Home Latest News HUU NDIYO UMAHIRI WA ARCHIMEDES

HUU NDIYO UMAHIRI WA ARCHIMEDES

6596
0
SHARE

NA KIZITO MPANGALA


HISTORI mbalimbali za nchi ya Uyunani (Ugiriki), ina mshawasha sana ukiifuatlia kwa karibu zaidi. Yohane alitumbukizwa kwenye pipa la mafuta yanaoyochemka, lakini hakuugua, au hakuiva kama iivavyo nyama ipikwapo jikoni.

Naam, sasa ni umahiri wa Mzee Archimedes, rafiki wa wakaribu wa Luca Paciolo, mwanahisabati aliyewavutia mabepari wa Venice. Mambo ya kale ambayo yanatoa mafunzo mbali mbali ukitafakari zaidi.

Archimedes alizaliwa mwaka 287 katika Mji wa Siracusa, kwenye Kisiwa cha Sicilia (sasa ni sehemu ya nchi ya Italia), wakati ule kisiwa hiki kilitawaliwa na Wagiriki, kabla ya kuzaliwa Mwalimu Emmanuel Joseph Masiha bin Daudi, yaani Yesu Kristo aliyekuwa “Mbunge” wa jimbo la Nazereti, “Iesus Nazarenum Rex Iudeum” (INRI). Archimeds alikuwa mtaalamu wa Uyunani (Ugiriki) ya kale (Ancient Greece). Alikuwa mwanahisabati, mnajimu, na pia mvumbuzi wa vifaa mbali mbali ambavyo vimekuwa vielelezo vya teknolojia kwa sasa. Kwa mfano, visima vinavyotumia pampu ya kusukuma na mkono. Baba yake pia alikuwa mnajimu.

Archimedes alipofikia umri wa miaka 10, alikwenda masomoni mjini Alekzandria nchini Misri. Mji wa Alekzandria ulikuwa kitovu kikuu cha elimu ya Kiyunani (Kigiriki), pamoja na maktaba yake maarufu mbayo sasa ni maktaba ya kihistoria nchini Misri.

Katika maktaba hiyo, ndiko ilikochimbuka namba ya usajili wa vitabu yaani ISBN (Internatinal Serial Book Number). Archimedes alipenda sana hisabati na fizikia. Alifanikiwa kutumia na kuunda nadharia nyingi na kuziweka katika vitendo halisi.

Kwa mfano Wenzo, pampu ya maji, na pia alijenga ukuta mkubwa uliozuia wanajeshi wa Italia kuingia katika kisiwa cha Sicilia.
Anafikiriwa kuwa mtu wa kwanza kuelewa na kutumia kanuni ya wenzo, ambapo katika wenzo huo ndipo misingi ya umakanika ilipozaliwa. Aliwahi kusema kwamba akipatiwa mtambo mrefu na aandaliwe mahali pa kusimama, angeweza kuisukuma dunia hii kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine aliyopendelea yeye.

Kituko ambacho watu wengi wa wakati ule wangekuwepo hadi sasa wanachokikumbuka, ni pale Archimedes alivyovumbua kanuni ya ueleaji na kukurupuka kutoka maliwatoni (bafuni) akiwa uchi na kuingia barabarani, huku akitangaza kwa sauti kubwa mtaani akisema “Eureka..eureka..eureka” yaani “nimegundua..ninegundua..nimegundua.”

Hapo ndipo alipojishughulisha na uundaji wa merikebu. Merikebu ni meli za kale zilizoundwa kwa mbao na zilitumika na wasafiri mbali mbali baharini. Ndipo mabaharia walipoanzia. Merikebu hizo ndizo zikawa kielelezo kikuu cha uundaji wa meli za kisasa ambazo zina mengi ndani yake. Kwa msaada wa kanuni za Jiometri za mwanahisabati Leonard Euler, meli za kisasa zinaundwa kwa kufuata Jiometri, hapa ndipo umuhimu wa hisabati ulipo, na maeno mengine.

Archimedes hakupenda kubaki na nadharia bila kuifanyia majaribio. Nadharia zake nyingi alizifanyia majaribio na kutoa matokeo mazuri.

Kwa mfano, skurubu ya Archimedes ambayo aliitumia kuchotea maji kutoka sehemu ya mbali. Skrubu hiyo kwa sasa imeundwa kisasa zaidi, lakini msingi wake ulibuniwa na Archimedes. Aghalabu hutumiaka katika kazi ya kutoa maji ndani ya meli na pia katika umwagiliaji.
Archimedes alikuwa pia muundaji wa silaha aina aina za kivita. Alihamasika kuunda silaha za kivita wakati wa vita ya mwaka 214 hadi mwaka 212 kati ya Warumi na Wasiracusa. Kati ya silaha alizotengeneza ni pamoja na:

1. Vioo vya parabola (parabolic mirror) ambavyo vilikuwa na nguvu kubwa ya kukusanya mionzi ya jua na kuipindisha kwenda kwenye meli za Warumi. Mionzi hiyo ikikusanywa mingi huweza kuunguza kitu chochote kianchoshika moto kwa urahisi. Katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia, vioo vya parabora vinatumika kama jiko la mionzi ya jua ambapo unaweza kupika chakula chochote.

2. Winchi kubwa zilizoweza kuinua na kuangusha meli/manowari za Warumi zilizokaribia ukuta wa bandari ya Siracusa kwa kuwa zilitegwa ukutani. Kwa sasa winchi hizo zimeongezewa matumizi na kuwa za mitindo mbali mbali, kuna winchi za kupakua na kupakia mizigo hasa bandarini, kuna katapila linalojulikana kama kijiko, kuna winch zinazotumika katika ujenzi wa majengo marefu na kadhalika. Yote hayo msingi wake ni Archimedes.

3. Mzinga mkubwa (catapult) wa kufyatulia mawe ambayo yalikwenda moja kwa moja kuzigonga manowali za Warumi.

Kumbuka kuwa zamani hapakuwa na mizinga ya kivita kama hii ya sasa na pia hapakuwa na mabomu, vita lipiganwa ana kwa ana kwa usafiri wa manowari za mbao na farasi.

Mzinga ulioundwa na Archmedes, mabomu yake yalikuwa ni mawe makubwa ambayo yakifyatuliwa yakwenda umbali mrefu, na hii iliondoa utegemezi wa kukutana na adui ana kwa ana, yaani hii ni kama sasa isemwavyo mabomu ya masafa marefu yanayoundwa Korea Kaskazini.

Hata vivyo wanajeshi Wakirumi walifanikiwa kuvuka kuta za maji zilizowazuia kupenya kirahisi na kuingia katika ardhi ya Siracusa.

Ingawa walipata taabu sana, Warumi walimsaka Archimedes na kumkuta nyumbani kwake akitafakari kanuni za hisabati kwa kuchora duara kwenye mchanga (wakati ule makaratasi yalikuwa adimu sana). Wanajeshi wa Rumi walipoingia nyumbani mwake, Archimedes aliwazuia wasiuuvuruge mchoro aliouchora kwenye mchanga, alikuwa tayari kufa, lakini si kupoteza mchoro wake.

Hapo akiwa kwenye vurumai ya kuulinda mchoro wake mwanajeshi mmoja mwenye hasira, alimua Archimedes.

Kazi zake zinaheshimwa hadi sasa, na ni kimoja wapo cha maendeleo ya Sayansi na Teknoloji yakiwemo katika Umakanika. Ajabu ilioje, Archimedes hakuwa na cheti chochote, wala diploma, wala digri ya kwanza, wala ya uzamili wala uzamivu yoyote.

Morali, bidii, na mapenzi yake ndivyo vilimuweka katika nafasi hiyo muhimu. Lakini kujisomea ni jambo jema sana. Nadharia za Archimedes zimo kwenye vitabu mbali mbali, hivyo kujisomea vitabu ni muhimu.

Huko mwezini kuna Kreta iliyopewa jina la Archimedes (29.7° N, 4.0° W) kwa heshima yake. Pia mwezini huko huko, sehemu yenye safu ya vilima inaitwa Montes Archimedes (25.3° N, 4.6° W). Medali za nishani za hisabati zimewekwa chapa ya sura ya Archimedes pamoja na tufe. Medali hizo zimeadnikwa kwa Kilatini: “Transire suum pectus mundoque potiri” yaani “Ibuka/jitokeze moingoni mwa watu dunia ikujue.” Nchi ya Ujerumani Magharibi (zamani) stempu zake ziliwekwa chapa ya Archimedes, pamoja nayo ni nchi za Ugiriki, Italia, Hispania na Nicaragua.

Tanzania inaweza kuwajali wabunifu mbali mbali, lakini wabunifu hao nao wasihamaki kutika mambo makubwa ndani ya muda mfupi. Archimedes anasomwa katika ngazi mbali mbali za elimu, hivyo ni vema pia kujua historia yake, japo kwa ufupi, ili kuongeza hamasa, lakini hamasa zisizo na dokezo la mambo ya hela moja kwa moja wengi hawazipendi, hiyo si tabia njema.

Wanafunzi waweke bidii na kujifunza kwa uhakisia, ili wafaidike na kuifaidisha nchi yao. Tanzania ni yetu sote, licha ya changamoto mbali mbali ziwazo, hivyo, tulekeezane, tuheshimiane, tupendane.