Home kitaifa Hii ndiyo historia ya Mto Ruaha

Hii ndiyo historia ya Mto Ruaha

2090
0
SHARE
Mto Ruaha

Na Mwandishi Wetu,

HAKIKA katika nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwa na mito yenye historia ya kusisimua. Lakini imekuwa jambo la kawaida kwa watu kuishi katika nchi yao bila kujua habariza vitu vinavyotuzunguka.

Ukweli ni kwamba kila kilichomzunguuka mwandamu kina historia yake. Wazee wa zamani walikuwa wakitambua kila kitu kilichokuwa kimewazunguuka.

Na walitoa majina ya vitu hivyo kwa kuangalia tabia, muoenekana na wakati mwingine uhusiano wa vitu hivyo na mwanadamu. Kwa ujumla tunapozungumzia habari za kabila la Wahehe itakuwa vigumu sana kuepuka historia ya mto Ruaha.

Kwa kurejelea ufafanuzi wa Padri Muso(1968) anafafanua kuwa Uhehe yenyewe yaenea hasa sehemu ya milimani kati ya mto Ruaha mkuu na Kilombero. Na kuna baadhi ya sehemu za uhehe zilipata kuenea maeneo ya mto Kizigo na Msombe.

Ukweli ni kwamba kabla ya ujio wa Wazungu hasa Wajerumani, hakukuwa na mto uliofahamika kwa jina la Ruaha. Kwani kabla ya hapo wenyeji walikuwa wakiita mito hiyo kwa lugha zao za kikabila.

Lakini wakati wazungu wanachora ramani zo kwenye miakia 1860/1870 walifanya makosa ya kiuandishi. Historia inafafanuliwa kuwa, hapo awali Wahehe walikuwa wasafiri hodari sana, kutokana na kusafiri huko, wahehe walipata ujuzi wa kutambua mambo mengi na kuyatofautisha.

Walifanikiwa kutofautisha mito iliyokuwa ikiwazunguuka. Hivyo walifanikiwa kutambua chanzo cha Mto Luvaha (Ruaha) kuwa ni mto Livindi Lya Mbangali.

Livindi Lya Mangali ulikuwa mto ambao ulitokea maeneo ya Ubena. Huu Ndio ulikuwa mto mrefu ambao ndio ulionekana kuwa mkubwa zaidi. Na kutokana na mto huo kuwa mkubwa ndipo walipouita Lya Mbangali ikiwa na maana yam to mrefu na mkubwa zaidi kuliko mingine. Na ndio baadae wazungu walipouita kuwa Mto Ruaha Mkuu.

Na mara baada ya kuupa jina mto huo kwa jina la Lya Mbangali(Ruaha Mkuu) walipata kutambua mito yote ambayo iliyokuwa imeungana na kuingia kwenye mto Lya Mbangali(Ruaha Mkuu).

Kwa kipindi hiko katika kabila la Wahehe kulikuwa na Baraza la wazee. Sasa wale wazee wanaounda lile baraza walifahamika kwa jina la Wamuvaha. Kila Muvaha mmoja ailikuwa na umuhimu kwa mtemi au kiongozi wa kabila hilo.

Kutokana na kazi za Muvaha katika baraza la wazee , Wahehe walifananisha mito ile na baraza la wazee, ambayo inaungana na kuunda Lya Mbangali (Ruaha Mkuu).

Ndipo waliamua kuita mito hiyo Luvaha. Kwa mantiki kiwamba wale wazee kwenye baraza waliungana pamoja na kufanikisha kazi moja iliyokuwa ikifanywa na Mtemi.

Hivyo mtemi alipata nguvu kutokana na wazee hao. Na huo ndio ukawa mwanzo wa mito hiyo kuitwa Luvaha midogo na Luvaha Mkubwa.

Sasa mambo yalikuja kuharibika pale wazungu walipowauliza wazawa kuwa mito hii inaitwaje, na wazawa kujibu Luvaha.

Na kwa kuwa wazungu hawakujua vizuri kutamka lugha hiyo, wakajikuta wakitamka Ruaha. Na kupata mito miwili yaani Ruaha Mkuu (Great Ruaha) na Ruaha Mdogo (Little Ruaha). Na mpaka leo mito hii inafahamika kwa majina hayo. Hiyo ndiyo historia fupi ya Mito hii.