Home Latest News KIVULI CHA SWITZERLAND CHAMKIMBIZA MSWATI SWAZILAND

KIVULI CHA SWITZERLAND CHAMKIMBIZA MSWATI SWAZILAND

5513
0
SHARE
NA HILAL K SUED  |

Wiki iliyopita Mfalme Mswati III wa Swaziland alibadilisha jina la taifa lake kutoka Swaziland na kuibatiza jina jipya la eSwatini.

Uamuzi huo ulifikiwa wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya kuzaliwa kwake na pia miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo.

Wachambuzi wa mambo barani Afrika wanaamini uamuzi na sababu za Mfalme Mswati za kubadili jina la nchi yake, hazina mashiko sana badala yake ni kama ameamua kukikimbia kivuli cha nchi ya Switzerland.

Kabla ya kufikia uamuzi wa kubadili jina hilo, tayari Mswati alishaanza kulitumia jina hilo ‘eSwatini’ lenye maana ya “ardhi ya Waswazi’.

Mfalme Mswati amekuwa akilitumia jina hilo kwa miaka mingi, hata alipokuwa akihutubia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka jana na katika ufunguzi wa Bunge nchini mwake mwaka 2014.

Sababu kuu aliyotoa ya kubadilisha jina la nchi yake ni kwamba kila aendapo katika mikutano ya kimataifa, mataifa mengine yamekuwa wakilichanganya taifa lake na nchi ya Switzerland iliyopo Ulaya.

Kuna baadhi ya wananchi katika maoni yao wamesema badala ya kushughulika na jina la nchi yake, Mfalme huyo alipaswa kupasua kichwa ni namna gani anaweza kuimarisha uchumi wa nchi hiyo unaodidimia siku hadi siku.

Swaziland ni nchi ya karibuni tu, katika milolongo ya nchi kadha Barani Afrika na kwingineko duniani ambazo zimebadilisha majina kwa sababu mbali mbali. Sababu hizo ni pamoja na matokeo ya vita zilizopiganwa, kuungana mataifa mawili au kujitenga kwa nchi.

Katika Bara la Afrika nchi zilizobadilisha majina yao ni pamoja na Ghana (ambayo zamani iliitwa Ivory Coast), Burkina Faso (Upper Volta), Benin (Dahomey) na Malawi (Nyasaland).

Nyingine ni Zambia (Northern Rhodesia) Zimbabwe (Southern Rhodesia), Burundi (Urundi), Lesotho (Basutoland) na Botswana (Bechuanaland).

Mwishoni mwa miaka y 60 nchi ya Congo maarufu Congo-Kinshasa wakati ule ilibadilshwa jina na kuwa Zaire. Rais Mobutu Seseko wakati huo alisema sababu ya kufanya hivyo ni kutofautisha na nchi jirani yake ya Congo-Brazzaville. Hata hivyo jina la Zaire lilidumu kwa takriban miaka 20 tu na baada ya kuondoka kwa rais huyo likarejeshwa jina la zamani la Congo.

Baada ya kuingia utawala wa wazalendo Afrika ya Kusini mwaka 1994, iliamuliwa nchi hiyo kuendelea kutumia jina hilo hilo – Afrika ya Kusini ingawa kulikuwapo wito wa kuitwa jina la kizalendo la Azania. Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 na kuitwa Tanzania.

Kwingineko duniani, katika miaka/miongo ya karibuni nchi zilizobadilisha majina yao ni pamoja na Iran (zamani ikiitwa Persia hadi mwaka 1935), Ethiopia (Abyssinia hadi 1922), Sri Lanka (zamani Ceylon), Myanmar (Burma) na nchi ya Amerika ya Kati ya Belize (zamani British Honduras).

Kwa ujumla mataifa mapya yamekuwa yakiibuka duniani mara kwa mara. Wakati Karne iliyopita (karne ya 20) ilipoingia kulikuwa nchi chahce tu zilizikuwa huru hapa duniani, lakini leo hii ziko karibu nchi 200.

Pale taifa linapoanzishwa, hudumu kwa kwa muda mrefu hivyo kutoweka kwa taifa huwa siyo kitu cha kawaida. Imetokea mara chache sana katika kipindi cha karne moja iliyopita – hutoweka kabisa kutoka uso wa dunia, yaani serikali, bendera na kila kitu.

Lakini wakati huo huo nchi mpya huibuka ambazo awali hazikuwepo kama nchi huru hususan kutokana kujitenga au vita. Barani Afrika ni Eritrea (iliyokuwa sehemu ya Ethiopia iliyojitenga mwaka 1992) na Sudan ya Kusini iliyokuwa sehemu ya Sudan hadi, 2011.

Huko barani Asia nchi ya Bangladesh, zamani sehemu ya Pakistan, iliibuka mwaka 1972 baada ya kujitenga. Na bila shaka wengi wanafahamu kwamba hata Pakistan yenyewe haikuwapo kama nchi hadi baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Ilikuwa ni sehemu ya India ambayo ilikuwa koloni la Uingereza na kabla ya kutoa uhuru, ilibidi Pakistan imegwe kutoka India kutokana na sehemu hiyo kuwa na idadi kubwa ya Waisilamu.

Na huko huko bara Asia, nchi iliyokuwa ikiitwa Vietnam ya Kusini (South Vietnam) ilifutika rasmi mwaka 1975 baada ya majeshi ya Kikomunisti ya iliyokuwa Vietnam ya Kaskazini kuyashinda yale ya Vietnam ya Kusini yaliyokuwa yanasaidiwa na Marekani.

Hali kadhalika nchi iliyokuwa ikijulikana kama Tibet (mpakani kati ya China na India) ilikuwapo kwa zaidi ya miaka 1,000 ingawa ilikuwa nchi huru mwaka 1913. Msururu wa utawala wa Dalai Lama ulidumu hadi 1951 pale kuliubuka mzozo na watawala wa China ya Kikomunisti ambapo majeshi ya Mao Zedong yaliivamia nchi hiyo ndogo na kuikalia na hivyo kusitisha uhuru wa muda mfupi wa nchi hiyo. Mwaka 1959 China iliifanya nchi hiyo kuwa jimbo rasmi la nchi hiyo.

Kwingineko duniani nchi huru zilizokuja kuibuka na ambazo awali hazikuwapo ni pamoja na Uturuki (zamani sehemu ya enzi ya Ottoman (Ottoman Empire) hadi baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia.

Nchi za Serbia, Croatia, Bosnia-Herzegovina, Moldova, Macedonia, na Slovenia zilikuwa sehemu ya Yugoslavia iliyosambaratika katika miaka ya 90 kutokana na kuanguka kwa himaya ya itikadi ya Kikomunisti Ulaya ya Mashariki iliyokuwa ikiongozwa na Urusi ya Kisovieti. Hali kadhalika Jamuri ya Czech na ile ya Slovakia kabla ya miaka ya 90 ilikuwa nchi moja ya Czechoslovakia.

Na Urusi ya Kisovieti yenyewe (Union of Soviet Socialist Republics –USSR) nayo baada ya kusambaratika ikazaa nchi huru 15 zikiwemo Armenia, Georgia, Ukraine, Latvia, Lithuania, Azerbaijan, Kazakhstan, Tajikistan, Belarus, Turkmenistan, Uzbekistan na Kyrgyzstan.

Kusambaratika kwa Urusi ya Kisovieti ambako kulikwenda sambamba na kusambaratika kwa taifa la Yugoslavia (hali kadhalika kusambaratika kwa Czechoslovakia) kulisababishwa na sababu moja kuu – kwamba mataifa hayo yaliyoibuka hayakuwa na lugha moja kwa wananchi wote, utamaduni mmoja na kwa ujumla hayakuwa yana mahusiano yoyote ya kihistioa au kivingine na mamlaka kuu – yaani mamlaka ya Kremlin Moscow (kuhusu Urusi-USSR) au ile ya Belgrade (kuhusu Yugoslavia) isipokuwa tu ile itikadi ya Kikomunisti.

Hivyo ilikuwa rahisi kwa mataifa hayo kupukuchika kwani ilitakiwa kitu kidogo tu cha kutoa msukumo. Hicho kitu ni kuanguka kwa ukuta wa Berlin, Ujerumani ya Mashariki, ukuta uliokuwa umeugawa mji kati ya Ujerumani ya Mgharibi nchi iliyokuwa huru iliyokuwa ikufuata itikadi ya kibepari na ile ya mashariki iliyokuwa ikifuata itikadi ya Kikomunisti, hali iliyokuwapo tangu baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya pili mwala 1945.

Hata hivyo ukuta huo ulijengwa mwaka 1961 baada ya kuibuka wimbi ka wakazi wa Berlin ya Mashariki kukimbilia magharibi.

HISTORIA YA SWAZILAND

Uswazi maarufu kama Swaziland, kwa lugha ya Kiswazi sasa itatambulika kama eSwatini, kwa lugha ya Umbuso itatambulika kama weSwatini ni nchi ndogo ya Afrika ya Kusini isiyo na pwani katika bahari yoyote.

Imepakana na Afrika Kusini na Msumbiji, Mji mkuu ni Mbabane.Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Waswati walianzisha ufalme wao katikati ya karne ya 18 chini ya Ngwane III; mipaka ya sasa ilikubalika mwaka 1881.

Baada ya vita kati ya Waingereza na Makaburu, Swaziland ilukuwa nchi lindwa ya Uingereza tangu mwaka 1903 hadi 1967.

Chini ya mfalme Sobhuza II aliyetawala kwa muda mrefu sana (1921-1982), Swaziland ilipata uhuru Septemba 6,1968.

SIASA

Uswazi tangu mwaka 1986 inatawaliwa na mfalme Mswati III. Mfalme anapingwa mara nyingi kwa sababu anatumia pesa nyingi kwa ajili yake binafsi ilhali wananchi ni maskini sana. Kwa muda mwingi wa uhuru wa nchi (6 Septemba 1968) Katiba imesimamishwa, na mfalme ametawala peke yake.

WATU

Wakazi wengi ni wa kabila la Waswati na kuongea lugha ya Kiswati ambayo ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza.

Upande wa dini, asilimia 83 ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, hasa Waprotestanti, lakini pia Wakatoliki wapo kwa asilimia 20. Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni asilimia 15 huku Waislamu wakiwa asilimia moja.

AFYA

Uswazi ni kati ya nchi zilizoathiriwa zaidi na Ukimwi duniani, umri wa wastani unafikia miaka 32.62 pekee kwa sababu ya vifo vingi (64%) vinatokana na ugonjwa huo

MSWATI APINGWA

Mwaka 2011 wakati huo akiwa amebakiza siku mbili kabla harusi ya mwana mfalme wa Switzerland, William na mchumba wake Kate Middleton, mam ia ya raia wa nchi hiyo na wanaharakati wa kutetea haki sawa, walifanya maandamano mjini London.

Watu hao walikuwa wakipinga ujio wa Mfalme Mswati ambaye alialikiwa kuhudhuria harusi hiyo.

Walisema safari yake itagharimu nchi hiyo maskini fedha nyingi ambazo bora zingetumika kufadhili huduma za afya na maji nchini mwake.