Home Burudani KAYUMBA AUKATAA MUZIKI WA KIKI

KAYUMBA AUKATAA MUZIKI WA KIKI

2160
0
SHARE

NA JEREMIA ERNEST

UNAPOTAJA wasanii wa Bongo flava watano nchini ambao walipata umaarufu wakiwa na umri mdogo kutokana na ubora wa kazi zao, huwezi kuacha kulitaja jina la Kayumba Juma,  ‘Kayumba wa BSS’,

Ilikuwa ni mwaka 2015, Kayumba alipoibuka kidedea katika mashindo ya kusaka vipaji yanayofahamika Bongo Star Search, yaliyoasisiwa na Mkurugenzi wa Bench mark  Production, Rita Paulsen.

Ushindi huo ulimfanya Kayumba kubeba kitita cha Sh milioni 50 zilizotolewa na waandaaji.

Baada ya shindano hilo, staa huyo aliachia nyimbo kadhaa, lakini kwa bahati mbaya baadhi hazikufanya vizuri sokoni, ikichangiwa na uchanga wake na pamoja na menejimenti yake kushindwa kutimiza majukumu yao.

Akifanya mahojiano na Rai nyota huyo anafunguka mambo kadhaa kuhusu maisha yake ya muziki alipotoka, alipo na matarajio yake kwa siku zijazo.

Lakini pia maisha yake ya kila siku.

 “ Kiukweli nilifikiria muziki wangu ukiwa chini ya mtu mkubwa anayefahamika itakua rahisi mimi kukua  kufanikiwa lakini mwanzo haikuwa hivyo,  nilijaribu kuwa chini ya watu tofauti tofauti mastaa, lakini sikufanikiwa kutimiza malengo yangu.

“Mwanzo kabisa nilikuwa chini ya ‘producer’(mzalishaji) Mazuu, nikatoka kwake nikajaribu kwa Jobiso wa THT, nikawa pia chini ya Abbah kama masanii wa studio lakini kote huko niliambulia kurekodi ngoma na kufahamiana tu na watu,” anasema.

Anasema baada ya kuhangaika, aliibuka upya na kutambulisha nyimbo kadhaa ambazo zilifanya vizuri sokoni na kumfanya arejea kwenye chati kama alivyong’ara akiwa BSS.

Anazitaka miongoni mwa nyimbo zilizompaisha kuwa ni Mazoea, Tuongee,  Maumivu, Bonge la Toto na Wasi Wasi  zote.

Anashukuru Mungu mashabiki wake kwa kumpokea kwa mikono  miwili.

“Aina yoyote ya muziki ninaoutambulisha wanaupokea, kikubwa ubunifu wa kukonga nyoyo zao,”anasema Kayumba.

Anasema ana mpango wa kubadili  uimbaji wake kutoka  nyimbo za kulalamika na kufanya aina nyingine ya uimbaji.

“Tayari  nina nyimbo ziko  tayari,muda si mrefu nitazitambulisha,”anasema.

Anasema kwa sasa muziki unahitaji uwekezaji  wa kutosha, huku akidai kuna vitu vingi anatamani kuvifikia ikiwemo kufanya  nyimbo za kushirikiana na  wasanii wakubwa duniani pamoja  na watayarishaji mahiri.

 “Wasanii ni wengi ninaohitaji kufanya nao kazi kama Wizz Kid, Panto Raking, Vannesa Mdee, Justin Bieber, Ally kiba, na RayVann.

“Hawa wote ninaowahitajia natakiwa niwe kiasi kikubwa cha fedha kwani kipato changu kwa sasa bado hakitoshelezi, lakini naamini ipo siku nitafikia malengo,”anasema Kayumba.

Anazugumzia soko la uuzaji wa muziki kwa kusema kwa kupande wake amejikita zaidi katika mitandao ya kijamii kuliko kufanya shoo.

“Muziki umetanuka sana kuna vitu vingi vinavyo tuingizia pesa wasanii kuliko shoo, kama vile kupitia mitandao ya YouTube, blogs kubwa tulizojiunga nazo mfano Boomplay, Caller tune na nyingine nyingi,”anasema.

 Kutokana na ukaribu wake na Ali Kiba unaotokana na biashara ya muziki unamfanya msanii huyo kuamini kuwa yupo karibu  kuwa chini ya lebo ya Kings Music.

Siku za karibuni kumekua na tetesi kuwa, staa huyo ana uhusiano wa mapenzi na muigizaji wa filamu za Bongo, Irene Uwoya.

Kayumba anakanusha  kuwa na uhusiana na nyota huyo wa filamu na kusema mwanadada huyo ni shabiki yake wa muziki na si vinginevyo.

“Mara kwa mara tunaonana kwa ajili ya kujadili mambo ya kazi na si mapenzi ama kutengeneza kiki kama walimwengu wanavyo sema.

“Muziki wangu hauhitaji kiki, unakwenda wenyewe bila vinogesho nje kwa kua una ujumbe, hivyo Irene hawezi kunipa kiki pia si mpenzi wangu,”anasema.

Anazungumzia madai ya kwamba alimfanya fujo msanii wa filamu, Steve Nyerere ambaye ni miongoni mwa watu wanaomtuhumu kwamba ana uhusiano na Irene.

“Sikuwahi kumfanyia fujo, tulikutana Lamada hotel ambako nilikwenda kumuona Irene, lakini nilipofika nilikuta wanarekodi video ndipo Steve alimzuia kwa muda.

“Steve hakuwahi kunifukuza, watu walitafsiri vibaya, alinizuia nisipite wamalize kurekodi video, walipoamaliza nilipita nikaendelea na kilichokuwa kimenipeleka pale,” anasema Kayumba.