Home kitaifa Kipele kilichodekezwa, jipu kwa Magufuli

Kipele kilichodekezwa, jipu kwa Magufuli

1770
0
SHARE

rai hii safi.inddNA FRANKLIN VICTOR

SERIKALI iliyomaliza muda wake ina mengi ya kusemwa katika kumbukumbu, kwa namna nyingi. Lakini moja kati ya vitu
tofauti kwayo ni uwepo wa ‘ukweli mgumu’ mwingi utakaozungumzwa juu ya utendaji wake, uzito na
uharaka wa maamuzi. Safari za nje ya nchi alizozizungumza Rais Dk. John Magufuli, kwenye hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la
11 ni mwanzo tu.

Safari nyingi zilizofanywa na wakubwa zimethibitika kutofaidisha
nchi ipasavyo ndiyo sababu amezifuta.
Miaka michache ijayo mambo yaliyofanywa dhahiri au kwa siri na serikali iliyopita yatajadiliwa zaidi kama ilivyosemwa serikali ya awamu ya tatu.

Uchambuzi wa ubutu na ufanisi wa serikali ya awamu ya nne utaonwa ndani ya kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na mwanasayansi msomi na mchapakazi asiyesita kufanya maamuzi, Rais Magufuli.

Nashawishi kusadiki kwamba kipele kupata mkunaji ni tofauti mno na jipu kupata mtumbuzi/mtumbuaji. Mkunaji hukiridhisha kipele, hukilea na kukibembeleza kipele kwa kukipapasa na mikuno ili kitulie, mwenye nacho aliwazike.

Lakini mtumbuaji majipu hasa yule mahiri ni adui kwa jipu kwa kuwa nia yake ni kuliua, kuliondosha jipu ili mwenye nalo apate ahueni, arudiwe na raha za awali kabla hazijatiwa karaha na
uwepo wa jipu. Ifae kusadiki, mkunaji kipele anakosa ujasiri wa kuamua anapopewa jipu atumbue, lakini mtumbuaji majipu anaweza kukipapasa kipele kama atalazimika kufanya hivyo.

Wakati wa kampeni, Rais Magufuli alisema anawachukia watendaji wa serikali wasiotimiza wajibu wao, majukumu yao na kuahidi atalala nao mbele kwa kuwashughulikia. Hili ameanza kulitekeleza ambapo miongoni mwa mashuhuda wazuri ni Rished Bade, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA.

Wananchi wanafarijika, wanashawishika kwa kuona hatua anazochukua Rais wao. Wananchi wanatiwa moyo na mwanzo mzuri wa Rais Magufuli anayetenda zaidi, anayefanya maamuzi
magumu bila kuongea sana huku akimuacha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, afanye kazi yake kwa nafasi yake stahiki.

Hata Waziri Mkuu Majaliwa Kassim hakurupuki, anajipanga, anajua anachofanya. Kwa mwendo huu na kama hautabadilika,
nchi itaacha kutambaa na kuanza kutembea, kukimbia na
hata kuruka ndani ya kipindi kifupi.

Katika kuhakikisha mambo hayakwami hata palipo ukata na serikali inajimudu, Rais anachukua tahadhari za kubana matumizi na kuokoa kwa kadri awezavyo fedha za umma kwa kufuta matumizi yasiyo ya lazima.

Serikali imefuta sherehe za kula, maadhimisho ya hadhira viwanjani, kupiga marufuku ununuzi wa zawadi za sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kutumia fedha za umma na kufuta uzinduzi na maadhimisho kuelekea siku ya ukimwi.

Wananchi wanatamani siku zijazo Rais afute mbio za mwenge ambazo hutumia fedha nyingi za umma na kukwamisha matumizi ya miradi mingi kwa kisingizio cha eti inasubiri kuzinduliwa wakati wa mbio za mwenge. Wakati akilizindua Bunge hilo Rais Magufuli alisema atafanya kazi ngumu ya kutumbua majipu yote yanayokwamisha maendeleo ambayo yawezekana miaka
iliyopita yalionwa kama ‘mapele’ tu.

Kwa Rais Magufuli, maajabu ya twiga kupanda ndege, makontena yenye meno ya tembo kwenda kukamatiwa ughaibuni, biashara ya dawa za kulevya, wizi, uuzaji wa mashirika kama UDA kinyemela, urasimu, utendaji wa kimazoea na yafananayo ni majipu yanayohitaji na kulazimu kutumbuliwa, kukamuliwa.

Rais Dk. Magufuli huyu na Waziri Mkuu Majaliwa wamefanya safari za kushtukiza na kutoa maamuzi mwafaka pasi kupoteza muda.
Kwa mfano; tatizo sugu la wizi (wenyewe wanasema upotevu), wa mali bandarini Dar es Salaam limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu na watumiaji wa bandari hiyo, hasa wafanyabiashara kiasi
cha wengine kuamua kuisusa na kutumia bandari nyingine.

Unakuta mtu anapata hasara eti kwa uamuzi wake mzuri wa kufanya biashara na mamlaka ya bandari Tanzania – TPA yenye watendaji wanaoendekeza mazoea ya kirasimu, rushwa na ulafi . Hii si sawa.

Pia Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA haikukosa kubebeshwa lawama kwa kushiriki au kuzembea kunakowezesha kodi
kukwepwa. Inawezekanaje makontena 349 kupotea kirahisi
tu halafu watendaji wanabaki kusema eti uchunguzi unaendelea.

Eti kodi bilioni 80 zinapotea hivi hivi huku hospitali ya taifa Muhimbili ikiwa na mashine za MRI na CT Scan zinazochechemea kiutendaji.

Majipu yanapotumbuliwa damu lazima itoke kabla ya mwenye jipu kupona.
Masuala kama serikali kuuziwa mabehewa chakavu yaliyonadhifi shwa kwa rangi, vichwa vya treni mtumba, uwepo wa kodi nyingi
zinazoelekea kukomoa badala ya kuwezesha wananchi kushiriki katika kukuza uwezo wa serikali na uchumi wa nchi, serikali kulimbikiza madeni, kutolipa mafao stahiki ya wastaafu kwa wakati na mengi yafananayo ni baadhi ya majipu yanayosubiri kutumbuka yenyewe mapema kama si kulazimu kutumbuliwa naye Dk. Magufuli aliye mamlakani kwa sasa.

Utitiri wa wizara hautarajiwi kujirudia kama rais Magufuli amedhamiria serikali yake kuwa ya mfano wa pekee
nchini Tanzania tangu kujipatia uhuru.

Wingi wa wizara na watendaji si ufanisi bali ulaji na matumizi mabaya ya mamlaka.
Inawezekana kabisa waziri mmoja mahiri kuwasimamia makatibu wakuu hata watatu bila mtetereko kiufanisi.

Yale mambo ya kulipana fadhila kwa vyeo vya umma yalazimu kuepukwa ili kupunguza ‘majipu’ na kuifanya serikali ya Magufuli kuwa bora, yenye kukidhi matarajio ya mabadiliko yanayotakwa sana na Watanzania.

Rais ateue watu makini wapya atakaowaamini, wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa, wakurugenzi, wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa umma ambao hawatamuangusha wala
kuwachanganyia habari wananchi.

Ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
– CAG imekuwa ikionesha ubadhirifu mkubwa kila mwaka
wa bajeti.

Jipu hili bila shaka liko mbioni kutumbuliwa. Haitapendeza kusikia tena eti halmashauri zimeendelea kufuja fedha huku wananchi wakilazimika kuchangia maendeleo yao, kuchangia ujenzi wa maabara, vyumba vya madarasa, vyoo, hadi eti mlinzi wa shule ya kata! Kwa kuwa Rais amesisitiza dhamira ya serikali kutoa elimu
bure ya msingi hadi sekondari kidato cha nne, wananchi wanasubiri kupata ahueni hii pindi ianzapo Januari 2016.

Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa rais Dk. John Magufuli si ya kipele kupata mkunaji. Ni serikali, kwa mujibu wake mheshimiwa rais, ya jipu kupata mtumbuaji. Kila mwenye dhima akitimiza wajibu na majukumu kwa weledi, uzalendo, ufanisi,
wigo wa kikatiba, sheria na kanuni, na kujali muda; majipunchi
yote yatatumbuliwa na mengine kutumbuka yenna wananchi wataipata tena raha kiuchumi na nafuu kimaisha.