Home Makala Kimataifa Julian Assange mwanahabari shujaa au wakala wa adui?

Julian Assange mwanahabari shujaa au wakala wa adui?

1143
0
SHARE


NA MITANDAO

Inadaiwa kwamba Julian Assange, aliyetolewa kwa nguvu kutoka ubalozi wa Ecuador jijini London wiki iliyopita baada ya miaka saba ya kukaa humo kama mkimbizi hakuwa mgeni mstaarabu kwa mtu yoyote.

Anadaiwa kupaka kinyesi kwenye kuta za ubalozi huo na kutomtunza paka wake na tabia nyinginezo mbaya, kwa mujibu wa Waziri wa Nchi za Nje wa Ecuadore.

Hata hivyo, wafuasi wake wanadai kwamba kufukuzwa kwake ubalozini hapo na kukamatwa na mamlaka za Uingereza ni ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa habari. 

Wengine wanaona hatimaye kukabiliwa na haki kwa mtu ambaye alihusika sana katika kutoa taarifa nyeti kuhusu nchi za magharaibi, ndizo zimeivuruga demokrasia ya Marekani. Je, Assange ni mwanahabari shujaa, mwanaharakati asiye na uangalifu, au ni wakala wa adui?

Hakuna shaka yoyote kwamba Assange na taasisi yake ya Wikileaks wamechapisha taarifa nyeti na za kusisimua zaidi katika muongo mmoja uliopita. Hizi ni pamoja na nyaraka zilizoibua madhambi makubwa ya Marekani nchini Iraq na Afghanistan – pamoja, kwa mfano, na kuwapo kwa idadi kubwa zaidi ya vifo na majeruhi nchini Afghanistan kuliko ilivyoripotiwa rasmi.

Mwaka 2010 Wikileaks ilifichua hazina ya zaidi ya nyaraka 250,000 za mawasiliano ya kidiplomasia za Marekani zilizoibiwa kwa msaada wa Chelsea Manning, wakati huo akiwa askari tu wa cheo cha chini kabisa katika jeshi la Marekani.

Labda kitu kibaya zaidi ni pale mwaka 2016 Wikileaks ilipokuwa ni njia ya mawasiliano kwa niaba ya barua pepe zilizodukuliwa kutoka chama cha Democratic, barua pepe ambazo huenda zilibadilisha mwenendo mzima wa uchaguzi wa Marekani uliomuingiza Donald Trump Ikulu ya nchi hiyo.

Mashabiki wa Assange wanauliza: kitu gani kinachomtofautisha yeye na gazeti la New York Times ambalo lilichapisha nyaraka za siri – “Pentagon Papers” mwaka 1971 zilizotoa habari za kusisimua kuhusu Vita ya Vietnam? 

Lakini pia kwa mtazamo mwingine, Assange alikuwa hafanyi zaidi ya kufuata nyayo za taasisi maarufu za habari ambazo zilikuwa zinatoa majukwaa kwa wanaharakati waliokuwa wanatoa siri za serikali na kufaidi kinga ya Marekebisho ya Kwanza (First Amendment) ya Katiba ya Marekani wakati wakifanya hivyo. 

Hata hivyo kuna sababu kadha kwanini aliyofanya Assange yanamuweka katika jamii tofauti. Tuhuma za Marekani dhidi yake zinaonyesha tofauti moja. Assange anatuhumiwa siyo tu kwa kuchapisha taarifa zilizodukuliwa – kwani hicho ndicho kila siku wanahabari hufanya – lakini pia kumsaidia Chelsea Manning kupata nenosiri (password) ya kuingia katika mtandao wa siri wa Pentagon (Makao Makuu ya Jeshi la Marekani) na hivyo kumfanya kuwa mshirika mwenza wa njama katika udukuzi.

Wanahabari wengi huvishawishi vyanzo vyao hata kufanya kitu cha hatari ili kupata taarifa zaidi – kama vile Assange alivyofanya kwa Manning.

Wizara ya Sheria wakati wa utawala wa Rais Barack Obama ilikiri kwamba isingeweza kumfugulia mashitaka Assange pasipo kuharamisha kitu kinachofanyika kikawaida katika medani ya uandishi wa habari.

Lakini wizara hiyo ilitoa onyo, kwa sababu zinazoeleweka kabisa, kwamba wanahabari hawana hati miliki – kweamba kama walidhaniwa kuwa ni mawakala wa mamlaka wa nchi za nje, au kula njama katika kufanya jinai na mamlaka hizo, wanaweza kushitakiwa. 

Baadhi ya walichokifanya Wikilieaks huenda yalikuwa karibu na kuvuka mstari huo – ingawa uhusika binafsi wa Assange katika hayo haujulikani kikamilifu.

Kwa mujibu na mashitaka yaliyotayarishwa na Mwanasheria Maalum Robert Mueller, mwaka 2016 Wikileaks iliwashawishi makachero wakiwa na majina ya b andia kutuma barua pepe kuhusiana na aliyekuwa katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa kugombea urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton. Lengo lilikuwa ni kuyumbisha uteuzi huo ili kumnufaisha mpinzani wake Bernie Sanders. 

Lakini hata hivyo mnufaika halisi alikuwa ni Donald Trump. Mwaka ule Trump alikiri kupenda kusoma Wikileaks, lakini sasa hivi anasema Wikileaks kati siyo mapenzi yake.