Home Michezo JPM aiongoza Taifa Stars kwenda Afcon

JPM aiongoza Taifa Stars kwenda Afcon

3302
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU

KWA lugha sahihi unaweza kusema Tanzania kama taifa sasa  wameamua kwenda kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ‘Afcon’hapo mwakani.

Kwa sasa si Rais, Waziri mwenye dhamana na michezo, taasisi za kimichezo, mashabiki au wadau wa mchezo huo wote kwa pamoja wameungana na kudhamiria kuifanya rahisi safari ya timu hiyo kuelekea fainali zijazo za Afcon.

Si kazi rahisi kutokana na ukweli kuwa kila timu au nchi ingependa kushiriki fainali hizo zinazotarajiwa kufanyika nchini Cameroon kwa kushirikisha mataifa 24 badala ya 16 zilizokuwa hapo awali.

Tanzania imekuwa katika harakati za kutafuta kushiriki fainali hizo kwa takribani miaka 38 sasa bila mafanikio. Ilishiriki kwa mara ya kwanza na mwisho mwaka 1980 na kutolewa katika za awali kwa kushika mkia katika kundi lake.

Wiki iliyopita Rais John Magufuli aliwaalika wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Timu ya Soka ya Taifa ‘Taifa Stars’ kula nao chakula cha mchana ikiwa ni kutaka kuwapongeza pamoja na kuwapa nasaha zake katika vita yao ya kuwania kufuzu fainali zijazo za Afcon.

Hakika ilikuwa ni siku nzuri na njema kwa wachezaji wa na viongozi wa Taifa Stars kwani mbali na kupokea nasaha za Rais lakini pia walikabidhiwa kitita cha sh. milioni 50 kusaidia maandalizi yao kuelekea mchezo muhimu dhidi ya Lesotho hapo Novemba 16 mwaka huu.

Rais Magufuli alitema nyongo kwa kuwanyooshea baadhi ya viongozi wanaoingia madarakani kwa maslahi yao binafsi hivyo kukwamisha maendeleo ya sekta hiyo ya michezo katika ujumla wake.

Kiongozi huyo mkuu wa nchi ameoneshwa kukerwa na hali ambayo ambayo anaamini ndiyo pia kuwa kiini cha kuwafanya wachezaji kupungua morali na hivyo kushindwa kujituma kikamilifu katiuka kutafuta ushindi.

Magufuli ana amini katika asilimia zote kuwa wachezaji wa Taifa Stars wana uwezo wa kufuzu fainali hizo zijazo hivyo kuwapa mtihani wa kuhakikisha wanafanikisha hilo ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wao lakini pia kuipeperusha vema bendera ya nchi.

Katika mkutanbo huo Rais magufuli aliangazia baadhi ya mambo aliyoyatilia mkazo katika mazungumzo yake ambayo kwa matazamo wake ndiyo hasa yanayochangia kupunguza kasi ya mafanikio katika mchezo wa soka.

Ushabiki

Hapa aliweka wazi ukereketwa wake katika soka japo amekuwa hapendi kujionyesha wazi wazi kutokana na kuvurunda kwa timu za Tanzania katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki.

Katika hali ya kawaida alifafanua mpenzi yoyote wa soka hawezi kufurahia timu yake kufanya vibaya bali kutaka kuona siku zote ikishinda.

Lakini matokeo mabovu ya mara kwa mara yamewafanya sasa mashabiki wa soka kutojitokeza waziwazi kushabikia timu kwa sababu hakuna furaha zaidi ya kushindwa. Alisisitiza yeye kama shabiki namba moja nchini hapendi kushindwa hivyo kuwataka kufanya yale ambayo mashabiki wanayahitaji.

Maadili

Suala hili liliwalenga zaidi viongozi ambao wamekuwa zaidi wabinafsi kuliko kuangalia maslahi ya mchezo husika na badala yake kuwa viongozi wengi wezi badala ya wazalendo.

Kuthibitisha hilo ndiyo maana TFF (Tanzania) ilikosa msaada wa fedha dola milioni tatu za kimarekani kutokana na ubadhirifu wa fedha uliowahi kufanywa na baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo miaka kadhaa iliyopita.

Akionekana kumuunga mkono Rais wa TFF, Wallace Karia alimtaka kiongozi huyo kusafisha viongozi wote wabadhirifu ili kujenga imani ya kuaminika miongoni mwa wananchi na wadau wote wa mpira.

Vilevile alisisitiza nidhamu kwa upande wa wachezaji ndani na nje ya uwanja kuwa nayo inajenga ari pamoja na ushindi hivyo kuwataka kulizingatia hilo.

Utawala

Katika hili kiongozi huyo alitahadharisha dhana iliyojengeka kuwa baadhi ya viongozi wamekwua na tabia ya kumuingia utendaji wa kocha hasa katika kupanga timu.

Alitaka kocha wa Taifa Stars aachwe atimize majukumu yake kwa kuzingatia taaluma yake ili iwe rahisi kumpima kutokana na mafanikio yake.

Atahadharisha

Rais alitoa msaada wa shilingi milioni 50 kwa timu hiyo ili kusaidia maandalizi ya mchezo wake unaofuata dhidi ya Lesotho mjini Maseru ambao ndiyo utakaotoa sura ya timu hiyo kama itakwenda Cameroon au la.

Alionya tabia ya baadhi ya viongozi kujazana katika misafara na kuwaacha wachezaji wakiwa wachache hivyo kuongeza bajeti na kutumia fedha nyingi bila mpangilio kutokana na kiasi kikubwa kwenda kuwalipia hoteli na posho. Alitaka kwa Taifa Stars hilo lisitokee.

Katika hili aliwanyooshea kidole TFF na kuwaonya katika hilo wasipokuwa makini katika matumizi hayo hatasita wakuaambia wazireje hizo fedha kwakuwa zimetokana na kodi ya watanzania.

Vilevile aliwakumbusha kutumia mfumo wa tiketi za kielektroniki hata katika viwanja vingine mbali na Taifa ili kupata mapato sahihi ikiwa ni pamoja na kulipa kodi ya Serikali kwa usahihi.

Ushindi

Rais Magufuli anaamini katika hilo kwa asilimia 100. Kwake anasema hana lugha nyingine zaidi ya neno ushindi kwa vile ana imani uwezo na sababu za kutimiza hilo vipo ndani ya uwezo wa timu hiyo.

 Muda

Alitahadharisha viongozi pamoja na benchi la ufundi kutumia vizuri muda uliobaki ukiwepo wa maandalizi ili kuhakikisha hesabu walizopiga kutaka kushinda mechi zao mbili zilizosalia dhidi ya Lesotho mwezi ujao na Uganda hapo Machi mwakani zinakamilika.

Alishauri pia kutokana na muda kuwa mfupi unaowakutanisha pamoja wachezaji wanaocheza ndani na wale wanaocheza nje ni vema benchi la ufundi likawatumia wachezaji wanaocheza ndani wenye uwezo saw ana wale wan je ili kuifanya timu kuzopeana na kuwa na ‘chemistry’ nzuri.

Kwake alichoona ni kuwepo kwa na umakini na mpangilio mzuri ili wote wapate muda wa kuunganika vizuri ili kupata matokeo chanya kwa timu katika upokeaji wa mafundisho.

 Uzalendo

Rais magufuli alitumia dakika kadhaa kufundisha somo la uzalendo kwa kumtaka kila mmoja kuwa na mapenzi ya dhati kwa nchi yake.

Alisema uzalendo unaleta mambo mengi sana kuweza kufanikiwa na kutolea mfano wakati wa mechi kati ya timu hiyo na Cape Verde mjini Praia wachezaji walishindwa kuimba wimbo wa taifa na kuumalizia na badala yake baada ya kumaliza ubeti wa kwanza wakapiga makofi ilihali ulikuwa haujamalizika hivyo kuonyesha wazi hata wimbo wao wa taifa hawaufahamu vizuri