Absalom Kibanda aliteswa na kuumizwa na watu wasiojulikana. Mpaka leo hawajajulikana.
Ben Saanane amepotezwa na watu wasiojulikana.
Ofisi za Wakili Omar Said Shaaban Zanzibar zililipuliwa na watu wasiojulikana, mpaka Leo hawajajulikana.
Ofisi za Uwakili za IMMMA Advocates Dar Es Salaam zililipuliwa na watu wasiojulikana. Mpaka leo hawajajulikana
Mwanaharakati dhidi ya Ujangili Bwana Lotter aliuawa Dar Es Salaam na watu wasiojulikana. Mpaka leo hawajajulikana
Mbunge Tundu Lissu amepigwa risasi 32 mchana kweupe mjini Dodoma Bunge likiendelea. Waliompiga risasi ni watu wasiojulikana. Watu wasiojulikana wanasakwa na Polisi.
Huu si Utanzania. Tukatae kuwa Jamhuri ya Muungano wa Watu Wasiojulikana
Zitto Kabwe