Home KIMATAIFA Kampuni ya Urusi yakosolewa kwa kuwalipa wanawake kuvaa sketi

Kampuni ya Urusi yakosolewa kwa kuwalipa wanawake kuvaa sketi

1161
0
SHARE

NA MITANDAO

Kampuni ya Urusi imekosolewa sana kwa kuwalipa wanawake pesa za ziada ili wavae sketi au gauni wawapo kazini.

Kwa mujibu wa BBC ilieleza kwamba kampuni hiyo Tatprof, ambayo hutengeneza bidhaa za aluminiamu inaendesha kampeni ya “muonekano wa mwanamke”  hadi Juni 30, mwaka huu.

Wafanyakazi wanawake wanaovaa sketi “ambazo zina urefu usiozidi sentimita tano juu ya magoti “wanalipwa dola $1.50, zaidi juu ya mshahara wao wa kawaida ambazo ni wastani wa Sh 3,500.

Ili kupata fedha hizo za ziada, wanawake wanatakiwa kutuma picha zao kwa kampuni hiyo.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wameonyesha kukasirishwa na kitendo hicho huku baadhi wakielezea hatu ya kampuni kuwa “udhalilishaji mkubwa wa wanawake”.

Blogi maarufu inayoendesha harakati za wanawake na mwandishi wa habari maarufu nchini humo Zalina Marshenkulova wameelezea hatua hiyo ya kampuni ya Tatprof kama “taarifa ya enzi ya zamani” kwenye ukurasa wa Instagram.

Kampuni hiyo,ambayo iliuza bidha za michezo ya Olyimpiki ya majira ya baridi mnamo 2014 katika mji wa Sochi na katika kombe la dunia la mpira wa miguu la 2018, imeviambia vyombo vya habari vya Urusi kuwa inakama shutuma za ubaguzi wa kijinsia na akasema wanawake 60 tayari wameshiriki katika kampeni yake.

“Tulitaka kuzifanya shule We wanted to brighten up our work days,” alisema Govorit Moskva msemaji wa kampuni katika mahojiano na kituo cha radio

“Asilimia 70 ya wafanyakazi wa kiwanda chetu ni wanaume . Aina hizi za kampeni zinatusaidia kupumzika. Hii ni njia ya kuifanya timu ya wafanyakazi iwe na umoja

“Wanawake wengi huvaa suruali kazini, ndio maana tunatumaini kampeni yetu itawaelewesha wanawake, na kuwaruhusu kujihisi ni wanawake na kujihisi wenye furaha wanapovaa sketi au gauni.”

Watumiaji wa Twitter nchini Urusi hawajafurahia kampeni hiyo.

“Kampuni hailioni hili kama ni ya kuwadhalilisha wanawake na inaamini kwamba kiwanda kimebadilika ‘,” ilielezea kwenye ujumbe wake wa Tweeter @shagaliev97.

“$1.50 za ziada kwa wanawake wanaovaa sketi na kujipodoa … Kuifanya siku yao kuwa yenye mwangaza kwa wafanyakazi wenzao wa kiume ,” iliandikwa tweeter nyingine .

“Jamani, kwanini sisi wanawake tunahitajika wakati tunapoweza kuwaridhisha wanaume kwa ajili ya pesa?” walihoji

Kampuni hiyo ilikuwa imepanga matukio mengine mwezi wa Juni iliyoita “kuwa mwanamke “, ikiwamo mashindano ya michezo mbalimbali.

Anastasia Kirillova, kutoka Idara ya Utamaduni wa Kampuni hiyo na mawasiliano ya ndani amesema kuwa wazo la kampeni hiyo lilitoka kwa Mkurugenzi wake mkuu Sergei Rachkov.

“Anahofu sana juu ya suala hili – majukumu yaliyochanganywa ya kijinsia,” aliiambia wavuti binafsi ya habari Business Online.

“Na kusema kweli anataka kuimarisha uanauke katika kila mwanamke muajiriwa wa kampuni, ili wanawake vijana wasiwe wanakata nywele kama wanaume, wasiwe watu wa kuvaa suruali wakati wote, iliwa wajihusishe na ubunifu wa kazi za mikono yao, na waonyeshe uchangamfu wao wanapowalea watoto wao.”

Kampuni pia inafanya mashindano ya michezo kwa ajili ya wafanyakazi wake wa kiume.

Mwisho