Home Makala HALI YA CHAKULA NCHINI HAIRIDHISHI- 1  

HALI YA CHAKULA NCHINI HAIRIDHISHI- 1  

684
0
SHARE

NA HAMISI DULLA


KILIMO ni moja ya sekta muhimu katika uchumi na maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa inatoa ajira kwa asilimia takribani 65 ya Watanzania na inachangia zaidi ya asilimia 80 ya chakula kinachopatikana nchini kwa miaka yenye mvua za kutosha.

Mara nyingi uwepo wa mvua za kutosha ni dalili ya uwepo wa mavuno mazuri hivyo mavuno mazuri hupelekea utoshelevu wa chakula.

Kutokana na ukweli kuwa kilimo kimekuwa kinachangia asilimia kubwa katika pato la Taifa, lakini hali ya chakula nchini kwa sasa siyo nzuri kabisa. Pamoja na kwamba Serikali imekuwa na vipaumbele mbalimbali katika kuendeleza shughuli za kilimo nchini lakini bado hizo jitihada hazijawa na manufaa katika upatikanai wa chakula cha kutosha hasa kwa wananch walio wengi.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini imekuwa ikitoa tahadhali juu kiwango cha mvua katika misimu ya 2016/2017, kiwango hiki kidogo cha mvua kimechangia kwa kiasi kikubwa cha upungufu wa chakula katika maeneo mengi nchini hasa maeneo yaanayotegemea mvua za vuli.

Kwa ujumla, hali ya uzalishaji, upatikanaji na uhakika wa chakula nchini imeendelea kuwa si ya kuridhisha katika maeneo mengi ya nchi kufuatia mavuno kutokuwa mazuri ya msimu vuli wa kilimo wa 2016 huku maeneo mengi yakishuhudia ukosefu mkubwa wa mvua.

 

CHANZO CHA UHABA WA MVUA

Mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa chanzo kikuu cha upungufu wa mvua na wakati mwingine kusababisha mvua kutonyesha kwa wakati. Upungufu huu wa mvua za kutosha kwa kiasi kikubwa huchangiwa sana na uharibifu wa mazingira ambapo uhaharibifu huu pia husababishwa na shughuli holela za kibinaamu kama kilimo kisicho kuwa na tija, makazi yasiyo na mpangilio, viwanda na migodi, shughuli hizi zote za kibinadamu zimekuwa zikichangia sana kaleta uharibifu wa vyanzo vya maji, uchafuzi wa hali ya hewa, ukataji ovyo wa miti na misitu mikubwa ambayo kwa namna moja au nyingine huchangia upatikanaji wa mvua na kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa.

 

HALI HALISI YA CHAKULA NCHINI

Kwa hali inavyoendelea kwa mwaka huu, inaonesha wazi kabisa Tanzania hatuna  chakula cha kutosha. Ripoti kutoka vyombo mbalimbali vya habari zinaonyesha kuwa karibu mikoa mingi ya Tanzania inakabiliwa na upungufu wa chakula hali ambayo inapelekea serkali na wadau katika sekta ya kilimo kutoa elimu na uhamasishaji juu ya umuhimu wa wananchi kutambua wa kutunza na kuhifadhi chakula kilichopo kwa usalama mkuu wa chakula na ili kuweza kuepuka upungufu wa chakula kwa kuwa hata miaka ambayo chakula kimekuwa cha kutosha bado kuna sehemu kubwa ya jamii imeendelea kukumbwa na balaa la njaa, ninachokiona mimi hapa ni kuwa sehemu kubwa ya jamii zetu hapa Tanzania hazina elimu ya kutosha jinsi ya kuweka hifadhi ya chakula hicho ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbinu hafifu za kilimo.

 

Maeneo mengi nchini chakula kimezidi kupanda bei kila siku kama inavyoonesha kwenye jedwali hapo chini.

ZAO BEI
Mahindi  16,000/= kwa debe la kilo 20 sawa na Tsh 800/= kwa kilo
Mtama 2,000/= kwa kilo
Mchele  1,600/= kwa kilo
Maharage 2,000/= kwa kilo

Chanzo ni kutoka katika masoko mengi ya vyakula mkoani Kilimanjaro- wilayani Same.

 

Wastani wa bei ya mazao katika soko la kimataifa la Kibaigwa tarehe 09/01/2017

ZAO BEI
Mahindi  830/= kwa kilo
Alizeti 760/= kwa kilo
Mtama mwekundu  400/= kwa kilo

Chanzo: ujumbe mfupi toka utawala wa soko la kimataifa la Kibaigwa