Home Makala Historia ya Krismasi na namna yake kwa Wakristo

Historia ya Krismasi na namna yake kwa Wakristo

575
0
SHARE

VICTOR MAKINDA NA MITANDAO

Krismasi ni sikukuu inayoadhimishwa Desemba 25 ya kila mwaka na hutambulika kama kipindi maalumu cha mapumziko ya kidini na jambo la kitamaduni na biashara kote ulimwenguni. 

Kwa zaidi ya milenia mbili, watu ulimwenguni kote wamekuwa wakiitazama siku hii kwa mila na mazoea ambayo ni ya kidini na ya kidunia. 

Wakristo husherehekea siku ya Krismasi kama kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo wa Nazareti, kiongozi wa kiroho ambaye mafundisho yake ndiyo msingi wa dini yao. 

Hii ni sikukuu inayifanyika katika ya mwaka wa Liturjia Sikukuu ya katikati ya mwaka wa Kiliturujia wa kiliturujia. Wakristo huadhimisha siku hii kwa heshima ya Bwana Yesu Kristo lengo la waamini likiwa ni kumtukuza Mungu kila siku, pamoja na Disemba 25.

Utamaduni maarufu katika kusherehekea sikukuu hii ni pamoja na kubadilishana zawadi, kupamba miti ya Krismasi, kuhudhuria kanisani, kushiriki chakula na familia na marafiki na kungojea Santa Claus afike. 

Katika nchi zilizoendelea shamrashamra zake huaza tangu Novemba ambapo maduka, nyumba, ofisi na mitaani hupambwa na kuanza kuuzwa kwa vitu vinavyohusiana na sikukuu hii. 

Desemba 25 siku ya Krismasi ilikuwa ni likizo ya shirikisho huko Marekani tangu miaka ya 1870.

Baadhi ya vyao vinaeleza kuwa mwanzoni mwa ukristo Pasaka ndiyo ilikuwa sikukuu kubwa wakati huo kuzaliwa kwa Yesu Kristo hakukuwa kukisherehekewa. Katika karne ya nne viongozi wa kanisa wakaamua kuanzisha sikukuu ya kuzaliwa YESU Kristo. hataIn the fourth century, church officials decided to institute the birth of Jesus as a holiday. 

Kwa bahati mbaya Biblia haikuwa imetaja tarehe ya kuzaliwa kwake inagwa baadhi ya ushahidi unaonesha alizaliwa wakati katika chemchem 

Inaaminika kuwa kanisa hilo lilichagua tarehe hii ili kuendana na utamaduni wa tamasha la kipagani la Saturnalia. Kwanza iliitwa sikukuu ya Kuzaliwa, na ilienea hadi Misri katika miaka ya 432 na kisha Uingereza mwishoni mwa karne ya sita.

Mwishoni mwa karne ya nane, maadhimisho ya Krismasi yalikuwa yameenea zaidi katika nchi za Scandinavia. 

Kwa sasa katika makanisa ya Kigiriki na Urusi sikukuu hii husherehekewa siku 13 hadi 14 baada ya 25. Hii ni kwa sababu makanisa ya Magharibi hutumia Kalenda ya Gregori, wakati Makanisa ya Mashariki hutumia Kalenda ya Julius, ambayo ni siku 13 hadi 14 nyuma ya Kalenda ya Gregori. Makanisa yote ya Magharibi na Mashariki husherehekea Epiphany au Siku ya wafalme watatu siku 12 baada ya Krismasi yao wenyewe. Hii ndio siku ambayo inaaminika kwamba wale watu watatu wenye busara walimpata Yesu ndani ya zizi.

Kuifanya Krismasi wakati huohuo kama sherehe za jadi za msimu wa baridi, viongozi wa kanisa waliongezea nafasi ambayo Krismasi ingependeza zaidi lakini waliacha uwezo wa kuamuru jinsi iliadhimishwa. 

Kufikia zama za Kati Ukristo kwa sehemu kubwa ulibadilisha dini ya kipagani. Siku ya Krismasi waumini walienda kanisani kisha kusherehea furaha katika hali ya ulevi. Kila mwaka mwombaji au mwanafunzi alipewa taji la “bwana wa makosa” na washiriki kwa shauku walishiriki sehemu ya masomo yake. 

Maskini walikwenda kwenye nyumba za matajiri na kuomba chakula bora na vinywaji. Ikiwa wamiliki walishindwa kufuata, wageni wao wangeweza kuwatisha kwa kujihusisha na ufisadi.

Krismasi ikawa wakati wa mwaka ambapo watu wa kipato cha juu wangeweza kujitolea sehemy halisi au ya kufikirika ya mapato yao kuburudisha raia maskini.

Mwanzoni mwa karne ya 17, wimbi la mabadiliko ya kidini lilibadilisha mfumo wa usherehekeaji wa Krismasi iliyoadhimishwa huko Ulaya. Wakati Oliver Cromwell na vikosi vyake vya Wapuritan walipoitwaa Uingereza mwaka1645, waliapa kuiondoa England katika uozo na kupitia mipango yao waliifuta Krismasi. 

Lakini kutokana na mahitaji ya wengi Charles II alirudishiwa kiti cha enzi na kurejeshwa kwa likizo maarufu ya msimu wa baridi.

Historia pia inaonesha kuwa katika karne mbili za mwanzo tangu kuzaliwa kwa Yesu, hapo ulipoanza ukristo, watu wengi hawakusherehekea siku za kuzaliwa wala kufa si tu kwa wafia imani au hata ya Yesu mwenyewe. 

Wakristo waliona kusherehekea siku ya kuzaliwa ni mazoea ya kipagani jambo linalopaswa kuepukwa, licha ya misimamo ya wakristo wa nyakati hizo ya kupinga mazoea ya kusheherekea siku ya kuzaliwa, kanisa Katoriki ndilo lilianza kusheherekea Chrismas katika karne ya nne. 

Kipindi hicho kanisa lilitaka kujiimarisha na kupunguza umaarufu wa sikuu za dini za kipagani za Roma ambazo zilikuwa zinafanyika katika msimu wa baridi, jua linapokuwa upande wa kasikazini wa Dunia kila mwaka, kuanzia December 17 mpaka Januali 1.

Waroma wengi walisherehekea pamoja, walicheza, walishiriki katika matamasha, magwaride, na sherehe nyingine walizokuwa wakiabudu miiungu yao. 

Kitabu cha Chrismas America kilichoandikwa na Penne L. Restand kinasema ilipofika Disemba 25 Waroma walisherehekea kuzaliwa kwa jua lisiloweza kushindwa, hivyo ilibidi kanisa kuwa na ushawishi mkubwa wa kuwashawishi Waroma kugeuza siku hiyo ya kuzaliwa jua iwe ni siku ya kuzaliwa Yesu na ilifanyika ili kuondoa ibada za kipagani japo Waroma waliweza kufurahia michezo yote waliyokuwa wakifanya katika msimu wa baridi.

Kitabu cha Santa Claus a Biography kilichoandikwa na Gerry Bowler kinaeleza bayana kuwa Waroma waliendelea kusherehekea sikuu hiyo mpya kama walivyozoea kufanya zamani.

Taa za Krismasi, inaelezwa kuwa wazungu walirembesha nyumba zao kwa “taa na mimea ya kijani-kibichi ya kila aina” ili kusherehekea majira ya baridi kali na ili kuwazuia roho waovu.

Mti wa mlimbo, mholi, Kwa kawaida mimea hiyo hutumiwa kama mapambo wakati wa Krismasi na utajwa kuwa ulikuwa na nguvu za kimuujiza, mmea ambao haunyauki, uliabudiwa kama ahadi ya kurudi kwa jua wakati wa sherehe za msimu wa baridi.

Mti wa Krismasi, kuabudu miti lilikuwa jambo la kawaida miongoni mwa wapagani wa Ulaya na waliendelea na waliendelea kufanya hivyo hata baada ya kuwa Wakristo utamaduni ambao umedumu hadi sasa ambapo Wakristo kote duniani wameendelea kupamba nyumba zao kwa kutumia miti hiyo wakati wa sikukuu ya Krismasi.