Prof. Mark Mwandosya ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, asiye na Wizara Maalum. Na nyuma ya Mwandosya ni aliyekuwa Mbunge wa Rufiji, Prof Idris Mtulia (marehemu).

Katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, Mh.Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge na baada ya hapo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, akishughulika zaidi na upande wa elimu.

Miaka mitano iliyofuata Majaliwa akawa Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ukiangalia picha hii unapata jawabu kuwa hakuna ambaye alikuwa anawaza kama Majaliwa atakuwa Waziri Mkuu baada ya Mh. Mizengo Pinda.

Hapo Mh. Majaliwa alikuwa akionekana mwenye cheo kidogo tu, Mkuu wa Wilaya. Pichani anaonekana ni mtu mnyonge tu, mnyeneyekevu mbele ya wezake.

Fundisho kutoka picha hii, hakuna ajuaye kesho yake. Mungu anaujua mwisho wetu kabla ya mwanzo wetu. Usimdharau mtu kwani leo sio kesho. Fikiria fundisho lingine hapa ni mwendesha mtumbwi huu, yuko wapi? Kuna mtu anamkumbuka? Usalama wa viongozi wote hao ulikuwa mikononi mwake na walimuamini. Na walifika salama. Unapofanya kazi yako fanya kwa umakini bila kujali nafasi yako. Maisha ni siri nzito sana. Anayemfahamu mwendesha mtumbwi tafadhali ani DM.

#maisha #kazinikazi #mungukwanza #kesho

CR: Siasa Safi na IPMM