Home Makala JOYCE BANDA ATUMIA SALAMU ZA MWAKA MPYA KUMSHAMBULIA MUTHARIKA

JOYCE BANDA ATUMIA SALAMU ZA MWAKA MPYA KUMSHAMBULIA MUTHARIKA

1076
0
SHARE

LILONGWE, MALAWI


Rais wa zamani wa Malawi Joyce Banda ametumia salamu zake za mwaka mpya kuishambulia serikali ya hasimu wake kisiasa Peter Mutharika. Bi. Banda amebainisha kuwa, serikali hiyo imegota katika kupambana na ufisadi na kwamba alitegemea ingefanya vema kuliko yeye lakini hali imekuwa vinginevyo.

Katika salamu zake za mwaka mpya alizozitoa kwa njia ya maandishi na kunukuliwa na gazeti la Nyasa Times la nchini huyo, rais huyo alisema Malawi inahitaji umoja wa kitaifa ambao utavuka mipaka ya vyama vya siasa, dini na makabila ili kurejea katika maendeleeo ya kweli.

“Tuko wote katika meli hii na kama itazama tutazama wote kama Malawi. Na tunaposonga mbele tujifunze kuheshimu kazi zilizofanywa na serikali zilizopita,” alisema Rais huyo aliyebwagwa katika uchaguzi na rais wa sasa.

Rais huyo alisema, licha ya aina ya ukandamizaji aliyokuwa nayo Rais wa zamani Dkt. Kamuzu Banda, lakini alikuwa na mchango mkubwa wa kuvunja muungano wa kikoloni chini ya Rhodesia na Nyasaland jambo lililosaidia sana katika suala la kupatikana kwa uhuru mwaka 1964.

Kamuzu Banda aliisaidia Malwi katika mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii na alifanikiwa kuijenga Malawi hasa katika Miundombinu, mabadiliko ya elimu, hospitali na kilimo cha kibiashara.

Aliongezea kuwa Rais Banda alihakikisha kuwa wananchi wake wanapayta ukakika wa mlo, mavazi na malazi.

“Kipindi cha Rais Bakili Muluzi nchi hiyo ilifanikiwa kujenga mfumo wa kiutawala na utawala wa kisheria. Ni katika kipindi hiki ambapo tume ya kukabiliana na rushwa ilianzishwa ikiwa ni pamoja na kuifanya mahakama kujitegemea. Anatakiwa kuheshimika kwa kukuza demokrasia nchini pamoja na kuhakikisha inakua,” alisema.

“Hayati Rais Profesa Bingu wa Mutharika alikwenda hadi benki ya dunia kuhakikisha Malawi inasaidiwa katika kuwa na mfumo wa serikali kuchangia uzalishaji. Kutokana na program hii Malawi ilifikia kiwango cha juu kabisa katika usalama wa chakula kuliko ilivyokuwa hapo nyuma,” anasema rais huyo.

Rais huyo za zamani akaendelea kusema kuwa, wananchi wan chi hiyo ni waamuzi wazuri na wao ndio wanaoweza kuzungumzia utawala wa sasa wa Rais Peter Mutharika.

“Ninachokifahamu ni kuwa wachunguzi wa masuala mbalimbali duniani wameiweka Malawi miongoni mwa nchi maskini kabisa tangu historia ya nchi hiyo baada ya uhuru,” anasema.

Kwa mujibu wa rais huyo, Malawi inahitaji kukubali ukweli na kujifunza kupitia awamu zilizopita. Kama haitafanyika hivyo basi hali ya kutafuta namna bora ya kurejesha mambo itakuwa ngumu.

“Mafanikio yaliyofanywa na tawala zilizopita yanabakia kuwa somo la kujifunza na tukiyatumia yanaweza kujenga matarajio kuwa mafanikio yanawezekana na hasa wakati viongozi wetu wanapokuwa wakitunga sera na miradi ambayo haikuweza kufanyika huko nyuma,” anafafanua na kuongeza kuwa serikali ya sasa imeshindwa kuwa makini katika kukabiliana na ufisadi na kwamba imeshindwa kuendelea na vita hiyo hasa pale alipoishia yeye.

Anasema kuwa, Septemba 2013 Kiongozi wa Umoja wa Ulaya Balozi Alexander Baum alimueleza kuhusu wasiwasi wake kutokana na fununu za kuwapo ufisadi katika mfumo wa serikali na kwamba mfumo huo ulikuwa na mianya mingi ya wizi wa fedha za umma. “Nilitangaza katika konferensi ya ECAM Septemba 7 mwaka huo kuwa serikali yangu inafanyia kazi suala la kufumua mfumo wa IFMIS na kuonesha nia yanbu ya kuhakikisha kuwa fedha ya wananchi inabaki salama na hailiwi na mtu yoyote. Sikuishia hapo nilitangaza kuwa wahusika wote nitakaowabaini nitawawajibisha,” anasema.