Home Latest News Ijue Bodi ya Parole na majukumu yake

Ijue Bodi ya Parole na majukumu yake

3030
0
SHARE
BXP06Y Hands on prison bars

Na Lucas Mboje – Jeshi la Magereza

Wiki iliyopita tulijadili kwa undani uanzishwaji, kazi na majukumu ya bodi ya Parole nchini. Wiki hii tunaendelea na maeneo muhimu yanayohusiana na bodi hiyo. Endelea..

BAADA ya maamuzi ya mwisho kutolewa na  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, wafungwa waliokataliwa kunufaika na Parole huendelea kutumikia vifungo vyao, wale waliokubaliwa taarifa zao hutumwa katika magereza husika ili utaratibu wa kuwaachilia kwa Parole ufanyike.

Kila mmoja hupewa kitambulisho (certificate) kitakachomtambulisha wakati wote akiwa kwenye Parole. Afisa Parole humpeleka mfungwa husika na kumkabidhi kwenye Uongozi wa Serikali ya mtaa/kijiji kwa ajili ya ufuatiliaji wa tabia na mwenendo wa maisha yake ya kila siku.

Uongozi wa kijiji/mtaa humteua mtu mmoja anayeheshimika katika jamii kuwa msimamizi wa mfungwa wa Parole, mfungwa wa Parole hutakiwa kutoa taarifa kwake kama atakavyokuwa amepangiwa. Afisa Parole kutoka katika gereza lililokaribu hutakiwa kumtembelea mfungwa husika kila mwezi na kuwasilisha taarifa kwenye Ofisi ya Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole kwa ufuatiliaji.

Mfungwa wa Parole wakati wote wa Parole anatakiwa kufuata masharti aliyopewa na kutii Sheria za nchi na kuishi kwa amani wakati wote kama Sheria ya Bodi za Parole na Kanuni.  Masharti hayo yameainishwa sehemu ya 3 kanuni ya 5(5) (a-h).

Aidha, inapotokea amevunja masharti ya Parole au kufanya uhalifu taarifa zake hupelekwa kituo cha Polisi na mfungwa hujulishwa kuhusu kusudio la kutengua Parole yake na ikithibitika tuhuma zilizotolewa dhidi yake ni za kweli hurudishwa gerezani na kufunguliwa mashtaka mapya na kupelekwa mahakamani kwa kosa hilo, ikithibitika kweli amevunja masharti Mahakama ndiyo yenye uwezo wa kutengua Parole baada ya kumsikiliza kwa mujibu wa Kanuni ya Sheria ya Bodi za Parole za mwaka 1997 sehemu ya 5, 9(a-d) na Kanuni ya 10  (1-2).

Hata hivyo, Mahakama inao uwezo kutengua Parole kwa mfungwa yeyote na kuamuru arudishwe gerezani kama ikithibitika kwamba mosi, amevunja sharti lolote la Parole, pili, baada ya kupata maombi kwa maandishi toka kwa Mhe. Waziri kwa maslahi ya Taifa kwa mujibu wa  Kanuni ya Sheria ya Bodi za Parole sehemu ya 5, 10(3) (a-c) na tatu ni kama mfungwa husika atafanya uhalifu akiwa kwenye utaratibu wa Parole.

 MAFANIKIO  YA PAROLE

Itaendelea wiki ijayo….