Home Latest News HISTORIA YA MADHEHEBU NA SIASA TANZANIA

HISTORIA YA MADHEHEBU NA SIASA TANZANIA

6117
0
SHARE

GERARD M. CHUCHUBA                |                     


Ni kweli Tanganyika na sasa Tanzania ilipata kuwa na vyama zaidi ya kimoja – TANU. Vilikuwapo ANC na UTP na kingine AMNUT cha kiislamu. Baada ya Mwalimu Nyerere – Baba wa Taifa, kuiangalia hali ya nchi, kwa busara na hekima aliyokuwa amejaliwa, akaeleza na kufafanua na kuuthibitishia umma wa watanganyika kwamba kuwa na vyama vingi vya siasa si sawa bali kimoja tu alichoikuwa akikiongoza yeye – TANU.

Mwaka 1992, kwa shinikizo lake yeye mwenyewe, katiba ya Tanzania ilitamka kwamba sasa ni nchi ya vyama vingi – Katiba ibara ya 3(1). Ibara hii ilitamka pia kuwa Tanzania ni nchi ya Kijamaa!

Madhehebu:- kamusi ya Kiswahili inasema: “ni kikundi cha dini fulani chenye mwelekeo tofauti na kikundi kingine cha dini hiyohiyo”

Dini nyingi, kama si zote zina madhehebu. Dini ya kikristo imefahamika sana kwa kuwa na madhehebu mengi.mwaka 2016 nilifahamishwa kuwa mkoa wa Mbeya peke yake ulikuwa una madhehebu ya kikristo yasiyopungua 70!

Dini ikidumu katika misingi yake sahihi, hakuwezi kukawapo madhehebu.

Ukristo, kama ilivyotokea kwa CCM, haukudumu katika misingi yake kama ilivyo bayana katika agano jipya.katiba ya nchi Tanzania na katiba ya ccm zinasema kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa.maisha Tanzania siya wa jamaa wanaojitegemea

Agano jipya linaposema njia ya kumfikisha mkristo mbinguni kwa Mungu Baba ni kristo peke yake (Yohana 14:6) kanisa katoliki, liliuacha ukweli huu ili kuwapendeza viongozi wa Dora la Kirumi liache kulitesa likaongeza kuwa Mama wa Yesu naye ni mlango wa Mbingu. Watakatifu (marehemu) nao wakapewa hadhi ya kuwaombea wakristu.

Papa naye akawa na uwezo wa kuuza “Indulgences” neema ya kumwondolea mtu adhabu ya dhambi zake mbele ya Mungu. Badala ya kanisa kuwa la kristo kama Agano Jipya linavyosema (Mtd 2:36, Efeso 1:22), Papa akawa ndiye kichwa cha Kanisa la Roma. Kanisa la kristo likaondolewa.

Walioupinga utaratibu huu waliitwa waasi – “heretics” wakauawa, wakachomwa na majivu yao yakatupwa katika mto Tiberius upitao kati ya mji wa Rumi. Mifano ya waliotendwa hivyo; Arnord of Brescia aliuawa kwa amri ya Papa Hadrian IV, akachomwa na majivu yake yakatupwa Mto Tiberius, (F.W. Mattox Harding College Searcy, Akansas, Uk 210).

Mwingine alikuwa Peter of Bruys alinyongwa 1130, kosa lake yeye na wafuasi wake walikula nyama Ijumaa Kuu na alipinga amri ya kuwakataza Mapadri kuoa.

Martin Luther, Padri, alipinga ufisadi wa Papa Leo X wa kuuza “Indulgences” – neema huko Ujerumani (F.W Mattox Uk 239-253). Wapinzani wa Papa nao hawakuona mbali. Walitaka waliunde upya Kanisa – “reform”.

Reformation, halikuwa neno sahihi katika mazingira haya. Neno sahihi ni “Restoration”. Kanisa lirudishwe katika misingi yake sahihi ya Agano Jipya – si vinginevyo.

CCM nayo ilifanya makosa yayo hayo. Iliacha msingi wake kama ulivyo katika Katiba ya nchi na chama chenyewe kulingana na Imani na madhumuni yake – ibara ya 4(1-3), ibara ya 5(3).

Kwa kulinyongelea mbali Azimio la Arusha na kulizika katika mchanga wa Zanzibar, CCM ilihimiza kuwapo kwa vyama vingine vya siasa kwa kufuata mkumbo eti Opposition Parties – kwa kuwa wazungu wanasema, tukaviita vyama vya upinzani badala ya vyama vya “ukosoaji”! wazungu wazungu wanatunanga, ukitaka wanatusi – nkula; “yaone tuliwaambia”, “An African can never grow beyond Childhood!”mwafrika haachi utoto

Waacheni wafanye yao na sisi tufanye yetu kulingana na utamaduni wetu na ngazi ya maendeleo tuliyoifikia na ile tunayoichuchumilia.

Nimekemea  matumizi ya neno “Reformation” nikapendekeza neno “Restoration” yaani tusiunde upya bali tuirudie misingi sahihi ya Ujamaa na Kujitegemea tukiongozwa na Katiba ya Nchi na Azimio la Arusha.

ACT-Wazalendo wakiwa Tabora mnamo mwezi Juni 2015; wameonesha uelewa wao wa kile kinachotakiwa Tanzania kuwa si “reformation” kuunda upya bali ni “restoration” kuirudisha nchi katika misingi sahihi iliyowekwa enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Maneno yaliyokusudiwa kuonekana kwanza katika kitabu kidogo walichokiita Azimio la Tabora juu ya siasa ya Ujamaa wa Kidemocrasia yamewekwa mwanzoni kabisa hivi

NDOTO YETU YA TANZANIA

Taifa lenye kujitegemea kiuchumi na kitamaduni, na ambalo linalinda na kudumisha usawa, ustawi wa jamii, uwajibikaji, democrasia na uongozi bora.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Anna Mghwira katika dibaji akaweka wazi jinsi wanavyoona mbali akasema, ACT-Wazalendo tunaamini kuwa taifa letu linahitaji kurejea katika misingi mama iliyojenga taifa hili, ikiwemo misingi ya umoja, udugu,uzalendo,uadilifu na uwajibikaji wa viongozi na taasisi za umma. Hivyo basi Azimio hili la Tabora linalenga kuhuisha misingi….. hayo yalitamkwa mwezi juni 2015.

Kiongozi, si mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, akihutubia katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam tarehe 29.03.2015 aliongea chini ya kichwa cha habari, “ Turejeshe nchi yetu Tanzania”! kirejeshwacho ni kilichochukuliwa kwa makubaliano ya kukirejesha au kilichoporwa kwa nguvu pasipo hiari ya mmiliki….. je, nchi yetu iko wapi?.

Haya ni mawazo sahihi, ni malengo sahihi watanzania tusipoyatekeleza, watanzania, sisemi chama, ashakum si matusi, watoto wetu miaka ijayo watatabawali juu ya makaburi yetu.

Mwalimu Nyerere alipoona CCM imekuwa madhehebu alitushinikiza watanzania wote turuhusu uwepo wa madhehebu ya siasa-vyama vingi akitamani kitokee chama  kimojawapo kiweze kuiweka pembeni CCM katika uchaguzi huru, wawazi-haijatokea Rais aliyepo amewakatalia hawataiondoa CCM. Nami nakubaliana naye, kwa utitili wa madhehebu ya Siasa, hiyo ni ndoto!

Ushauri kama kuna Azimio la Tabora la ACT – Wazalendo kitafute kijitabu hicho bila kujali chama bali uzalendo kwa nchi yako. Achana na mageuzi, tuirudie misingi yetu sahihi tuliyoiacha kwa kujua au bila kujua.

Tafadhali zingatia

0768 462511